Maisha ya chuo yanaweza kuwa choo, kufaulu taaluma sio kufaulu maishaa

Living Pablo

JF-Expert Member
May 17, 2020
3,230
10,096
Chuo kinaweza kuwa choo, mkumbushe ndugu au rafiki yako kuwa maisha ya chuo ni sawa na Bongo movie watu wengi huigiza. Hata yule wa Mbeya Vijijini atasema kwao Mwanza!

1. Mwambie anaenda kusomea taaluma sio kazi. Anaweza kusoma uhasibu akawa dobi, anaweza somea Ualimu akawa mhudumu wa bar au boda boda.

2. Mwambie Kufaulu Taaluma sio Kufaulu maisha, wapo watu wenye elimu kumzidi yeye ila hawana ajira. Hata wenye ajira bado maisha magumu.

3. Mwambie kupata alama nyingi sio kujua mambo mengi. Wapo walio kuwa wanashika nafasi za kwanza darasan ila leo Wanazidiwa uchumi na wenzao walio onekana hawana akili.

4. Mwambie akifika chuo atakutana na watu wa mikoa tofauti na hata majiji. Ila akumbuke anatokea kijijini au wilaya iliyo duni, tena kule ndanindani, hivyo asijikweze ili aonekane.

5. Mwambie marafiki wa chuo hubadilika kila baada ya semester. Kuendelea kung'ang'ania wale wa awali ataisoma namba. Akumbuke chuo ndiko mlokole hujifunza kwenda club, kulewa na kuvaa nguo za ajabu.

6. Mwambie semester1 atakuwa na wapenzi wengi sana ila atumie kinga kwa gharama yoyote ile. Kama ni wakike akumbuke anasubiriwa na wale wa mwaka wa 2 na 3 ili asajiliwe katika orodha ya 'kontena jipya'.

7. Mwambie makundi makundi chuoni humaliza hundi mfukoni. Atapata marafiki wapeta starehe. Pesa zake zitaisha.

8. Mwambie Boom huwa linakuja ila laki 5 ya chuoni sio laki 5 ya nyumbani. Hela ya chuoni huisha haraka na bila mpangilio hivyo awe makin katika matumizi yake.

9. Mwambie chuoni hakuna ndoa ila kuna uzinzi, hivyo aachane kubeba majukumu ya ndoa ikiwa kaenda kusoma. Mwambie kuishi kiunyumba na girl au boy kama wana ndoa sio ujanja ila ni ulimbukeni na kesho ataumbuka.

10. Mwambie awe na msimamo na asikurupuke kuanzisha mahusiano chuon ikiwa nyumban ana mtu anayempenda kwa dhat. Chuoni kuna watu wapo kuharibu Malengo ya wengine awe makin

11. Mwambie Wahadhiri (Lecturers) wa kitanzania wanatamaa ya ngono hivyo akiwa mvivu darasani basi atafeli na ili apewe marks itabid awe tayari kumvulia chupi kila Mhadhiri ambao weng wao wagonjwa

12. Mwambie chuoni kuna Makanisa na Misikiti. Wanafunzi ni zaidi ya 1000 lakini waumini ni wachache. Akumbuke kusali.

13. Mwambie kama ni wa kike kuwa aridhike na hali ya nyumbani. Asifikirie kutafuta Sponsor ili kupunguza ugumu wa maisha. Atajiingiza katoka matatizo makubwa.

14. Mwambie kuwa asiwadharau watu aliosoma nao nyuma kisa hawajapata nafasi kufika chuo. Siku akimaliza chuo wapo atao wakuta wana biashara kubwa hivyo kumpa kibarua.

15. Mwambie simu na nguo za gharama ni muhimu lakini sio lazima. Hivyo asipende tumia vibaya pesa ambayo anapewa kwa awamu mana siku atazikumbuka akimaliza masomo.

16. Mwambie marafiki wanaokuwa naye kipindi hana hela asiwasahau. Awaepuke marafiki wanafik wanao mfundisha kutafuta wanawake au wanaume.

17. Mwambie chuoni ni sehemu ya kutengeneza connection na watu muhimu, akae mbali na watu wasio msaada kwake.

18. Mwambie chuoni kuna watumishi wanao jiendeleza, husoma huku wakiendelea kupokea mshahara wengi wao ni waume na wake za watu. Hawa ndio wanaotumia pesa zao kulaghai mabint na vijana.

19. Mwambie pia baada ya kumaliza chuo haina maana amefanikiwa maisha. Hapa ndipo msoto mpya unapoanzia. Anapowaona kaka na dada zake wamemaliza chuo ila wapo tu mtaani asifikiri ni wazembe ila usawa na mfumo unabana.

20. Mwambie maisha ni mafupi sana adumu kumcha Mungu na kufanya mambo mazurii. Lastly Asimdharau mtu yeyote, akumbuke na azingatie kuwa kuna maisha baada ya chuo.

Asijisahau sana maana mtaani kugumu. Mabinti wenye Degree wanaamua kuolewa na vibabu nao vijana kutembea na wazee sababu ya kukosa ajira!

Atambua kuwa leo hii dreva boda boda au bajaji anauhakika wa kuilisha familia yake kila siku kuliko muhitimu wa chuo kikuu. Hivyo asiwe na dharau kuwa hawezi olewa na mtu mwenye elimu ya chini.

Pia akumbuke sio kila dreva au konda hajasoma, watu wana vyeti vyao na ufaulu mzuri, kama haelewi basi tumuache tumsubiri akimaliza.

Ikikufaa ifanyie kazi, Mungu awaongoze katika njia iliyo sahihi na awape ujuzi utakaowasaidia hata kama watakosa ajira.

Ameen.

