Vihoja wanavyofanya mwaka wa kwanza pindi wanapoingia chuoni kwa mara ya kwanza

Hicho ni chuo au kambi ya jkt
Na pia kutokuwa na smartphone unaturudisha miaka ya 1921
Mkuu sijasema wafunzwe siraha nasema wafanywe wakakavu,sijasema wasiwe kabisa na smartphone wasiingie nazo lecture room,leo mtoto anaenda chuo akimaliza anarudi na kitambi,kajifunza ulevi,ana poor saving behavior ,anachagua kazi za mati tai ,ni kwa sababu mnawaharibu kimtu kinaishi kwa boom (pesa ya wananchi wasioweza kula milo mitatu) afu anacheka mtu ambae hajawahi kula mshahara kutumia deka
 
Kijana usijione mjanja. Haya ni maisha ya kawaida kwa watanzania walio wengi. Hata sisi ambao tuko kwenye maofisi makubwa leo hii tulipita huko. Wengine hatukuwa hata na pesa ya kununua sanduku la chuma. Lakini Mungu alitoa baraka zake na kutufikisha mbali. Acha watoto wa masikini wasome pia. Acha wajikune kwa kadiri ya urefu wa mikono yao. Usiwadhalilishe. By the way, sanduku la chuma sehemu yake ni chuoni. Halitamanishi wezi. Ukimaliza chuo unamwachia mtu hapo hapo unakwenda kununua la kwenye ndege uraiani.
francis mboya,
 
Mmeyafanya yawe ya aibu kwa kuwachamba na kuwapiga picha za kudhalilisha kama hizi. Vinginevyo hayana aibu yoyote. Ulimbukeni wa watu kama hawa na nyie unayafanya yaonekane ya aibu. Vinginevyo sanduku la chuma shuleni na jeshini ndio sehemu yake.
Ingekuwa si kitu cha aibu wangemaliza nayo chuo ila cha kushangaza baada ya semester tu kuisha huyaoni tena.
 
Mmeyafanya yawe ya aibu kwa kuwachamba na kuwapiga picha za kudhalilisha kama hizi. Vinginevyo hayana aibu yoyote. Ulimbukeni wa watu kama hawa na nyie unayafanya yaonekane ya aibu. Vinginevyo sanduku la chuma shuleni na jeshini ndio sehemu yake.
Shida hawa vijana wanabadilika kila kitu kuanzia mavazi mpka lifestly vijana wengi wa chuo wanaongoza kwa kuigiza maisha.
 
Shame All of you
Hawa youngsters wengine wametoka mbali na kwenye Maisha magumu sana,
Bidii yao imewafikisha hapo na wanakumbuka walikotoka na wanajua wanakotaka kwenda na GOD BLESS watafika
Ningekuwa na uwezo, ningesimama getini chouni na kumpongeza mmoja mmoja
Na hawa ndio wanamalizaga chou mpaka mwisho
Don't take it seriously,,,,,, unaelewa nini maana ya utani ?????? acha tufurahi maisha yaende

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi sanduku la chuma limekuwa kitu cha aibu sana??

Mimi nilijua sanduku la chuma linafaa sana katika mazingira ya chuo kwa ajili ya wizi na panya?

Huko vyuoni huwa hakuna wizi na mapanya?

Hapa ofisini kwangu nimenunua sanduku kubwa sana la chuma ninatunzia documents na nyaraka za muhimu!

Duuh! inawezekana mimi ni mshamba sana!

Kweli we mshamba, Hujui tofauti ya Document na nyaraka !
 
First year wamekuwa wakifanya vimbwanga mbalimbali pale tu wanaopenda kufanya usajili mimi nimevinyaka hivi kwa first year wanaoingia chuoni kufanya usajili mwaka huu.

Navibandika hapa na wewe bandika vyako hapo chini tuongezea angalau siku za kuishi.

View attachment 1245104View attachment 1245105View attachment 1245106View attachment 1245109
View attachment 1245103
Huyo jamaa aliyekuja na mfuko wa SHANGAZI KAJA ndio kaua kabisa aisee hata Profesa Ndalichako angekuwepo hapo angecheka nusu afe
 
Back
Top Bottom