Uwekezaji wa NHC - Mchechu awajibike

Uwekezaji wa NHC - Mchechu awajibike

Sabayi
Mbona sikuelewi? Ndugu yangu funguka fikra zako. Acha kujifungia ndani ya box rafiki yangu, wee unajua huyu ameletwa na nani? Narudia tena nafasi aliyopata nehemia ya uDG hapo NHC ni opportunity, mimi sio mtu wa kijizuia kufikiri kama wewe kwamba eti akijihuzulu nehemia eti shirika linarudi kule kule! Haya ni mawazo ya watu wazembe wa kutumia bongo zao. Ukiondoa interference za wanasiasa nchi hii ina wataalamu lukuki wanaoweza kufanya makubwa hapo NHC hata zaidi ya nehemia. Ukiyasoma maelezo ya nehemia mwenyewe na maelezo ya NHC kama taasisi utagundua kwamba pamoja na uzuri unaonekana kwa nje wa utendaji kazi wa nehemia na NHC kuna tatizo kubwa ktk utendaji wao na ikichunguzwa kwa makini mengi yatajitokeza!

Mkuu kama umesoma vizuri post zangu tunaweza kuwa tunaongea lugha moja ila hatuelewani tu.Hao wataalam unaosema ni kweli tunao wengi ila ukisoma post yangu hapo juu nimesema hii nchi bado ni ya hovyo hizo presidential appointments hazitolewi kwa kigezo cha utaalamu au utendaji bali ni kujuana,ushakaji,ukabila,udini n.k so akiondolewa yeye hatuna uhakika wa kupata mtu mwingine mzuri system yetu bado ni mbovu ni kweli Neemia ana mapungufu yake ila ukilinganisha na waliopita amejitahidi sana so it's just a coincidence unless we get our politics right hatuwezi kuwa na wataalam wazuri kuongoza taasisi zetu nyeti bila kuingiliwa na wanasiasa na hivyo kuathiri utendaji wao.Ni matumaini yangu umenielewa nazungumza nini
 
Kanji,
Kukimbilia kuhukumu bila kulielewa tatizo unaweza usitatue chochote. Hapa tatizo sio mkataba, bali ni ujenzi mbovu, material dhaifu, design mbovu au mchanganyiko wa hivyo nilivyotaja. Kwa hiyo watu wanaotakiwa kuwa wa kwanza kuminywa ni Mjengaji (Contractor), Msimamiaji wa ujenzi (Project/Resident Engineer/Consultant), Archtect, Structural Engineer, idara ya ujenzi NHC, City Engineer na wengine wengi wanaohusika moja kwa moja na ubora wa jengo kitaaluma.

Mchechu na wengine wasiohusika na ujenzi moja kwa moja kitaaluma, wao zamu yao itakuja baada ya uchunguzi wa nini kilichoangusha jengo kujulikana. Ushirikiano kwenye uwekezaji wa miradi ya NHC sio ulioangusha jengo. Lakini kama ujenzi na usimamizi ungekuwa ni huu huu, basi hili lingetokea hata kama pesa ya ujenzi ingekuwa ya NHC peke yake.


Ukistaajabu ya musa hii sasa ni ya Firauni kudadeki!
 
Rais wa nchi kashasema "hii ni kazi ya mungu tu" baada ya wachimbaji madini kufukiwa ardhini, huku hakuna hata preventative measures zilizochukuliwa.

Itakuwa huyu kidampa wake?

Tanzania hatuna meritocracy, kijamaa kimewekwa wekwa tu kiajabu ajabu. Kumbe achilia mbali mambo ya technical nitty gritty huko. Kujieleza tu tabu.

Lakini tutategemeaje ajue kujieleza na kuwa competent wakati rais wake mwenyewe hakuchaguliwa kwa competency?

Mchakato wa kumteua kuwa CEO hauko transparent na haujali competency.

Mtu kama huyu anaomba kazi kuwa CEO hata humfanyii oral interview, unaweza kupoteza muda tu. Unamfungia chumbani na kalamu na karatasi, unampa dakika 30 aandike insha anataka kuwa CEO ili afanye nini (ukimwambia aandike nyumbani ataandikiwa, na hakikisha hana simu asipate msaada wa nje).

Unaenda chumba cha pili kufanya mkutano mwingine.

