Mkandarasi Reli ya SGR asema sababu za Wafanyakazi kutoingiziwa malipo ya NSSF ni kwa kuwa kuna makubaliano maalum

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Siku chache baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kuandika andiko akilalamikia juu ya Mkandarasi Mkuu anayejenga Reli ya SGR, Yapi Merkezi kutowaingizia wafanyakazi wake malipo ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa zaidi ya miezi 9, ufafanuzi umetolewa na Mkandarasi akisema kuna makubaliano maalum.

Andiko la Malalamiko hili hapa - Mkandarasi SGR anataka kutupunguza 50% ya Wafanyakazi wakati hajatuingizia fedha za NSSF miezi 9

Akitoa ufafanuzi juu ya madai hayo ya Wafanyakazi Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Yapi Merkezi, Amisa Juma anasema:

“Changamoto ya malipo ilitokea kipindi cha miezi kadhaa nyuma wakati kulipotokea changamoto ya kifedha, yakafanyika mazungumzo kati ya Yapi Merkezi na NSSF ambapo walikubaliana kuwa Mkandarasi ataingiza malipo hayo kwa awali ili hadi kufikia mwisho wa Novemba 2023 yawe yamekamilika.

“Yapi ni moja ya taasisi ambayo ina Wafanyakazi wengi ndio maana hata wakati wa kuingiziwa fedha za NSSF kwa awamu kuna baadhi wamepata wengine hawajapata.

“Hivyo, ikifika hadi mwishoni mwa Novemba (2023) malipo yakiwa hayajakamilika hapo ndipo NSSF wanaweza kuishtaki Yapi kwa kutotekeleza kile ambacho wamekubaliana kwa kuwa ni haki inayotambulika kisheria.

“Wafanyakazi wengi walijulishwa juu ya makubaliano hayo, inawezekana wapo wachache ambao hawakupata taarifa hiyo ndio maana wakaanza kulalamika mtandaoni.”
 
Back
Top Bottom