Habari za asubuhi wanajamii,
Hii ya vijana wengi wake kwa waume kubeba mabegi mgongoni, hata sielewi huwa yanakuwa na nini, utafikiri mtu yupo safarini. Huwa nashuhudia hata wata wafanyakazi wenzangu utakuta anakuja na begi mgongoni akifika analiegesha hadi jioni wakati wa kuondoka analibeba sometimes mnapanda daladala moja haendi kokote zaidi ya nyumbani.
Sasa mtu unabaki unajiuliza hilo begi lina nini ndani? Sijui huwa mnachukua nguo, vitabu au nini? Kilichonifanya niandike humu ni ile kero tunayoipata kwenye mabasi hasa haya ya mwendo kasi. Watu wanaingia na mabegi mgongoni hajali kama linamsukuma mtu mwingine upande wa pili.
Punguzeni kuchukua mabegi imekuwa kama fashion....