Ukirudi baada ya dakika 30 ukisoma insha tu unajua huyu hata raundi ya pili kumpeleka ni kupoteza muda tu.

Leo ndo mtu wa aina hii kaja kuwa CEO!

Kikwete anaendeleza tu appointees wake kuwa wa ajabu ajabu kama yeye.

Kuna tofauti kubwa sana jinsi waafrika tunavofikiria na jinsi wenzetu wazungu wanavofikiria, Ulaya jengo lkidondoka Watu wanangia maabasa na kufanya Tafiti zinazoweza kusema nini sababu ya hiyo kitu, Sisi ni neno mbili tu.....Kazi Ya Mungu, mungu anasingiziwa kila baya.

Mwendo kama huuu na mentality zetu tuaendelea kufanya yale yale vile vile.
 
Rais wa nchi kashasema "hii ni kazi ya mungu tu" baada ya wachimbaji madini kufukiwa ardhini, huku hakuna hata preventative measures zilizochukuliwa.

Itakuwa huyu kidampa wake?

Tanzania hatuna meritocracy, kijamaa kimewekwa wekwa tu kiajabu ajabu. Kumbe achilia mbali mambo ya technical nitty gritty huko. Kujieleza tu tabu.

Lakini tutategemeaje ajue kujieleza na kuwa competent wakati rais wake mwenyewe hakuchaguliwa kwa competency?

Mchakato wa kumteua kuwa CEO hauko transparent na haujali competency.

Mtu kama huyu anaomba kazi kuwa CEO hata humfanyii oral interview, unaweza kupoteza muda tu. Unamfungia chumbani na kalamu na karatasi, unampa dakika 30 aandike insha anataka kuwa CEO ili afanye nini (ukimwambia aandike nyumbani ataandikiwa, na hakikisha hana simu asipate msaada wa nje).

Unaenda chumba cha pili kufanya mkutano mwingine.

Ukirudi baada ya dakika 30 ukisoma insha tu unajua huyu hata raundi ya pili kumpeleka ni kupoteza muda tu.

Leo ndo mtu wa aina hii kaja kuwa CEO!

Kikwete anaendeleza tu appointees wake kuwa wa ajabu ajabu kama yeye.


Niliwahi kusoma elimu ya magugu yaliyoshindikana. Lakini kuna madawa yanayoyauwa kuanzia kwenye majani hadi kwenye mizizi. Kwa elimu hiyo naona serikali imekufa tangu majani hadi mizizi.

Hakuna mchakato wowote wa maana ambao ungeweza kumpata mtendaji wa maana. Hebu angalia kule juu kulikuwa na mtu aitwaye Luhanjo. Yeye mwenyewe kwa wale wasiomfahamu angalau walimuona akimtetea yule K/mkuu Jairo.

Kidogo nikosane na maelezo ya Shaaban Robert kuhusu umuhimu wa nywele nyeupe kichwani. 🙂)
 
Asante Ogah! Yaani inaniuma sana kuona watanzania wanakufa kizembe kwenye nchi yao na watu wasiojali uhai wa watu! Maana kwa akili ya kawaida tu isiyoenda shule foundation ya ghorofa tisa haiwezi kuhimili ghorofa 16!! Kuongezea hapo nondo milimita sijui 16 ndio walitumia plus mchanga kibao!! Hao wahusika wafungulie mashtatka ya mauaji sio uzembe!!!

Nguto,

Umeandika jambo moja muhimu sana kwa a common person kutakiwa kuliona...msingi wa nyumba unakuwa designed ku-accommodate a designed load..........sasa kwa uzembe uliotokea inabidi wajuzi wa-establish source of failures.....

Pili kuhusu insurance.....kwenye miradi ya Ujenzi....Mkandarasi ndio anakuwa ana-own the site kwa kipindi cha mradi mpaka atakapo kabidhi kwa Client......na Ujenzi wake unakuwa insured na Mkandarasi.....na pia kunakuwepo na bond kadhaa....cha msingi cha kuangalia, je zilikuwepo valid insurance ku-cover matukio/majanga (endapo litakuwa defined as janga au vinginevyo ili liwe valid kwa insurance compensation), je bond zilizopo ziko valid? na je zina-cover vitu gani, pia kuna masuala ya license liabilities......inabidi license za baadhi ya watu zisimamishwe NHC ni mojawapo......license zao zisimamishwe na zifanyiwe review......
 
