Tunaweza kufanya jambo kwa vijana wanaomaliza darasa la 7, ambao hawajabahatika kuendelea na masomo ya sekondari

Charmaine

Member
Jan 4, 2023
61
160
Niko safarini mkoani Tanga, nafika maeneo ya Michenzani, nasimamishwa na kijana mmoja. Akaniomba nimpatie chupa tupu za maji (endapo ninazo kwenye gari yangu), ili akauze apate japo pesa kiasi.

Moyo wangu unanisukuma kuzungumza na kijana huyo japo kwa dakika chache. Naam, kijana wa umri wa miaka 13 sasa, aliyemeliza darasa la 7 mwaka jana, 2022.

Shughuli yake kubwa ni kuokota chupa tupu na kwenda kuuza. Vilevile shughuli nyingine kubwa anayojihusiha nayo ni kupakia machungwa pindi malori yanapofika mkoani hapo kubeba. Ujira wa kupakia machungwa ni mdogo sana. Mfano, alisema, kupakia Tandam (wastani wa tani 15 hadi tani 16), analipwa shilingi elfu 3 tu!

Kisa cha kijana huyu kinanifanya nikumbuke jinsi taratibu zilivyokuwa miaka ya 90s mwishoni, na miaka ya 2000s mwanzoni kabisa. Utaratibu ulikuwa kijana asipochaguliwa kwenda sekondari, basi pengine angechaguliwa kwenda chuo cha ufundi stadi. Wakati huo vyuo hivi vilifahamika kama FTC, yaani Full Technical Certificate, ambapo vijana walisoma na kujifunza ufundi stadi kwa miaka miwili (2).

Ingawa, siyo wote wambao hawakuchaguliwa kwenda sekondari walichaguliwa kwenda FTC. Walibaki wengi mitaani pia ambao hawakuchaguliwa pande zote mbili.

Utaratibu wa FTC ulifutwa baada ya VETA kuimarishwa. Hivyo ikawa inamlazimu muhitimu mwenyewe aombe kujiunga na VETA badala ya kuchaguliwa moja kwa moja. Hii ilikuwa ni hatua ya kwanza ya kupoteza mfumo mahususi wa kusaidia vijana hawa.

Pamoja na kwamba VETA wanaweza kupokea vijana waliomaliza darasa la 7, lakini ukweli ni kwamba wamewekeza nguvu zaidi kwenye wale waliomaliza walau kidato cha 4. Hili linaweza kuwa kosa lingine kubwa lililopelekea kuua matamanio na ndoto za vijana wengi walioishia darasa la 7.

Katika muktadha huuhuu, ukiangalia ada ya sekondari kwa shule za kutwa ilikuwa TZS 20,000 kwa mwaka. Wakati ada ya kozi za VETA (za muda mrefu) si chini ya TZS 200,000 kwa mwaka. Hili nalo linaweza kuwa sehemu ya kuzima ndoto za vijana wengi walioishia darasa la 7!

Zaidi, ukienda mikoani, bado kuna idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza darasa la 7 lakini hawajui kusoma na kuandika kwa ufasaha. Je, nini hatima ya kundi hili pia?

Well, nina mapendekezo matatu (3) hapa.

#Mosi, VETA wana kozi zaidi ya 75 na katika kozi hizi, sifa ya kujiunga ni lazima uwe umehitumi kidato cha 4 ama 6. Katika zile kozi chache zinazosalia (ambazo zote ni ufundi), kijana wa darasa la 7 anaweza kusoma lakini hatoweza kukidhi kudahiliwa diploma endapo ataamua kujiendeleza.

Sasa kwa ngazi ya kitaifa, unaweza kuanzishwa utaratibu (vyuo) maalumu wa kudahili vijana waliomaliza darasa la 7 ambao hawajachaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari. Udahili huu unakuwa ni spesheli kwa ajili ya ufundi na stadi za maisha.

