Uzi maalumu kwa wafanyakazi wa miradi ya kikandarasi (watingaji) kwenye kampuni za kigeni

Lugoda lwa chuma

Senior Member
Mar 21, 2023
179
338
Habarini wana jamvi huu uzi ni mahususi kwa watingaji wote iwe umeajiriwa (YAPPI, CHICO, CCE, CRSG au kampuni nyingine yoyote inayo simamia mradi wowote wa ujenzi iwe barabara, reli, uwanja wa ndege au bwawa la umeme n.k.

Tupeane changamoto, uzoefu na connections haijalishi wewe ni engeneer, surveyor, dereva, operator, mpishi au labour tujumuike tuyatoe ya moyoni. Kwa kuanza mimi ni store keeper katika kampuni ya china henan international cooperation(chico) kwa sasa tupo mkoa x sitautaja kwa sababu maalum tukitengeneza barabara ya lami km kadhaa.

Kwanza napenda kuanza na changamoto tunazopitia kutoka kwa hawa mabosi zetu wachina. Moja asilimia kubwa wana dharau za kufa mtu na matusi kwa wafanyakazi wabongo, mainjinia labda ndo wanaheshmika na ma human resource officers kidogo, Kingereza hakiwachomoki hivyo huchanganya Kichina, Kingereza na Kiswahili sasa usipomuelewa boss anakuona wewe ni mjinga huna akili lazima uoge matusi marakapii, sinchuba, shakapyu mara kajiba kujisa hadi akili ikae sawa.

Pia ni watu wenye short temper kupanic na ku shout ni kawaida. Kingine hawajali kabisa usalama wako kazini unakuta mtu safety boot imechakaa, gloves hana, refrector imechoka ila wadudu hilo hawajali wanacho angalia kazi zao zinaenda wewe utajijua mwenyewe usipokuwa makini.

Ila kwenye malipo angalau wanajitahidi malipo minimum ni 16K kwa siku kwa labour kila kitengo kina hela yake, pia NSSF wanakuwekea. Karibuni na wengine tupate kushare.
 
Muda wengine ukipeleka kesi ya mdudu(mchina) kwenye office za HR hautosikilizwa zaidi tu utapewa warning asee!! nchi yetu hii watu wapo kwaajili yakuangalia ugali wao tu.
 
Back
Top Bottom