Uwekezaji wa NHC - Mchechu awajibike

Uwekezaji wa NHC - Mchechu awajibike

Hapo hapo unasema unamuheshimu mtu, hapo hapo unamuita "mbeba box".

Hata ukipewa kuandika line moja tu unaboronga pumbaa bin pumbaavu!
kwani kubeba box ni tusi kaka?
 
kwani kubeba box ni tusi kaka?

Mie mtani wako?

Ukaka umeupataje kutoka kwangu? Tumezaliwa pamoja au kujikaribisha ukaka tu?

Mie sikujui hivyo mpaka uniite kaka yako.

Na sifagilii ujamaa jamaa usio na kichwa wala miguu kama ndo kijijini kwenu umefundishwa hivyo.

Kama unafikiri kwa kuniita kaka kisago ulichoomba kitapungua umenoa.
 
Wengi tulisema tukapuuzwa, mchechu hayuko katika orodha ya CEOs bora, rafiki yake wa karibu mafuru yuko wapi leo!!!!! watu walimsifu lakini yanayoendelea leo NBC baada ya yeye kutoka ni michosho tupu bank ni kama inaanza upya, kwishney bank iliuzwa kwa bure leo kodi ya wabongo inachotwa kuongeza mtaji, ni ujinga.Ila ya NHC itakuwa sawa na HIROSHIMA just wait.
 
Kwa nini awawajibishe walio chini yake na yeye asiwajibike?

Tungekuwa Ujapani kabla ya mtu kusema lolote tungesikia tu "CEO kaangukia upanga wake mwenyewe katika hara-kiri". The honorable thing.

Ila huku bongo mtu kaua watu kibao kwa uzembe halafu bado anakuja JF kuleta "maneno mbofumbofu"!

Ni jamii inaposhindwa kuzomeya mchafu kama huyu, eti anajitokeza bingwa wa kutetea na kusifu mafanikio ya mzembe ili iwe kinga ya makosa.

Matokeo, jitu bovu linavimba kichwa na kusema, sijiuzulu ng'o! Nimelikumbuka na lile la Elimu yetu.
 
Hapa sidhani kwamba kuna chuki na DG wa NHC. Inashangaza DG wa NHC anajitoa katika sakata hili, wao NHC wanahusika kwa kiasi kikubwa na uzembe uliopelekea watu 36 kufariki. Inapaswa nao wawe ni miongoni mwa watu 8 wanahojiwa na Polisi kituo cha kati. Pamoja na kazi nzuri zote DG wa NHC anazofanya bado NHC kuingia mikataba ya rushwa na matajiri wa kihindi ndio chanzo cha kuanguka kwa ghorofa la ubia wa NHC na matajiri.

wewe hujui wahindi ndo "wamiliki wa nhc?
Kuanzia kwenye upangaji hadi mikataba?
Na utashangaa hili linapita.....na likiondoka na mtu basi vidagaa bya Nhc watatolewa kafara

Mkurugenzi na genge lake watapeta"
 
au zile 6 za nyongeza ni za asante? matokeo yake zimeshusha mzigo mzima...dah
 
Pasco huyu ni mchumia tumbo siku nyingi. Alikuwa Jeshi la Wananchi kukamshinda ndio akaibukia Radio Tanzania. Ni mmoja ya watu wanaomtetea sana huyu MD wa NHC. Halafu nasikia jamaa ametembeza bahasha iliyoendana na press release ili kina Manyenyre Jackton wamsafishe na waandishi wengine wamsafishe
Mkuu Machomdili,
Kwanza ni kweli nilipomaliza JKT niliunganisha JWTZ kwa sababu tuu ndivyo familia walivyotaka!, nikitoka familia ya wajeda kwa baba na mama hivyo nilipaswa kuwa mjeda!. Niliacha jeshi!, sio kwa kushindwa bali kutopenda tuu jeshi!. Since then nimekuwa mwandishi mpaka leo, na sio kwa sababu siwezi kazi nyingine yoyote, bali I'm just doing what I love most!.

Hili la mchumia tumbo nalo neno!, nadhani ukiondoa ualimu, the second less paying job ya wito ni uandishi wa habari!, hivyo ningekuwa mchumia tumbo, si ningeajiriwa kwenye PR?, badala ya newsroom nivute mkwanja wa maana tuu?!.

Katika kazi yangu ya uandishi wa habari for more than 15 years!, sijawahi hata siku moja, kuvutishwa bahasha hata ya seti tano toka NHC!.

Hili la kumtetea DG wa NHC, nitasimama nalo mpaka mwisho!, kwa sababu msingi mkuu wa taaluma ya habari ni kusema ukweli daima!, "nothing but the truth!". Sasa kama ni kweli Mchechu ameitransform NHC from nothing into something!, huna haja ya kuambiwa, you can just see the difference with your own eyes!.