Udahili huu unakuwa unahusisha wanafunzi wote ambao hawajachaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari, bila kujali kama wanajua kusoma na kuandika kwa ufashaha. Naamini kuna stadi nyingi sana za maisha zinazoweza kufundishika bila qualification ya kusoma na kuandika kwa ufasaha.

#Pili, udahili wa vijana hawa uwe ni wa moja kwa moja, siyo wa kuomba. Mathalani, laiti kama utaratibu wa kupitia mafunzo ya JKT kwa vijana wa kidato cha 6 ungekuwa ni wa kuomba, basi ni vijana wachache sana wangeshiriki mafunzo haya.

Zoezi hili limekuwa na ufanisi kwa kuwa kijana akimaliza tu kidato cha 6, anapangiwa kambi ya kwenda kupatiwa mafunzo, yaani hatumi barua ya kuomba, badala yake anapangiwa moja kwa moja.

Utaratibu kama huu unaweza kutumika kwa vijana waliomaliza darasa la 7, na ukafanikiwa kwa viwango vikubwa sana. Hapa nikiwa na maana kwamba, vijana wote ambao hawajachaguliwa kwenda sekondari, wanachaguliwa moja kwa moja kujiunga na vyuo vya ufundi na stadi za maisha.

#Tatu, gharama/ada za vyuo hivi. Kama serikali iliweza kuendesha mpango wa “elimu bila malipo” kwa shule za sekondari, naamini kabisa inawezekana kufanya utaratibu huu kwa vyuo hivi maalumu vya vijana waliomaliza darasa la 7. Ama kukawa na kiwango kidogo cha ada ambacho ni rahisi kwa mzazi/mlezi kukimudu.

Aidha, kuanzishwa kwa mifumo na taratibu nyingi za kiserikali huwa inachukuwa muda kidogo. Je, tutaendelea kupendekeza na kusubiri utaratibu huu kwa vijana hawa wa darasa la 7 mpaka lini…???

Well, kwa ngazi ya kitaifa mwenye uwezo wa coordinate jambo hili ni serikali yenyewe. Lakini kwa ngazi ya mikoa, wilaya, tarafa, kata, mtaa, n.k., tunayo nafasi sisi wenyewe ya kuanzaisha progamu za kusaidi vijana hawa. Ingawa, wanaoshikilia dhamana katika ofisi za mikoa na wilaya wananafasi nzuri zaidi ya kuanzisha mifumo na taratibu hizi.

Bahati nzuri sana, katika teuzi hizi za wakuu wa wiliya zilizopita hivi karibuni, wakuu wa wilaya 19 ni vijana. Tuzungumzie wilaya ya Kisarawe, kama mfano katika hili ninalolijadili.

Kisarawe imebahatika kupata mkuu wa wilaya kijana kabisa, na msomi, Bw. Niki Wa Pili. Ili kuokoa kizazi cha wahitimu wa darasa la 7 kuna jambo linaweza kufanyika hapa.

#Moja, ikafanyika survey kujua kuna karakana za ufundi (seremala na makenika) ngapi, kuna taasisi ngapi za ufundi ujenzi na upauwaji, kuna vikundi vingapi vya kilimo na ufugaji, kuna vikundi vigapi vya biashara na kuwezeshana, kuna asasi ngapi za kiraia, nakadhalika, nakadhalika…!

#Mbili, ikishapatikana idadi ya hivyo nilivyovitaja hapo juu, mkuu wa wilaya anaweza kuwatembelea na kuwaomba wajiandae kuanza kupokea vijana na kuwafundisha kazi na stadi za maisha. Vijana ambao watadumu kwenye mafuno hayo ya kazi kwa vitedo kwa mwaka mmoja tu!

Ubia huu unakuwa ni kati ya serikali ya wilaya, na wadau wote wanaomiliki karakana ama taasisi hizo zitakazohusika kuwapokea na kuwafundhisha kazi vijana.