Mtu kama huyu anaomba kazi kuwa CEO hata humfanyii oral interview, unaweza kupoteza muda tu. Unamfungia chumbani na kalamu na karatasi, unampa dakika 30 aandike insha anataka kuwa CEO ili afanye nini (ukimwambia aandike nyumbani ataandikiwa, na hakikisha hana simu asipate msaada wa nje).

Ebwana eeh umenikumbusha wakati nimeitwa kwenye usaili hapa kwenye boksi. Ile nimefika tu administrative assistant akaniita kwenye chumba akanipa writing pad akaniambia bosi yupo mkutanoni na atatoka baada ya dakika 20 ila in the meantime andika insha ya kwa nini unataka umeomba kufanya kazi hapa.

Nikaona kama vile nimedharauliwa. Lakini kwa vile shida ilikuwa ni yangu ikabidi tu niyameze majivuno na kuandika walichotaka.

Nikaandika, nikampa akampelekea bosi. Baada ya dakika chache nikaitwa kwenye usaili/maongezi na bosi. Nikawakuta wako watu wawili ofisini. Nikamaliza nikaondoka zangu. Nilijua nimefanya vizuri na wao wakasema watajadiliana halafu wataona kama wataniita tena kwa duru ya pili.

Na kweli baada ya siku kadhaa nikaitwa tena kwenye duru ya pili. Mambo yakawa mswano.

Baadaye sasa kukaa na kufikiri na kujiuliza kwa nini waliniomboa niandike insha wakati resume yangu walikuwa nayo ndiyo nikahisi (baadaye nilikuja kujua) kwamba hiyo ni moja tu ya njia wanazotumia katika kuchekecha applicants.

Hawawezi wakategemea tu application letter na resume peke yake maana hizo mtu unakuwa umejitayarisha kuziandaa na kadhalika. Lengo lao ni kutaka kujua kama kweli sifa zako ulizoorodhesha kwenye resume zinaendana na uwezo wako.
 
Wamesema wapi hilo?

Watarudisha na maisha ya waliokufa?
Patamu hapa, Smile umeingia cha kiume leo, unaambiwa tatizo ni umakini wala siyo lugha, tafuta series moja ya Wasouth Korea inaitwa IRIS ndio utamuelewa vyema Kiranga.
 
Last edited by a moderator:
Ebwana eeh umenikumbusha wakati nimeitwa kwenye usaili hapa kwenye boksi. Ile nimefika tu administrative assistant akaniita kwenye chumba akanipa writing pad akaniambia bosi yupo mkutanoni na atatoka baada ya dakika 20 ila in the meantime andika insha ya kwa nini unataka umeomba kufanya kazi hapa.

Nikaona kama vile nimedharauliwa. Lakini kwa vile shida ilikuwa ni yangu ikabidi tu niyameze majivuno na kuandika walichotaka.

Nikaandika, nikampa akampelekea bosi. Baada ya dakika chache nikaitwa kwenye usaili/maongezi na bosi. Nikawakuta wako watu wawili ofisini. Nikamaliza nikaondoka zangu. Nilijua nimefanya vizuri na wao wakasema watajadiliana halafu wataona kama wataniita tena kwa duru ya pili.

Na kweli baada ya siku kadhaa nikaitwa tena kwenye duru ya pili. Mambo yakawa mswano.

Baadaye sasa kukaa na kufikiri na kujiuliza kwa nini waliniamboa niandike insha wakati resume yangu walikuwa nayo ndiyo nikahisi (baadaye nilikuja kujua) kwamba hiyo ni moja tu ya njia wanazotumia katika kuchekecha applicants.

Hawawezi wakategemea tu application letter na resume peke yake maana hizo mtu unakuwa umejitayarisha kuziandaa na kadhalika. Lengo lao ni kutaka kujua kama kweli sifa zako ulizoorodhesha kwenye resume zinaendana na uwezo wako.

Precisely,
Wengine wametumwa na kijiji wanaweza kuandikiwa hata by facsimile.

Unambana mtu hapo hapo.

Tatizo Kikwete na huyu fungu moja, sasa nani atambana nani?
 
nimemuuliza mkuu! navojua yule mjenzi ana insurance ya huo mjengo! hope watalipwa

Kwanza "watalipwa", pili "hope watalipwa", tatu "faili limepotea masijala" (masijala ni code word hivyo maana yake sijala nilishe)....
 
