Karibuni tuzungumzie fursa za kutengeneza pesa ya uhakika kwa internet nje ya vitu kama forex, kubeti na michezo ya upatu

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Maada hii haihusiani na forex, kubeti, michezo ya upatu, n.k.


Dunia ya sasa imekuwa sana kiteknolojia hasa kwenye upande wa internet na kuna fursa zipo za kupiga hela za uhakika, Fursa hizi zimefanya watu wajiajiri rasmi mitandaoni, Kwenye majiji kama Arusha kuna watu wa nje ya nchi wanaishi kwa muda mrefu na kazi zao rasmi zipo mitandaoni, huwa wanaitwa Digital Nomads, Hawa hata waende kuishi huko Namtumbo wanachohitaji ni mtandao na Laptop tu kuingiza pesa.

Binafsi nimepiga ka research kidogo nimpata mwanga walau kujua kwamba kuna aina hizi za njia za uhakika

Online Gigs - hapa kuna mitandao inawakutanisha wenye ujuzi wa kufanya kitu online na wale wanaohitaji huduma yao, mfano kuna gigs za kutafsiri kiingereza kuja kiswahili, kuchapa maneno yaliyoandikwa, kuchora ramani kwa software, graphics designing, n.k. muhitaji anaweza kuwa huko London Uingereza ila anaefanya kazi yupo Dar-es-Salaam, Baada ya kazi kila mtu anachukua chake, Mitandao maarufu ni kama Upwork na Fiverr.

Affiliate marketing - Hapa ni kuwa dalali wa bidhaa,, Mfano kama bidhaa inauzwa elf 60 unapewa elf 5 .. faida yake ni kwamba haususiki na uzalishaji wa bidhaa, hauhusiki kuwapa guarantee wateja, hauhusiki na castomer care ya bidhaa, hayo yote ni juu ya mwenye bidhaa,,

Blogging - Hapa unakuwa na blog yako mfano blog ya udaku au michezo, kwa siku unaweza kupata wasomaji wa umbea elf 50 ama wasomaji elf 80 wa yaga / simba, unaweza kuweka matangazo ya makampuni kama google na taboola, kwa siku si haba ukawa unaingiza hata elf 40,

Youtube - hii mishe ilikuwa safi sana enzi hizo mabando bei chee kuna views za kumwaga, watu kama kina millard walipokuwa kwenye peak 2013 hadi 2017 kabla ya channel za youtube kujaa kuna tetesi walikuwa wanabonda takribani milioni 20 kila mwezi, hakuna kiwango cha uhakika cha malipo ya views, ila kwa haraka haraka kwa views elf 1 unaweza kulipwa shilingi elf 2, hapa unaweza kuweka videos kibao ili kwa mwezi upate hata jumla ya views laki 5, Ninawajua vijana waliobadili maisha kwa hii youtube hasa baada ya 2017 channel zilivyoanza kujaa.

Magroup ya simulizi - Kama ni mpenzi wa siulizi nadhani hii inaweza isiwe ngeni, Ni kwamba mtu mwnye kipaji cha kusimulia anakuwa na wafatiliaji wa simulizi zake, anatengeneza group la kuweka simulizi zake na anaanza kuwachaji wasomaji wastori zake bili ya kila mwezi, Mfano kwenye group tunaweza kuwemo watu elf 1 na kila mtu ni lazim alipie elf 2 kwa mwezi

Ningependa tupeane ramani ya haya mambo
 
Siti ya mbele
Tutoane huku mashimoni aisee, Pesa za mzungu zinatupita kizembe sana, huwa naona kuna madogo nchi za nje wanalaza hadi laki 6 kila siku inanipa hasira sana mie fundi seremala navuja jasho mpaka basi ila kipato duni.
 
Hivi Kwa upande wa blog, si kwanza unalipia leseni au kibali Serikalini?
Ningeenda kufahamu.
Alafu si Fiverr haitumiki bongo?
 
Hivi Kwa upande wa blog, si kwanza unalipia leseni au kibali Serikalini?
Ningeenda kufahamu.
Alafu si Fiverr haitumiki bongo?
Kipindi cha magufuli zilianzishwa hizo mambo na ilikuwa unalipia takribani milioni 2 kuisajili

alipoingia mama siku za mwanzo tu walifuta huo ukadamizaji ila jaribu kufatilia zaidi
 
Kipindi cha magufuli zilianzishwa hizo mambo na ilikuwa unalipia takribani milioni 2 kuisajili

alipoingia mama siku za mwanzo tu walifuta huo ukadamizaji ila jaribu kufatilia zaidi
Nifatilie wapi mkuu, maana nikijaribu kutafuta kwenye search engines, wananiletea mambo ya 2018, 2020 ambapo blog zilikuwa zinasajiliwa, sijui kwa sasa.
 
Back
Top Bottom