#Tatu, vijana wote ambao wanakuwa hawajachaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari, wanapangiwa moja kwa moja kwenda kwenye karakana na taasisi hizi.

Tuchukulie kwa wilaya nzima ya Kisarawe, vijana hawa wako 2000. Basi vijana 100 watasambazwa kwenye karakana mbalimbali za ufundi. Vijana 100 wengine watapelekwa kwenye ujenzi. 100 wengine watapelekwa kwenye vikudi vya kilimo na ufugaji. 100 wengine watapelekwa kwenye vikundi vya Sanaa na michezo. 100 wengine watapalekwa kwenye vikundi vya biashara na uwezeshanaji, 100 wengine watapelekwa kwenye vikundi vya cherehani, 100 wengine kwenye vikundi vya upishi na mapambo. Nakadhalika, nakadhalika…!

Mwaka ukiisha, wanaletwa vijana wengine wapya, na wale wa mwanzo wanaingia mitaani kuanza maisha wakiwa tayari walau wana fani zao na ujuzi. Utaratibu huu unaendelea mpaka pale ambapo serikali inaweka programu na vyuo maalumu vya kuwasaidia vijana hawa.

Zaidi, jukumu hili la kuwasaidi vijana hawa tusiwaachie wakuu wa wiliya ama mikoa tu, bali hata sisi watu binafsi tunaweza kufanya kwa nafasi zetu. Tunaweza kuweka nuru katika kiza kilichotawala maisha ya vijana hawa. Tunaweza kuwafungulia njia vijana hawa.

Kama wewe ni fundi makenika (uko gereji), hebu chukua kijana mmoja aliyemaliza darasa la 7. Mshike mkono kwa mwaka mzima ukimfundisha kazi. Mwaka utakaofuata chukua kijana mwingine tena. Fanya hivi kila mwaka kadiri Mungu atakavyokujaalia pumzi.

Kama wewe ni fundi cherehani, hebu chukua kijana mmoja aliyemaliza darasa la 7. Mfundishe kazi kwa mwaka mmoja, kisha mwaka unaofuata unachukua kijana mwingine tena.

Kama wewe ni fundi rangi, hebu chukua kijana mmoja aliyemaliza darasa la 7. Mfundishe kazi ya kupaka rangi kwa mwaka mmoja. Mwaka utakaofuata chukua kijana mwingine.

Kama wewe ni mtaalamu wa kuandaa vitalu vya bustani majumbani, hebu chukua kijana mmoja aliyemaliza darasa la 7. Mshike mkono katika kazi yako hiyo kwa mwaka mmoja.

Kama wewe ni mfugaji wa kuku wa nyama ama mayai, hebu mchukue kijana mmoja aliyemaliza darsa la 7. Mfundishe jinsi unavyofanya shughuli yako hiyo kwa mwaka mzima.

Kama wewe ni mjuzi wa Sanaa na michezo, hebu mchukue kijana mmoja wa darasa la 7. Mshike mkono kwa mwaka mzima, kisha mwaka utakaofuata chukua kijana mwingie tena. Nakadhalika, nakadhalika…!

Mmoja ya wanawake wanaoheshimika sana katika Kanisa Katoliki, Mama Teresa alipata kusema, “Kama hatuwezi kufanya mambo makubwa, basi walau tufanye mambo madogo katika namna kubwa”! Nami nasema, na tuanze leo, tuanze sasa.
 
Wazo zuri,tatizo vijana hao hasa wa mijini wengi wao akili zao wameziwekeza kwenye MCHINA,nimekuwa nikiwakuta wamejazana wanacheza kamari za wachina kwenye maeneo mengi sana,ni wachache sana wanaoweza kukubali kwenda kufundishwa Gereji au Mashambani na kuacha KAMARI ZA WACHINA
Pili,Charity Begin At You,huyo kijana aliyekusimamisha kukuomba chupa ulimsaidiaje in terms of mawazo mazuri ya kumuwezesha kujikwamua au hata Ajira ya muda nyumbani au kwenye shughuli zako?ulipaswa uanze na huyo kumsaidia maana tayari umeshamuona ni kijana mhangaikaji anayehitaji msaada wa kushikwa mkono kwa kumpa kazi na si Pesa.Nimependa kwamba alikusimamisha kukuomba Chupa tupu na si Pesa
 
