VIDEO: Mlipuko wa Bomu Arusha - Sehemu ya Kwanza...

VIDEO: Mlipuko wa Bomu Arusha - Sehemu ya Kwanza...

Yeyote aliyehusika damu ile itamuwinda yeye na kizazi chake chote for 10 rebirths in lord shiva's name.
 
Eeh! MUNGU ULIYE HAI, Kwako hakuna kilicho gizani, wala hakuna kilicho mafichoni, naam unawapitiliza wana uovu wa baba zao kizazi hata kizazi, ninakuomba ee Mfalme mkuu, baba wa milele uyaweke haya peupe, ili kila aliyehusika na unyama huu apatikane!! Laana ikatafune maisha yao kama mzoga wa jangwani na ukiwa wa maisha yao kama mifupa kaburini, amen!
 
tukio hili kwa kweli linasikitisha sana na la kikatili mno.
Embu itazame tena hiyo video mwishomwisho,muangalie vizuri godbless lema,uzito wa jambo na alivyo.kuna kitu utagundua
 
Binafsi nitafarijika sana hawa watu wakitiwa nguvuni na kupatiwa hukumu stahili.

Kama ni wanasiasa basi nitawachukia hadi naingia futi sita.
 
Nilidhani kile cha Mwangosi niliona kupita kiasi. Sikutegemea kuona tena damu za watanzania zikitapakaa. Kikwete na mafisadi wenzako mtalipa hadi kizazi cha nne. Ni njaa ya madaraka tu? Inatia mpaka aibu. Serikali gani hii jamani?
 
Dah! jamani! nimeangalia na kutokwa machozi.

Yaani nikiangalia yule mtoto mdogo alivyokuwa anajithaidi kunyanyuka, nimetokwa machozi sana

Sina la kusema, mwenyezi wapunzishe kwa amani! dah
 
Mungu wangu, hii yoote kuwatisha watu wasiende kwenye mikutano ya wapinzani, ikiwezekana CCM iendelee kuwa madarakani, kwani wakiondolewa, siri zoote zitakuwa wazi kwa mfano:-

1. Kifo cha Sokoine hakitakuwa fumbo tena.
2. Kifo cha Holace kolimba wahusika watafahamika na wananchi watajua ni nani aliyewatuma wafanye mauaji yale.
3. Kifo cha Imrani Kombe kitaangaliwa upya, na kutakuwa na fursa ya kohoji kwanini wauaji waliachiwa huru na kwa maslahi ya nani
4. Ufisadi wa melemeta utahojiwa, kupata ukweli kama kweli ulikuwa ni mradi wa Usalama wa Taifa na kama kweli Usalama wa Taifa wanafanya biashara.
5. Kutakuwa na fursa ya kuwabana wale wezi wa Pesa za EPA ambao walisamehewa na Kikwete na kuwaomba warudishe ilihali, kuna watu wamebainika kuiba Baiskeli wanaozea jera.
6. Kutakuwa na fursa ya kujua kama kweli Pesa ya EPA imerudishwa yoote au ilikuwa ni funika Kombe Chadema ipite.
7. Kutakuwa na fursa za kuhoji uhusika wa Kikwete katika ishu ya Richmond, japo Lowassa alitaka kutudokeza lakini alisita.

.
.
.
.
.
.
.
.
6548. Kutakuwa na fursa ya kujua kuna siri gani ya kuendelea na watu kama akina Kamuhanda japo ametajwa katika mauaji ya Songea na Iringa?

6549. Itafahamika kama Balali alifariki kweli au yupo hai, na kama yupo hai kwanini afichwe?
Bila kusahahau nani aliyempandikizia sumu mwalimu nyerere
 
Ben Saa8,Tafadhali malizia tumuone aliyerusha Bomu kisha Polisi wakamkamate kama walivyomkamata Lwakatare kwa kupitia youtube,hivyo nawashauri makamanda wasiukabidhi mkanda kwa chagonja wala yeyote yule ila wauweke humu kisha Polisi wakajikamate! INASIKITISHA SANA na inatia uchungu mno,nipo Dar na si mwanachama wa CDM lkn kwa ukatili huu kuanzia sasa hata kama CDM itasimamisha jiwe kwenye uchaguzi nitaipigia kura!
 
Lakini katika mkusanyiko kama huo watoto wako kwenye risk ya kupoteza uhai wao.

Children are vulnerable na wakati wa vurumai kama hiyo hakuna atakayemjali mtoto.