Kwanza "watalipwa", pili "hope watalipwa", tatu "faili limepotea masijala" (masijala ni code word hivyo maana yake sijala nilishe)....
mmmh hivi kaka huku jf hamna thread nyingine jamani? hadi tuaribiane sikukuu hivi hivi? twende mmu basi!
 
mmmh hivi kaka huku jf hamna thread nyingine jamani? hadi tuaribiane sikukuu hivi hivi? twende mmu basi!
Mwenzio Le Mutuz alikuwa anaambulia ban, maana kukomaa na Kiranga yataka ujiandae.
 
Patamu hapa, Smile umeingia cha kiume leo, unaambiwa tatizo ni umakini wala siyo lugha, tafuta series moja ya Wasouth Korea inaitwa IRIS ndio utamuelewa vyema Kiranga.
twende zetu kule tukacheki rangi za nanilii bwana
 
Kwa system corrupt kama yetu,Sera ya Public Private Partneship(PPP) bado kama taifa hatujajiandaa kiitekeleza.........Tutengeneza katiba mpya itakayo mpunguzia Head of state madaraka ya kuteua watu,tume huru ya uchaguzi itakayo simamia uchaguzi huru na wahaki ili kupata bunge bora litakalochagua speaker bora atakae simamia uchaguzi bora wa kamati za bunge ambazo zitahoji utendaji wa mashirika ya umma na kuleta utamaduni wa kuwajibika pindi mambo yanapokwenda ndivyo sivyo.
Suala Mchechu ni system failures,kuanzia kwa appointing authority wa DG na BoDs na hata POAC na Bunge kwa ujumla kutokuona mapungufu ya sera yenyewe na utekelezaji wake kwa case ya NHC.
Katiba mpya itatuletea vyombo huru si tu vya kusimamia serikali iliyo madarakani bali uwazi katika usimamizi wenyewe.
Ngoja niishie hapa,lakini hii haiondoi dhana ya Mchemu kuondoka
 
katika historia ya nchi hii sidhani kama alishawai kutokea kiongozi mwenye akili kama nehemia
jamaa ana maono ya mbali,
huo ubia wala hakuingia yeye na kuvunja mkataba sio jambo rahisi kama unavodhani.
ungeanza kulaumu tbs wanaokubali vifaa feki vya ujenzi kuingia nchini

singepenga kuside na upande wowote, ila nilifikiria kuwa MD wa NHC angewajibisha wahusika chini yake, mara moja, kwa uono wake kwa kuwa wameingizia shirika hasara na aibu.
Kabla yeye hajawajibishwa na bosi wake,
ila swala akili halipo hapa, hapa uadilifu, teamwork na integrity ndio vinaonekana kukosekana kuna mtu anaweza kuwasemea NHC kuwa wako makini katika haya?
 
mmmh hivi kaka huku jf hamna thread nyingine jamani? hadi tuaribiane sikukuu hivi hivi? twende mmu basi!

Thread zote zangu, unanipangia thread ya kuchangia sasa?
 
singepenga kuside na upande wowote, ila nilifikiria kuwa MD wa NHC angewajibisha wahusika chini yake, mara moja, kwa uono wake kwa kuwa wameingizia shirika hasara na aibu.
Kabla yeye hajawajibishwa na bosi wake,
ila swala akili halipo hapa, hapa uadilifu, teamwork na integrity ndio vinaonekana kukosekana kuna mtu anaweza kuwasemea NHC kuwa wako makini katika haya?

Kwa nini awawajibishe walio chini yake na yeye asiwajibike?

Tungekuwa Ujapani kabla ya mtu kusema lolote tungesikia tu "CEO kaangukia upanga wake mwenyewe katika hara-kiri". The honorable thing.

Ila huku bongo mtu kaua watu kibao kwa uzembe halafu bado anakuja JF kuleta "maneno mbofumbofu"!
 
ahaaaaa dah namuheshimu tu ..haniwezi huyu mbeba box

Hapo hapo unasema unamuheshimu mtu, hapo hapo unamuita "mbeba box".

Hata ukipewa kuandika line moja tu unaboronga pumbaa bin pumbaavu!
 
Back
Top Bottom