Hili jambo linawezekana, ila hakuna watunga sera wazuri wa elimu. Kama nchi kutokana na kurithi mfumo mkongwe wa elimu tumekuwa tukipoteza nguvu kazi kubwa kwa vijana wenye elimu ya msingi na hata elimu ya sekondari kwa kuamini kuwa ni mafelia. Tunaangalia wa elimu ya juu tu. Kimsingi hakuna mtu anayeenda shuleni kufeli. Iandaliwe mikakati ya kielimu kuwapata vijana wenye elimu tunazoona ni za chini. Vijana hao wana vipaji na vipawa katika uzalishaji na kuleta tija kwa taifa
 
Nashindwa kuelewa ni kwa nini watu wenye mawazo mazuri kama haya hawapo Bungeni.Barikiwa sana kiongozi
 
Nashidwa kuelewa ni kwa nini watu wenye mawazo mazuri kama haya hawapo Bungeni.Barikiwa sana kiongozi
Kiongozi wangu haya mawazo bungeni huwezi kuyaona wamejaa machawa tu
Kuna mama mmoja mtandao fulani wa kijamii alikuwa analeta mada mtanadoni wanajukwaa wakawa wanatoa maoni yao sasa mama akawa anachukua maoni ya watu anaenda mbele zaidi anasema nimemshauri mh fulani jambo hili hili hili bila kutoa credit kwamba ushauri huu niliutoa mahali fulani kutoka kwa watu fulani
 
Ndugu mleta mada toka ndani ya moyo wangu na kupongeza sana kwa andiko hili.
Kusema ukweli kwa hali ilivyo sasa, hawa vijana wanaoshindwa kuendelea na elimu ya pili yaani wanapitia na watapitia changamoto kubwa sana , hii izingatiwe kuna wenye elimu kwa ngazi ya digrii lakini kutokana na hali ya ajira na maisha kwa ujumla wanapitia changamoto kubwa sana kiasi wamefika hadi kukata tamaa.
Sasa kama hao wenye digrii wako kwenye hali hiyo vipi hawa walio kwenye elimu ya msingi tu.

Bahati mbaya nyingine serikali huwenda haijui ifanye nini au haina mpango wowote juu yao kwa hii tumaini ndani mwao halipo tena.

Nimekuunga mkono sana hoja zako haswa hizo za mwisho kwa wale walio na fani mbalimbali waweze kuwashika mkono vijana hawa mmoja mmoja walao inaweza kuleta tumaini.

Binafsi nina ushuhuda kwa hili, kwani tokea nilipoanza kazi ya ufundi mwaka 2007 mpaka sasa walao sikosi vijana 30 mpaka 50 ambao kwa mkono wangu wameweza kuujua ufundi na wengi wao wanaendelea nao ingawa wengine waliachana na ufundi na kuwa dereva wa pikipiki lakini naweza kusema nimefanya kitu katika jamii na ninaendelea .

Kwa hiyo mafundi na wengine wenye chochote wanachojishika nacho wasiwasahau vijana hawa kwa sababu hali sio nzuri kwao.
 
Mkuu kungekuwa na like infinite ungeipata kwangu Sina Cha kuongezea. Ilo linatakiwa iwe lazima mbona. Majengo Kama yapo vijana wapelekwe wapate mafunzo ya vitendo kusoma kidogo tu Kama robo Basi. Yaani hata wanakuwa wanaenda saiti
 
Niko safarini mkoani Tanga, nafika maeneo ya Michenzani, nasimamishwa na kijana mmoja. Akaniomba nimpatie chupa tupu za maji (endapo ninazo kwenye gari yangu), ili akauze apate japo pesa kiasi.

