Video: Rais Ruto avunja kamati ya Utekaji

Video: Rais Ruto avunja kamati ya Utekaji

Mbali na Elimu nzuri walizonazo, lakini pia uzoefu kutoka duniani kote kabisa unaonyesha kwamba kwenye nchi ambazo Uhuru wa nchi husika ulipatikana baada ya kupigana vitani, Wananchi wengi zaidi kwenye nchi hizo wamekuwa Wana mwamko wa kudai na kupigania HAKI zao bila woga pale wanapoona kuwa Haki zao hizo zinahujumiwa na Watawala wa nchi.
Ni elimu brother, vyuo vikuu vyetu vinazalisha majitu majinga haswa hayawezi hata kujieleza, nilipomaliza chuo nilifanya kazi na Shirika la nje kwa miaka 4 tulifanya kazi kwa karibu sn na serikali utadhani na sisi ni serikali, asee ni aibu tupu wasomi wetu hata kuandika taarifa ambayo ameshiriki kwenye hiyo activity hawezi na huku ana masters + uzoefu kazini wa miaka hata 10, kwenye interview ndiyo usiseme ni aibu tupu mtu hawezi kujibu swali la historical background ake na huyo ni graduate. Kuna shida kubwa asee acha waende VETA kwanza naunga mkono hoja afadhali wanafunzi wa VETA ila siyo hawa wa UDOM, UDSM n.k.
 
Hayo ni makundi yao kaona maji yamezidi unga kalifutilia mbali..!!

Lakini sasa isiwe anafanya danganya toto, huku public kalivunja halafu nyuma ya pazia wanaendeleza ukola..!!
Hapo Kaa ukijua Kuna Kundi lingine limepewa jukumu
 
Spana zako unazopiga huwa nacheka sana nikiingia jukwaa la siasa..!!
Unanyoosha km rula hucheki na yoyote 😹
Mkuu nchi yetu inateswa na ujinga wetu, nimefanya kazi na shirika kwa miaka 4 nilijionea mengi sn kwenye utumishi wa umma kuna madudu sababu tulikuwa tunafanya kazi karibu sn na serikali, asee kuna mambo ya kijinga sn na aibu tupu, watu wanapenda pesa lakini siyo kufanya kazi wala hawajitambui na hao ndiyo tunawategemea watufikishe nchi ya ahadi asee.
 
Ushindi atapata kwa kutumia Balot Box

Ukiwa siyo mtu mnafiki, au ukiwa mkweli kabisa kabisa katika nafsi ya moyo wako, utakubaliana na Ukweli mchungu Sana kwamba huyu Mama Kamwe hawezi kupata Kura hata za Asilimia Kumi tu kwenye Uchaguzi Mkuu ujao endapo kama kutakuwa na Tume ya Uchaguzi iliyo HURU kama ile iliyopo kule nchini Afrika Kusini.
 
Sio km Tz sababu huku hawachukuliwi hatua zozote za kuwajibishwa kisheria, tofauti na Kenya wale wana katiba nzuri na hawapendi ujinga..!!
Unadhani na kwa sababu zipi? wananchi ukifanya upumbavu kesho wanaadamana kudai haki, huku kwetu haki ni hisani ya Rais na siyo wajibu, serikali ina matumizi makubwa kuliko serikali ya Marekani mambo ni hovyo hovyo na ufisadi ni mwingi, wananchi kutwa ni Simba na Yanga, bettings, movie, pombe kali, pool table na alkasusi wakafanye mapenzi akili zimeishia hapo, hawana habari na maendeleo ya nchi yao hata kidogo siyo maofisini wala uraiani, mkuu ngoja hawa wasomi wetu waende VETA kwanza labda watapata akili kidogo.
 
Mkuu nchi yetu inateswa na ujinga wetu, nimefanya kazi na shirika kwa miaka 4 nilijionea mengi sn kwenye utumishi wa umma kuna madudu sababu tulikuwa tunafanya kazi karibu sn na serikali, asee kuna mambo ya kijinga sn na aibu tupu, watu wanapenda pesa lakini siyo kufanya kazi wala hawajitambui na hao ndiyo tunawategemea watufikishe nchi ya ahadi asee.
😥 Watanzania wavivu wa kila kitu ndiomana tunapelekeshwa..!!

Na hao viongozi washatujua udhaifu wetu na wao wanapitia humo humo.
 
Back
Top Bottom