Wataishia kukanyagwa kanyagwa tuu.

open up your mind bro! tunazungumzia "uhai" hatuzungumzii "usalama" wala vulnerabilty, by the way kufanya mikutano is it considered a risk in this country? that watoto wakae mbali wasije kufa! mbona mikutano mingi ya ccm watoto ndio wengi, is this risk???? au ni risk kwa cdm pekee???
 
damu mumwage nyie halafu lawama tupate sisi! punde si punde mtaumbuka na ni lazima muipate fresh mwaka huu. haiwezekani chama kinalea magaidi, mnapoteza maisha ya watu na wengine wanabaki vilema halafu tuwachekelee tu. tutapambana humu jf na polisi watapambana nanyi huko nje

Ni rahisi kufanya mizaha pale ambapo aliyeuawa si nduguyo.. Hali hii haiishii CHADEMA tu, hata mashabiki wa CCM mtakuwa wahanga tu!... Mungu yuko!... Saddam alipoua wapinzani wake kwa sumu, risasi, upanga na kunyonga hakujua ipo siku na yeye mambo haya yatamfika. Nanyi ni akina Saddam wa leo.
 
wacheni upuuzi hizi ni siasa tu, mimi naamini kabisa kuwa hata hao chadema wenyewe inaweza kuwa ndio walorusha bomu hilo kwa kumtumilia polisi (kama ni kweli) wanaweza kuwa wamevaa uniform za polisi, au munadhani hao polisi hakuna wafuasi wa chadema????? Na kwa nini bomu hilo lirepuliwe karibu na hicho kiriri cha kutoa hutuba tena pale alipopanda muheshimiwa aliyetaka kuhutubia watu wa arusha????
Kama lengo ilikuwa ni huyo muheshimiwa basi huyo muheshimiwa angelipigwa risasi 1 tu ya kichwa bila ya hata kujulikana aliyefanya tukio, ila hili bomu nina imani kabisa kuwa mfanyaji na wapangaji wa hili tukio na shambulizi ni wenyewe chadema, msidanganywe na hizi siasa na hawa wanasiasa, kwani walofanya september eleven attack marekani ni osama kweli???? Amkeni nyinyi wachaga
tanzania sasa imekalia time bomb niliwaambia zamani haya maneno tokea 2010 tusubiri hiyo 2015 time bomb iripuke pasikalike tena hapa ndio lilobakia, hivi unadhani chadema watakubali kushindwa 2015? Hivi unadhania ccm watakubali kushindwa 2015 basi ujue tanzania ipo katika time bomb, ndio maana huku zanzibar tunataka kujitoa na mapemaaaaa katika muungano na hii time bomb yenu munayotegeshewa muirepuwe wenyewe.....mwenye remote hayupo hasaaaa.

usifikiri kwa kutumia Masaburi,hata kama alivaa uniform za Polisi na ni CDM na aliondoka na gari la Polisi,kwa nini wanamtafuta? Millioni 100 ni za nini? kumbuka ni huyuhuyu Chagonja aliyetudanganya kuwa Mwangosi aliuwawa na kitu kilchorushwa kwa Polisi na si kilichorushwa na Polisi ila Teknologia ikamuumbua kama itakavyowaumbua sasa! Naiona Tanganyika ileee inarudi,Mungu ibariki Tanganyika!
 
This is too much,wapiga kura wao vijijini hawayajui haya ndio maana hawashtuki wala kuteteleka
mimi ninashauri hizi video tuzihifadhi,kila anayekwenda kuelimisha watu vijijini aende na projector wananchi wajionee wenyewe unyama huu...we are at the critical point that we need to sacrifice OUR lives to bring changes..nitakuwa wa kwanza kuzipeleka video hizi kwa wapiga kura wao hata waniue sitakuwa wa kwanza kuililia ardhi yangu.....

Ben hongera kwa ujasiri huu

they have killed one but we are coming
 
jamani nisaidien na mimi nione cm yangu imeshindwa kuifungua please tumekusanyika hapa tuone jaman
 
Sijaamini bado, hii ni Tanzania? au Syria, nadhani CDM fanyeni kitu kupitia UN, haiwezekani mbinu za kukandamiza demokrasia zikaachwa hivihivi. Hivi ungekuwa mkutano wa CCM mlipuaji angekuwa bado hajakamtwa? AAgh!!!!
 
huo ni mpango wa CHADEMA wenyewe ila wananchi hawajui tuu kwanini hilo bomu halijalipuka wakati MBOWE akihutubia na huyo mlipuaji wa bomu malengo yake yalikuwa nini?? lazima tuwetunajuiliza jamani..
 
Nimeangalia hii video machozi yakaanza kutoka,nimekuwa nikijiuliza hivi hawa CCM bado wanaamini kuua ni suruhu?Eee Mungu wa mbinguni walaani CCM na vizazi vyao vyote milele na milele hakika damu ya watu i juu yao.
 
Dah! jamani! nimeangalia na kutokwa machozi.

Yaani nikiangalia yule mtoto mdogo alivyokuwa anajithaidi kunyanyuka, nimetokwa machozi sana

Sina la kusema, mwenyezi wapunzishe kwa amani! dah

It's sad and so painful brother.Hatuwezi kuliacha hili hivi hivi.Let us join hands together ....!
 
Back
Top Bottom