Moyo wangu unanisukuma kuzungumza na kijana huyo japo kwa dakika chache. Naam, kijana wa umri wa miaka 13 sasa, aliyemeliza darasa la 7 mwaka jana, 2022.

Shughuli yake kubwa ni kuokota chupa tupu na kwenda kuuza. Vilevile shughuli nyingine kubwa anayojihusiha nayo ni kupakia machungwa pindi malori yanapofika mkoani hapo kubeba. Ujira wa kupakia machungwa ni mdogo sana. Mfano, alisema, kupakia Tandam (wastani wa tani 15 hadi tani 16), analipwa shilingi elfu 3 tu!

Kisa cha kijana huyu kinanifanya nikumbuke jinsi taratibu zilivyokuwa miaka ya 90s mwishoni, na miaka ya 2000s mwanzoni kabisa. Utaratibu ulikuwa kijana asipochaguliwa kwenda sekondari, basi pengine angechaguliwa kwenda chuo cha ufundi stadi. Wakati huo vyuo hivi vilifahamika kama FTC, yaani Full Technical Certificate, ambapo vijana walisoma na kujifunza ufundi stadi kwa miaka miwili (2).

Ingawa, siyo wote wambao hawakuchaguliwa kwenda sekondari walichaguliwa kwenda FTC. Walibaki wengi mitaani pia ambao hawakuchaguliwa pande zote mbili.

Utaratibu wa FTC ulifutwa baada ya VETA kuimarishwa. Hivyo ikawa inamlazimu muhitimu mwenyewe aombe kujiunga na VETA badala ya kuchaguliwa moja kwa moja. Hii ilikuwa ni hatua ya kwanza ya kupoteza mfumo mahususi wa kusaidia vijana hawa.

Pamoja na kwamba VETA wanaweza kupokea vijana waliomaliza darasa la 7, lakini ukweli ni kwamba wamewekeza nguvu zaidi kwenye wale waliomaliza walau kidato cha 4. Hili linaweza kuwa kosa lingine kubwa lililopelekea kuua matamanio na ndoto za vijana wengi walioishia darasa la 7.

Katika muktadha huuhuu, ukiangalia ada ya sekondari kwa shule za kutwa ilikuwa TZS 20,000 kwa mwaka. Wakati ada ya kozi za VETA (za muda mrefu) si chini ya TZS 200,000 kwa mwaka. Hili nalo linaweza kuwa sehemu ya kuzima ndoto za vijana wengi walioishia darasa la 7!

Zaidi, ukienda mikoani, bado kuna idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza darasa la 7 lakini hawajui kusoma na kuandika kwa ufasaha. Je, nini hatima ya kundi hili pia?

Well, nina mapendekezo matatu (3) hapa.

#Mosi, VETA wana kozi zaidi ya 75 na katika kozi hizi, sifa ya kujiunga ni lazima uwe umehitumi kidato cha 4 ama 6. Katika zile kozi chache zinazosalia (ambazo zote ni ufundi), kijana wa darasa la 7 anaweza kusoma lakini hatoweza kukidhi kudahiliwa diploma endapo ataamua kujiendeleza.

Sasa kwa ngazi ya kitaifa, unaweza kuanzishwa utaratibu (vyuo) maalumu wa kudahili vijana waliomaliza darasa la 7 ambao hawajachaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari. Udahili huu unakuwa ni spesheli kwa ajili ya ufundi na stadi za maisha.

Udahili huu unakuwa unahusisha wanafunzi wote ambao hawajachaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari, bila kujali kama wanajua kusoma na kuandika kwa ufashaha. Naamini kuna stadi nyingi sana za maisha zinazoweza kufundishika bila qualification ya kusoma na kuandika kwa ufasaha.

#Pili, udahili wa vijana hawa uwe ni wa moja kwa moja, siyo wa kuomba. Mathalani, laiti kama utaratibu wa kupitia mafunzo ya JKT kwa vijana wa kidato cha 6 ungekuwa ni wa kuomba, basi ni vijana wachache sana wangeshiriki mafunzo haya.