Ila pia hii sio mara yangu ya kwanza kutetea watu humu JF ambao huwa wanahukumiwa papo kwa papo na hii ni baadhi ya mifano michache!.
kwa kawaida kwenye kila jambo kuna two sides, side moja ni the truth, na side ya pili ni the Perceived perception. Hii Perceived perception ndio public opinion. Mimi siku zote huwa nafuata the truth, sio public opinion.

Kuna issues nyingi natofautiana na watu humu kwa vile wengi huamini ile Perceived perception ambayo unfortunately sio the truth.The Truth ni mahakama ya Kadhi, haina problem kwa isiyowahusu!.Ila pia mimi nasimamia kwenye ukweli ninauamini.Mfano,


    • Kwenye kashfa ya Richmond, nilisimama na EL kuwa "he was condemned unheard" ambayo ni kinyume cha principals of natural justice!. Lowassa hakuonewa; alichelewa kujiuzulu!
    • Liumba anaonewa, huwezi kumshitaki kwa full value ya Twin Tower wakati jengo liko na limesimama. Angeshitakiwa kwa ile addition value iliyozidi ndio ingeitwa hasara. Kwa vile BOT, walibudget kiasi fulani kujenga Twin Tower, baada ya kukamilika walitakiwa wafanye kwanza uthamini wa jango kupata full value, wafanya value for money, any amout ambayo ni access ndio wamshitaki Liyumba kusababisha hasara. Japo rufani imekataliwa, Makakimu wetu ndi binadamu tuu kama binadamu wengine hawajamtendea haki. Kwa msimamo huu, nilishambuliwa sana!.
    • Kesi ya kina Mramba, Yona na Mgonja, nilisema sio kesi, ni danganya toto kwa JK kujisafisha mbele ya wafadhili na wananchi ili aonekane anachukua hatua, it is very weak case na itakuwa thrown out within no time.
    • Hata hii kesi ya Prof. Mahalu pia sio kesi kweli!. Hii ni visasi tuu kukomoana kwa vile Mahalu akiwa Balozi, hii deal alimbypass JK akiwa MFA, kwa ku deal direct na Ben, sasa maadam JK ndie top, sasa anamkomesha!. Mahakama ikitenda haki, this case will be thrown out!.
    • Kwenye issue ya Kagoda, mimi ni miongoni mwa waliosema kamwe haitafikishwa mahakamani, huku wengi wakimtaja Rostam, mimi nilikataa na bado nakataa, Rostam ni dalali tuu, wenyewe walikuwepo na bado wapo, watajifikishaje mahakamani?.
    • Na sasa kwenye hii issue ya malipo ya Dowans, mimi ni miongoni mwa wanaosema lazima tulipe kwa sababu hatuna pa kutokea. Wengi wanamtaja taja tena Rostam, mimi nawakatalia tena kuwa Rostam ni dalali tuu wa wenye mali. Nikasisitiza tutalipa sio kwa sababu ni halali, bali kwa sababu watoa uamuzi wa kulipa ndio wenyewe, hivyo wanajilipa wenyewe kwa fedha zetu!.
    Hivyo nimeshajizoelea kusimama kwenye ukweli ninao uamini, hata ukishutumiwa vipi, unabaki na amani moyoni mwako na dhamira yako haikusuti!.
Hao wote miliorodhesha hapo, sijawahi kupokea hata senti tano yao!. Na pia naomba niweke wazi msimamo wangu kumuunga mkono EL kwenye jukumu la kitume, kuhakikisha CCM inapata mgombea bora 2015!, pia ni kazi ya kujitolea tuu bure!. Mimi sio timu ya EL, wala sijawahi kukaa nae popote kwa hili, wala kukutana nae popote, wala kuhudhuria press conference zake zozote, au sherehe zake za Monduli, na kikubwa kuliko vyote, sijawahi kupokea hata senti tano ya EL au ya mwanasiasa yoyote kwa minajili ya kisiasa!.

Anayeniamini, aniamini, asiyesiamini asiniamini!.

Tuendeleeni na mjadala!.

Pasco.
 
nhc watalipa damage kwa familia kwani huo mjengo haukuwa na insuarance?

Kama kuna kampuni ya bima itakayolipa fidia kwa uzembe wa wazi kama huu, basi ipo Tanzania tu.
 
Asante!
Nguto,

Umeandika jambo moja muhimu sana kwa a common person kutakiwa kuliona...msingi wa nyumba unakuwa designed ku-accommodate a designed load..........sasa kwa uzembe uliotokea inabidi wajuzi wa-establish source of failures.....

