Kidato cha kwanza mwaka 2023 kuanza na upungufu wa madarasa 4,341

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Takriban wanafunzi milioni moja wanatarajia kujiunga kidato cha kwanza kwenye shule za Serikali mwakani huku changamoto ikiwa ni upungufu wa vyumba vya madarasa.

Takwimu za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Baraza ka Mitihani Tanzania (Necta) zinaonyesha shule hizo zina uhaba wa madarasa 4,341 nchini kote.

Upungufu wa madarasa hayo utashuhudiwa baada ya wanafunzi 1,719,996 wa kidato cha kwanza hadi cha tatu mwaka huu kuungana na wenzao wa kidato cha kwanza mwaka 2023.

Shule zikifunguliwa, idadi ya wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne itakuwa 2,793,937 na madarasa 62,089 kuhitajika kwa wastani wa darasa moja kwa wanafunzi 45.

Kwa kidato cha kwanza wanaojiunga, watahitaji madarasa 23,865 lakini wanafunzi 518,606 wa kidato cha nne waliohitimu mwaka 2022 waliacha madarasa 11,524 huku Serikali ikijenga mengine 8,000 hivyo kuacha upungufu wa vyumba vya 4,341 vya madarasa vinavyotosha wanafunzi 195,345.

Katibu Mkuu wa Tamisemi, Profesa Riziki Shemdoe alisema Serikali inatumia uwiano wa darasa moja kuwa na wanafunzi 60 hivyo hakutakuwa na uhaba wowote.

“Nadhani unafahamu kuwa kuna wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na kuacha madarasa wazi, haya madarasa 8,000 ni gepu ambayo imebaki ili wote wanaotakiwa kuingia kidato cha kwanza waweze kuingia,” anasema.

Hata hivyo Meneja Programu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMet), Nicodemus Shauri anasema bado Serikali haijaipa sekta ya elimu kipaumbele cha kutosha kwani ongezeko la wanafunzi si jambo la dharura hivyo ilipaswa kutenga bajeti ya kutosha kuhakikisha utoshelevu wa walimu na madarasa kwa wanafunzi kwani madhara ya kuwarundika kwenye darasa moja ni makubwa kwao.

“Wanafunzi watakwenda kurundikana kwenye darasa moja lakini hakuna kiongozi atakayelalamika. Matokeo ya kuwa na wanafunzi wengi kwenye darasa moja ndio yale mwanafunzi anajiunga kidato cha kwanza akiwa hajui kusoma wala kuandika,” anasema Shauri.

Mdau wa elimu, Mustapha Puya anatolea mfano kwenye mpira wa miguu kunakopaswa kuwa na wachezaji 22 na wakizidi inakuwa haiwezekani hivyo anashauri kuwe na uwiano unaotakiwa darasani.

Ili kukabiliana na wingi wa wanafunzi kuliko madarasa yaliyopo, Puya anashauri kutambua vipawa vya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba ili huko mbele wasome kulingana na vipawa vyao.

“Elimu yetu inaamini wanafunzi wote wanatakiwa wasome hesabu au Kiingereza kana kwamba wote wanakwenda kwenye uprofesa, hatujui kuna mafundi au wachezaji. Ndio maana unaona nguvu inawekwa kwenye madarasa lakini kama hiyo nguvu ya kujenga madarasa ingeelekezwa kwenye vyuo vya ufundi hao wanafunzi wangekuwa na ujuzi,” anasema.

Kama ujuzi ungelenga kuwawezesha wanafunzi, Puya anasema kungekuwa na watu wa kuisaidia jamii lakini kwa miaka minne wanafunzi wanasoma vitu vya taaluma tu.

Dk Elifuraha Laltaika, mdau wa elimu mkoani Arusha anasema kitaaluma wanafunzi wanapokuwa wengi darasani “mwalimu hushindwa kufuatilia mahitaji yao hasa wale wanaojifunza taratibu.”

Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Christian Bwaya anasema idadi kubwa ya watoto darasani inarudisha nyuma matamanio ya kuwa na ufundishaji unaomshirikisha mtoto kujenga ujuzi na umahiri.

“Mwalimu anahitaji kumfikia kila mtoto darasani ajue upekee na aelewe anavyopambana. Katika kujifunza unapokuwa na wanafunzi 60 kwenye darasa moja unampa kazi ya ziada mwalimu kutimiza wajibu wake,” anasema Bwaya.

Bwaya ambaye ni mwanasaikolojia pia anasema itakuwa vigumu kwa mwalimu kumfikia mwanafunzi mmoja mmoja darasa likiwa na wanafunzi wengi.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk Harieth Hellar anasema idadi ya wanafunzi inapaswa kuendana na ile ya walimu.

“Kama kuna ruzuku ilikuwa inatolewa nayo inapaswa kuongezeka, kama kutakuwa na wanafunzi zaidi takwimu ambayo inapendekezwa kwenye darasa moja lazima mbinu za ufundishaji na ujifunzaji itaathirika kwa sababu mwalimu atashindwa kutumia mbinu zake kuwafikia wengi,” anasema.

Kwa mara ya kwanza, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilitoa waraka uliofuta ada ya sekondari mwaka 2015 na michango yote ya shule za msingi.

Tangu kuanza kutekelezeka kwa sera hiyo, wanafunzi waliomaliza darasa la saba mwaka 2022 ndio wa kwanza kunufaika nayo.

Matokeo ya sera ya elimu bila ada yana akisi wingi wa wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza mwaka huu ambao ni nusu ya wanafunzi 2,238,602 ambao waliandikishwa mwaka 2022 kwa kidato cha kwanza hadi kidato cha nne.

Takwimu za Tamisemi zinaonyesha wanafunzi wa kidato cha kwanza wa mwaka huu ni wengi wakilinganishwa na wale wa mwaka 2022 ambao idadi yao ni 907,802 pekee.

MWANANCHI
 
Kwanini kila mwaka hadithi ni hii hii? pesa za Uvico zimefanya kazi gani
Ukweli kama nchi tumelaaniwa kila mwaka hadithi hii, na shule zinajengwa na kila Mkuu wa Wipaya na Mkurugenzi ni kumsifia Rais katoa fedha za ujenzi wa madarasa na majengo ya shule. Tujitafakari, serikali iamke hawa Wakurugenzi ni wabadhirifu sana wa mali za umma.
 
Na wale walio rudia mtihani, wanapangiwa lini shule? Au ndo hatatoshi madarasa
 
Kila mwaka tatizo ni hili hili, ila kutwaa kusifia kuwa ujenzi umekamilika, kumbe ni holla. Lol
hapana majengo ya madarasa ni kweli yanajengwa na kukamilika

Tatizo ni kwamba elimu bure imesababisia wanafunzi kuwa wengi

Swali, je kabla ya kuja na sera hii hawakujua kwamba wanafunzi watazidi majengo yaliyopo?
 
Back
Top Bottom