Zoezi hili limekuwa na ufanisi kwa kuwa kijana akimaliza tu kidato cha 6, anapangiwa kambi ya kwenda kupatiwa mafunzo, yaani hatumi barua ya kuomba, badala yake anapangiwa moja kwa moja.

Utaratibu kama huu unaweza kutumika kwa vijana waliomaliza darasa la 7, na ukafanikiwa kwa viwango vikubwa sana. Hapa nikiwa na maana kwamba, vijana wote ambao hawajachaguliwa kwenda sekondari, wanachaguliwa moja kwa moja kujiunga na vyuo vya ufundi na stadi za maisha.

#Tatu, gharama/ada za vyuo hivi. Kama serikali iliweza kuendesha mpango wa “elimu bila malipo” kwa shule za sekondari, naamini kabisa inawezekana kufanya utaratibu huu kwa vyuo hivi maalumu vya vijana waliomaliza darasa la 7. Ama kukawa na kiwango kidogo cha ada ambacho ni rahisi kwa mzazi/mlezi kukimudu.

Aidha, kuanzishwa kwa mifumo na taratibu nyingi za kiserikali huwa inachukuwa muda kidogo. Je, tutaendelea kupendekeza na kusubiri utaratibu huu kwa vijana hawa wa darasa la 7 mpaka lini…???

Well, kwa ngazi ya kitaifa mwenye uwezo wa coordinate jambo hili ni serikali yenyewe. Lakini kwa ngazi ya mikoa, wilaya, tarafa, kata, mtaa, n.k., tunayo nafasi sisi wenyewe ya kuanzaisha progamu za kusaidi vijana hawa. Ingawa, wanaoshikilia dhamana katika ofisi za mikoa na wilaya wananafasi nzuri zaidi ya kuanzisha mifumo na taratibu hizi.

Bahati nzuri sana, katika teuzi hizi za wakuu wa wiliya zilizopita hivi karibuni, wakuu wa wilaya 19 ni vijana. Tuzungumzie wilaya ya Kisarawe, kama mfano katika hili ninalolijadili.

Kisarawe imebahatika kupata mkuu wa wilaya kijana kabisa, na msomi, Bw. Niki Wa Pili. Ili kuokoa kizazi cha wahitimu wa darasa la 7 kuna jambo linaweza kufanyika hapa.

#Moja, ikafanyika survey kujua kuna karakana za ufundi (seremala na makenika) ngapi, kuna taasisi ngapi za ufundi ujenzi na upauwaji, kuna vikundi vingapi vya kilimo na ufugaji, kuna vikundi vigapi vya biashara na kuwezeshana, kuna asasi ngapi za kiraia, nakadhalika, nakadhalika…!

#Mbili, ikishapatikana idadi ya hivyo nilivyovitaja hapo juu, mkuu wa wilaya anaweza kuwatembelea na kuwaomba wajiandae kuanza kupokea vijana na kuwafundisha kazi na stadi za maisha. Vijana ambao watadumu kwenye mafuno hayo ya kazi kwa vitedo kwa mwaka mmoja tu!

Ubia huu unakuwa ni kati ya serikali ya wilaya, na wadau wote wanaomiliki karakana ama taasisi hizo zitakazohusika kuwapokea na kuwafundhisha kazi vijana.

#Tatu, vijana wote ambao wanakuwa hawajachaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari, wanapangiwa moja kwa moja kwenda kwenye karakana na taasisi hizi.

Tuchukulie kwa wilaya nzima ya Kisarawe, vijana hawa wako 2000. Basi vijana 100 watasambazwa kwenye karakana mbalimbali za ufundi. Vijana 100 wengine watapelekwa kwenye ujenzi. 100 wengine watapelekwa kwenye vikudi vya kilimo na ufugaji. 100 wengine watapelekwa kwenye vikundi vya Sanaa na michezo. 100 wengine watapalekwa kwenye vikundi vya biashara na uwezeshanaji, 100 wengine watapelekwa kwenye vikundi vya cherehani, 100 wengine kwenye vikundi vya upishi na mapambo. Nakadhalika, nakadhalika…!

