Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,801
- 43,177
Si utapata madonda, inasaidia nini kufanya hivyo?
Well namshukuru maulana sijawahikuwa na maradhi ya tumbo zaidi ya kuharisha mara mojamoja tumbo linapochafuka.
Nikiwa mdogo nilikuwa mvivu/msumbufu wa kula. Nilipopata hela nilikuwa na appetite kula kila ambacho sijawahi kukionja mradi tuu kisiwe kichungu.
Namshukuru Maulana tena sinaga aleji.
Ila nina udhibiti mkubwa wa chakula ninapofanya maamuzi au kuamua kuutiisha mwili usinipelekeshe kadri unavyojiskia.
Siwezi kukwambia faida ninazopata moja kwa moja ila huu ni mtindo wa maisha yangu. Kuna vipindi na vipindi mwili unasahau kama kuna starehe za hii dunia. Unapitia shuruba kama uko jeshini, Ila kuna kipindi najiachia hadi mwili unasema yeees, Kasinde is spoiling us eehehehehe.