Pili kuhusu insurance.....kwenye miradi ya Ujenzi....Mkandarasi ndio anakuwa ana-own the site......na Ujenzi wake unakuwa insured na Mkandarasi.....na pia kunakuwepo na bond kadhaa....cha msingi cha kuangalia, je zilikuwepo valid insurance ku-cover matukio/majanga (endapo litakuwa defined as janga au vinginevyo ili liwe valid kwa insurance compensation), je bond zilizopo ziko valid? na je zina-cover vitu gani, pia kuna masuala ya license liabilities......inabidi license za baadhi ya watu zisimamishwe NHC ni mojawapo......license zao zisimamishwe na zifanyiwe review......
 
Mama Nyoni ni mama mdogo wa Mchechu na mama Nyoni anamwita Luhanjo uncle...get the pic.?
 
Mkuu with due respect wewe hoja zako ndio hazina mashiko!

1. Unadai mkataba ulifungwa 2006 na kwa kuwa Mchechu aliingia 2007 hahusiki! wot a joke! Jengo limeanguka jana 2013 kwa taarifa yako. Kibaya zaidi mkataba ulikuwa wa kujenga ghorofa 10 tu ngoma imeendelea mpaka ghorofa ya 16! under watchfull of Mchechu!

2. Eti "sasa wanatembelea Hilux!" kichekesho mkuu, kutembelea Hilux ndio justification ya kuua watu 20+?

Huu utetezi ulioleta hapa ni mwembamba sana, sidhani hata kama unafahamu dhana ya kuwajibika ilivyo. Likibuma chini ya uongozi wako ndio lako hilo, kaingia toka 2007 kwanini ali review mikataba ya kimagumashi?

Mchechu has to go....

Without being disrespectful of you, mie nadhani tunataka kuhamisha lawama na uwajibikaji kutoka kwa serikali kwenda kwa watu binafsi. Seikali inatakiwa iwe na mifumo madhubuti ya kuhakikisha quality ya ujenzi wa majengo ya kila aina mpaka nyumba za watu za kawaida.

Ukiangalia mifano ya wenzetu kuna mfumo ulioshiba wa swala zima la ujenzi wa nyumba, huwezi kuibuka tu ukaanza kujenga hata kama ni mtu binafsi bila kupitia kwenye mamlaka zinazohusika. Nionavyo mimi ni kuwa uozo uliopo na uliokuwa calculated na serikali ya CCM wa kutokuwa na mifumo independent inayosimamia quality ya kila kitu ndio unaotucost.

CCM wamecreate mfumo holela si kwa bahati mbaya, wanajua mkiwa na mifumo independent inayoshughulikia quality, ufisadi hawataweza kufanikiwa kwenye malengo yao ya kupora mali za uma, maana unajua mwenyewe kuwa wanaCCM wa top brass si wanaitikadi ni kundi la wolves. Hilo litaendelea kututafuna mpaka tukakaposema basi tumechoka ondokeni.
 
katika historia ya nchi hii sidhani kama alishawai kutokea kiongozi mwenye akili kama nehemia
jamaa ana maono ya mbali,
huo ubia wala hakuingia yeye na kuvunja mkataba sio jambo rahisi kama unavodhani.
ungeanza kulaumu tbs wanaokubali vifaa feki vya ujenzi kuingia nchini

Watu mmemkomalia Msechu, ok let Msechu go, je itakuwa mwisho wa majengo kuanguka? The answer is no. Sasa kama No tatizo lipo wapi, tatizo lipo kwenye mfumo mzima wa quality check na integrity katika mamlaka zinazohusika na mambo mbalimbali katika taifa la Tanzania na wala si ujenzi peke yake.

Mbona tunashindwa kuchimbua kiini cha matatizo tunakimbilia kwenye symptoms?? Majengo kuanguka ni Symptoms za problem na sio problem, tutafute problem watanzania nyie vipi?? Sioni candidate wa urais hata mmoja hapa naona wote mmekomalia symptoms.
 
Akishajiuzulu ndo what, kwani yale majengo mengine yalodondoka alihusika yeye, kujiuzulu kwa sababu mfanyakazi wako kakosea haina tija kwani itacreate watu kufanya makusudi ili kuwatoa wasiowapenda kwenye title ndo mana hata Lowassa alipojiuzulu iliishia kula kwake tu, mikataba mibovu inaendelea tu kusainiwa na urais ndo asahau kwani tutakuwa watanzania wa ajabu kama tutampa nchi mtu ambae hata mbwa wa ikulu akibweka bila sababu yeye anajiuzulu on behalf

Yaani nimeshindwa kukutafutia kundi la kukuweka. Unafahamu nini haswa maana ya uwajibikaji, uongozi na uzalendo? Tuanzie hapo
 
Joshi anaugomvi personal na Msechu maana Msechu amejitahidi sana maana NHC ilikuwa mfu!!

Joshi usimharibie mwenzako kwa mambo personal bana!

Bora ingebaki mfu kuliko kusababisha makumi ya vifo kwa watanzania wenzetu
 
Back
Top Bottom