Vijana hasa wanachuo mnaoingia mitaani, hizi ndio mishe za uhakika na rahisi kujifunza kupata hela ya kujitunza, achaneni na visivyo na uhakika

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
N:B.. fikiria kwanza kupata hela ya kujitunza kuweza kusurvive mtaani kabla ya kufikiria luxury needs, ni pesa inayoweza kukutoa hata hapo nyumbani kwenu kama unataka kuondoka

Huwa naona kuna vijana wanashauriana kupiga mishe sijui za mtandaoni na upatu, hizo mishe huwa hazina uhakika japo wapo wanaozipiga lakini katika 10 unakuta zinaowatoa ni wawili tu.

Leo naweka hapa mishe ambazo unajifunza fasta, unaweza kuanza haraka, zina mitaji ya kawaida na ukianza unaanza kupiga pesa kesho yake...

Kukaanga chipsi, hizi chips zina wateja wengi tu, ni rahisi kujifunza na mtaji wake ni average kuumudu pengine hata ukiuza simu yako unaanza, cha muhimu uwe na constant supply ya viazi.

Kunyoa nywele, ni ujuzi ambao unaweza kujifunza ndani ya mda mchache, ukishajifunza ingia kitaa
 
Izo chips kwa Dar watapiga pesa maana izo foleni kweny vibanda vya chips sio wanaume wala wanawake watu nyomi.
 
Back
Top Bottom