Credit: FB page
 
CHUO kinaweza kuwa CHOO
Mkumbushe ndugu au rafiki yako kuwa maisha ya CHUO ni sawa na BONGO MOVIE watu wengi huigiza. Hata yule wa MBEYA vijijin atasema kwao MWANZA....

1. Mwambie anaenda kusomea taaluma sio kazi. Anaweza kusoma uhasibu akawa dobi...Anaweza somea Ualimu akawa mhudumu wa Bar au boda boda

2. Mwambie Kufaulu Taaluma sio Kufaulu maisha.wapo watu wenye elimu kumzid yeye ila hawana ajira. Hata wenye ajira bado maisha magumu

3. Mwambie Kupata alama nyingi sio kujua mambo mengi.... Wapo walio kuwa wanashika nafas za kwanza darasan ila leo Wanazidiwa uchumi na wenzao walio onekana hawana akili

4. Mwambie akifika chuo atakutana na watu wa mikoa tofauti na hata majiji. Ila akumbuke anatokea kijijini au wilaya iliyo duni, tena kule ndanindani... Hivyo asijikweze ili aonekane

5. Mwambie Marafiki wa chuo hubadilika kila baada ya semester. Kuendelea kung'ang'ania wale wa awali ataisoma namba....Akumbuke chuo ndiko mlokole hujifunza kwenda Club..kulewa na kuvaa nguo za ajabu

6. Mwambie semester1 atakuwa na wapenzi wengi sana ila atumie kinga kwa gharama yoyote ile. ..kama ni wakike akumbuke anasubiriwa na wale wa mwaka wa 2 na 3 ili asajiliwe ktk orodha ya Kontena jipya....

7. Mwambie makundi makundi chuoni humaliza hundi mfukoni... Atapata marafiki wapeta starehe. Pesa zake zitaisha

8. Mwambie Boom huwa linakuja ila Laki5 ya chuoni sio Laki5 ya nyumbani....hela ya chuoni huisha haraka na bila mpangilio hivyo awe makin ktk matumiz yake

9. Mwambie chuoni hakuna. NDOA ila kuna uzinzi.. Hivyo aachane kubeba majukum ya ndoa ikiwa kaenda kusoma. Mwambie kuishi kiunyumba na girl au boy kama wana ndoa sio ujanja ila ni ulimbuken na kesho ataumbuka

10. Mwambie awe na msimamo na asikurupuke kuanzisha mahusiano chuon ikiwa nyumban ana mtu anae mpenda kwa dhat.. Chuon kuna watu wapo kuharibu Malengo ya wengine awe makin

11. Mwambie wahadhiri (Lecturers) wa kitanzania wanatamaa ya ngono hivyo akiwa mvivu darasan bas atafeli na ili apewe Marks itabid awe tayar kumvulia chupi kila muhadhir ambao weng wao wagonjwa

12. Mwambie Chuoni kuna Makanisa na Misikiti. Wanafunzi ni zaidi ya 1000 lakini waumini ni wachache. Akumbuke kusali.

13. Mwambie kama ni wa kike kuwa aridhike na hali ya nyumban. Asifikirie kutafuta SPONSOR ili kupunguza ugum wa maisha .. Atajiingiza ktk matatizo makubwa

14. Mwambie kuwa asiwadharau watu alio soma nao nyuma kisa hawajapata nafas kufika chuo.. Siku akimaliza chuo wapo atao wakuta wana biashara kubwa hivyo kumpa kibarua

15. Mwambie Simu na nguo za gharama ni muhimu lakini sio lazima... Hivyo asipende tumia vibaya pesa ambayo anapewa kwa awamu mana siku atazikumbuka akimaliza masomo

16. Mwambie marafiki wanaokuwa naye kipindi hana hela asiwasahau... Awaepuke marafik wanafik wanao mfundisha kutafuta wanawake au wanaume

17. Mwambie chuoni ni sehemu ya kutengeneza Connection na watu muhimu...akae mbali na watu wasio msaada kwake

18. Mwambie chuoni kuna watumishi wanao jiendeleza..husoma huku wakiendelea kupokea mshahara wengi wao ni waume na wake za watu.. Hawa ndo wanao tumia pesa zao kulaghai mabint na vijana

19.Mwambie pia baada ya kumaliza chuo haina maana amefanikiwa maisha. Hapa ndipo msoto mpya unapoanzia... Anapo waona kaka na dada zake wamemaliza chuo ila wapo tu mtaan asifikir ni wazembe ila usawa na mfumo unabana

20. Mwambie Maisha ni mafupi sana Adumu kumcha Mungu na kufanya mambo mazurii, Lastly Asimdharau mtu yeyote.,....Akumbuke na azingatie kuwa kuna maisha baada ya chuo...
Asijisahau sana maana mtaani kugumu.. Mabinti wenye DEGREE wana amua kuolewa na vibabu nao vijana kutembea na wazee sababu ya kukosa ajira....
Atambua kuwa leo hii dreva boda boda au bajaji ana uhakika wa kuilisha familia yake kila siku kuliko muhitimu wa chuo kikuu. Hivyo asiwe na dharau kuwa hawez olewa na mtu mwenye elimu ya chini
Pia akumbuke sio kila dreva au konda hajasoma..watu wana vyeti vyao na ufaulu mzur
Kama haelewi basi tumuache
Tumsubiri akimaliza.
IKIKUFAA IFANYIE KAZI
MUNGU AWAONGOZE KATIKA NJIA ILYOSAHIHI NA AWAPE UJUZI UTAKAOWASAIDIA ATA KAMA WATAKOSA AJIRA.
Ameen..

CREDIT: FACEBOOK PAGE



Mbona MAISHA ya CHUO ni ya kawaida Sana Ila mna Overrated Sana .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom