Bado, hata Wilaya ya Mafia yenyewe, yenye wananchi zaidi ya 67,000; na ukubwa wa kilomita za mraba 640 huwezi ukailinganisha kwa vyovyote na jimbo la uchaguzi lolote toka Zanzibar; hata kwa vigezo hivyo pekee.Naona kuna shida ya kuelewa point kuu ninayotaka kuzungumzia. Nilipoandika mfano wa Mafia, lengo kuu lilikuwa kwa ujumla, si Zzibar tu bali hata bara ubunge kati ya jimbo na jimbo haulinganishwi kwa idadi ya watu.
Nilichotaka kusema, Lissu kama anataka kuwa muwazi basi vile vile alaumu kwanini Mafia ina mbunge mwenye hadhi sawa na mbunge wa Kawe, kama idadi ya watu ndio vigezo?
Sasa tuliungana ili iweje, Zanzibar ifaidi matunda ya Muungano bila ya yenyewe kupoteza chochote? Iendeshe mambo yake yenyewe bila ya kujali kuwa imo kwenye Muungano?Suala la Muungano. Kwanza tukubaliane kuwa ni nchi 2 ndio zilizoungana, sio mikoa 2. Kumbuka Zanzibar ilkuwa na kiti umoja wa mataifa kilichokuwa na uzito sawa na Tanganyika. Tunaposema Tanzania imepiga kura umoja wa mataifa kupitisha suala fulani, kura hiyo ina uzito sawa na kura ya Burundi na Rwanda zenye watu chini ya 6 mil kila moja. Hivyo suala la nchi huheshimiwa kama nchi bila kujali kuna watu wangapi. Twende pamoja!