Vihoja wanavyofanya mwaka wa kwanza pindi wanapoingia chuoni kwa mara ya kwanza

Nakumbuka kipindi nimeanza mwaka wa kwanza kwenye masomo yangu ya hoteli menejimenti, kuna kijana siku ya kwanza kujiunga na chuo aliletwa na baba yake, muda si mrefu akawa sharobaro, uwiiii watu walikuwa wanampa makavu, wakawa wanamtania kuwa aliletwa chuo cha baba yake!
Ilikuwa wakimshamkumbusha hilo anakuwa mdogo kama "nukta"
 
Hivi sanduku la chuma limekuwa kitu cha aibu sana??

Mimi nilijua sanduku la chuma linafaa sana katika mazingira ya chuo kwa ajili ya wizi na panya?

Huko vyuoni huwa hakuna wizi na mapanya?

Hapa ofisini kwangu nimenunua sanduku kubwa sana la chuma ninatunzia documents na nyaraka za muhimu!

Duuh! inawezekana mimi ni mshamba sana!
 
Ukiwa nalo uraiani sio ushamba ila siku utakapo kwenda chuo ili kuongeza elimu ukibeba Trunker utaitwa mshamba...
 
though it's funny but kuna picha ungefanya kuziba sura zao for privacy hasa zile za mwanzo mwanzo za Udom umewaanika sana, sio poa wala sio utu.

Hivi hayo matranker baada ya miezi miwili huwa yanaenda wapi, maana unaweza tembea hostel nzima usiyakute wakati walijaa kama kumbikumbi.

Yote kwa yote funga kazi ni huyo mwamba aliyeenda na godoro, salute kwake.
 
Shame All of you
Hawa youngsters wengine wametoka mbali na kwenye Maisha magumu sana,
Bidii yao imewafikisha hapo na wanakumbuka walikotoka na wanajua wanakotaka kwenda na GOD BLESS watafika
Ningekuwa na uwezo, ningesimama getini chouni na kumpongeza mmoja mmoja
Na hawa ndio wanamalizaga chou mpaka mwisho
 
Wajinga sana hawa!

Hii mitandao imefunua tabaka kubwa sana la wajinga na wajuaji wasiojua kitu!

Tranka haliwezi kuwa sanduku la aibu kiasi hicho mpaka kufikia hatua ya kudhalilisha hawa wanafunzi!

Actually, mimi mwenyewe nina tranka ofisini kwangu kubwa kama jeneza na nalipenda mno maana hakuna panya anayesogea humo! Nikiweka documents nina uhakika ziko salama mpaka yesu anarudi!

Oooh chuo kikuu...chuo kikuu my ass!

Hawa ndio aina ya watu wakifika vyuoni wanaolewa na madume wenzao kwa kupenda kuishi maisha fulani ya maigizo!
 
Ninyi mnaodhalilisha hawa wanafunzi wenye mabegi ya chuma, si ajabu mama zenu huko vijijini wanaishi kwenye matembe na kunywa maji ya tope.

You are not any better. Msiwalazimishe hawa wanachuo waishi maisha yenu ya kisasa ya kimaigizo!

Wengi wanatoka familia duni kama familia za mama zenu huko vijijini na mijini wanapokula miguu ya kuku ya kuokota mahotelini!

Wajinga sana ninyi!
 
Back
Top Bottom