Mwaka ukiisha, wanaletwa vijana wengine wapya, na wale wa mwanzo wanaingia mitaani kuanza maisha wakiwa tayari walau wana fani zao na ujuzi. Utaratibu huu unaendelea mpaka pale ambapo serikali inaweka programu na vyuo maalumu vya kuwasaidia vijana hawa.

Zaidi, jukumu hili la kuwasaidi vijana hawa tusiwaachie wakuu wa wiliya ama mikoa tu, bali hata sisi watu binafsi tunaweza kufanya kwa nafasi zetu. Tunaweza kuweka nuru katika kiza kilichotawala maisha ya vijana hawa. Tunaweza kuwafungulia njia vijana hawa.

Kama wewe ni fundi makenika (uko gereji), hebu chukua kijana mmoja aliyemaliza darasa la 7. Mshike mkono kwa mwaka mzima ukimfundisha kazi. Mwaka utakaofuata chukua kijana mwingine tena. Fanya hivi kila mwaka kadiri Mungu atakavyokujaalia pumzi.

Kama wewe ni fundi cherehani, hebu chukua kijana mmoja aliyemaliza darasa la 7. Mfundishe kazi kwa mwaka mmoja, kisha mwaka unaofuata unachukua kijana mwingine tena.

Kama wewe ni fundi rangi, hebu chukua kijana mmoja aliyemaliza darasa la 7. Mfundishe kazi ya kupaka rangi kwa mwaka mmoja. Mwaka utakaofuata chukua kijana mwingine.

Kama wewe ni mtaalamu wa kuandaa vitalu vya bustani majumbani, hebu chukua kijana mmoja aliyemaliza darasa la 7. Mshike mkono katika kazi yako hiyo kwa mwaka mmoja.

Kama wewe ni mfugaji wa kuku wa nyama ama mayai, hebu mchukue kijana mmoja aliyemaliza darsa la 7. Mfundishe jinsi unavyofanya shughuli yako hiyo kwa mwaka mzima.

Kama wewe ni mjuzi wa Sanaa na michezo, hebu mchukue kijana mmoja wa darasa la 7. Mshike mkono kwa mwaka mzima, kisha mwaka utakaofuata chukua kijana mwingie tena. Nakadhalika, nakadhalika…!

Mmoja ya wanawake wanaoheshimika sana katika Kanisa Katoliki, Mama Teresa alipata kusema, “Kama hatuwezi kufanya mambo makubwa, basi walau tufanye mambo madogo katika namna kubwa”! Nami nasema, na tuanze leo, tuanze sasa.
Lakini boss, huo ni mgawanyo wa kazi, division of labour.
Asipookota yeye chupa, au kupakia machungwa, hizo kazi atafanya nani? 😲🤔
 
Safi sana akili fresh kama hizi ndizo zinahitajika sio akili za mabhange na mirungi ukisaidia kijana leo umeokoa taifa la kesho
 
Inabidi itumike nguvu ya ziada kunishawishi kwanini mtoto aliyemaliza darasa la 7 mwaka jana hayupo sekondari leo? Shule za kata zimejaa kila sehemu na elimu ni bure kwanini mtoto ashindwe kuendelea? Miaka ile ya 90 ingekuwa sahihi kabisa kusaidia walioshindwa kuendelea. Kuna watu hawakupata nafasi za kwenda kidato cha kwanza hadi leo hii ninawalilia kwasababu walikuwa na akili na ninaamini wangepata nafasi wangefika chuo kikuu. Aliyefeli darasa la 7 kwa nyakati hizi atakuwa kilaza aliyeshindikana.
 
Back
Top Bottom