Utumishi, Wizara ya Fedha na TAKUKURU kwanini mnaruhusu watumishi wa umma kukopea mishahara yao hadi Senti ya mwisho? Hamuoni kuwa inachangia Rushwa?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,397
Kuna watu wamechukua Mikopo mikubwa sana na ndani ya mkopo hiyo wameongeza mikopo mingine tena juu kwa juu (inaitwa TOP-UP)

Sipo hapa kumpangia mtu Matumizi ya Mikopo yake; lakini swali langu je hao watumishi wanaokatwa mishahara yao yote kwa mikopo wanaishije kwa kubakiwa na chenji kwenye AKAUNTI?

Naomba utumishi, wizara ya fedha na TAKUKURU pigeni marufuku Mikopo holela kwa watumishi umma haina afya kimaadili!
 
Umbea, inakuhusu nini? pambana na ya kwako, mihahara ya watu haikuhusu. HuyuJiwe amewaondoa kufikiri kabia!
 
Umbea, inakuhusu nini? pambana na ya kwako, mihahara ya watu haikuhusu. HuyuJiwe amewaondoa kufikiri kabia!
inachangia Sana watu kutaka rushwa katika utumishi wao,
tatizo siyo umbea lakini Ukweli inachangia Sana watu Hawa kushawishika kufanya uovu! rushwa na umalaya
 
Hapa JF kuna watu wazushi ukiwemo wewe Mleta mada. Kwa taarifa yako Mtumishi akikopa makato yakaathiri 1/3 ya Gross pay yake makato hayapitishwi kamwe na huo mkopo hauchukui ng'oo. Rejea taarifa ya CAG ya mwaka huu kipengele cha Mishahara huwezi kukuta hoja kama hiyo.

Kama yupo mtumishi wa aina hiyo anayekatwa mpaka kubaki na elfu 5 unayosema tatizo laweza kuwa ALISHUSHWA MSHAHARA AKIWA TAYARI KAKOPA na hivyo kuathiri uhalisia, ANAKATWA DENI LA SERIKALI KUREJESHA FEDHA ZA HASARA AU WIZI, AMEBADILISHWA CHEO AU TAASISI KUTOKA KIKUBWA KUJA KIDOGO.

Huko serikalini upo mfumo ambao hauwezi kuruhusu mtumishi kukopa zaidi ya 1/3 labda kama kwa sasa haupo lkn najua kwa sasa ndio uppo imara huenda kutokana na maendeleo ya ICT.
 
Watu wameona wachukue chao mapema tutakatana mbele kwa mbele. Maana kutumbuliwa ni nje nje. Pia unaweza maliiza muda wako wa kazi kiinua mgongo chako kikawa nacho cha kusalandia kama demu wa kizanzibar.
 
halafu Mikopo yenyewe Ni kununulia magari yasiyozalisha hahahah dah,
 
Hapa JF kuna watu wazushi ukiwemo wewe Mleta mada. Kwa taarifa yako Mtumishi akikopa makato yakaathiri 1/3 ya Gross pay yake makato hayapitishwi kamwe na huo mkopo hauchukui ng'oo. Rejea taarifa ya CAG ya mwaka huu kipengele cha Mishahara huwezi kukuta hoja kama hiyo...
we acha tu Ndugu,. mabenki yanashindana kukopesha watumishi, hivyo wanakwangua hadi Senti ya mwisho! almradi Chao kinarudi!
mfano mtu mwenye mshahara wa laki sita, akikatwa mkopo laki nne, lakini mbili inakatwa katwa mifuko ya jamii na bodi ya Mikopo ya elimu kinachobaki hapo Ni Senti hakitoshi hata nauli kuja kazini!
 
Jana ijumaa nilikuwa napitia mafaili ya mishahara kwenye ofisi (X) ya umma!

Asilimia kubwa watumishi wa umma wamechukua Mikopo ya pesa nyingi kiasi wengine hukatwa hadi asilimia 98% ya mshahara yao!..
Mshahara wangu basic 1,235,000/=. Lakini takehome bila mkopo wowote ni 890,000/=. Inayobaki yote yote ni makato mbalimbali. Kodi ya mapato peke yake 223,000/=. Nitaachaje kukopa na ku topup. Wewe una posho za ziada nje ya mshahara. Mimi zaidi ya kudaiwa michango ya mwenge na ujenzi wa sekondari za serikali, sina posho yoyote.
Acha ujinga, fanya yako.
 
tatizo ni kutaka maendeleo ya mkato ghafla, mnakopa Hadi Senti ya mwisho
 
Hapa JF kuna watu wazushi ukiwemo wewe Mleta mada. Kwa taarifa yako Mtumishi akikopa makato yakaathiri 1/3 ya Gross pay yake makato hayapitishwi kamwe na huo mkopo hauchukui ng'oo. Rejea taarifa ya CAG ya mwaka huu kipengele cha Mishahara huwezi kukuta hoja kama hiyo.
Kama yupo mtumishi wa aina hiyo anayekatwa mpaka kubaki na elfu 5 unayosema tatizo laweza kuwa ALISHUSHWA MSHAHARA AKIWA TAYARI KAKOPA na hivyo kuathiri uhalisia, ANAKATWA DENI LA SERIKALI KUREJESHA FEDHA ZA HASARA AU WIZI, AMEBADILISHWA CHEO AU TAASISI KUTOKA KIKUBWA KUJA KIDOGO.
Huko serikalini upo mfumo ambao hauwezi kuruhusu mtumishi kukopa zaidi ya 1/3 labda kama kwa sasa haupo lkn najua kwa sasa ndio uppo imara huenda kutokana na maendeleo ya ICT.
ahsante sana, nilikuwa nafahamu kitu kama hiki. tatizo kubwa sana linalotunyemelea/kutuharibu watu siku hizi ni kuwa wengi ni kama vile tupo katika ushindani wa kuanzisha mada ili tuwe labda wa kanza kusema hiko kitu.......matokeo ndo hivi tunaleta mada ambazo hazijachunguzwa kwa undani kabisa
 
Mkuu usiwe mbishi! Mambo mengi Sana yenye utaratibu mbona yanafanyika kinyume na utaratibu?! au nikupe mifano mikubwa!?
Taratibu za manunuzi ya serikali zinasemaje? mbona tunatekeleza miradi mingi kwa maagizo?

Hata kwenye mishahara Ni hivyo hivyo, waajili wanaidhina Mikopo ya watu hivyo hivyo juu kwa juu!
 
Mkuu una wadhifa gani kufungua hadi strong room na kuanza kuperuzi mafaili ya watu? Hata hivyo kwenye faili hakuna salary sleep, wewe umejuaje yote hayo?

Hivi kimantiki ruhusa ya kukopa na kuidhinisha mwisho wa kiwango cha kukopa si kinatolewa ns mwajiri? Hapo mfanyakazi maskini ana kosa gani?
 
Mkuu una wadhifa gani kufungua hadi strong room na kuanza kuperuzi mafaili ya watu?
Hata hivyo kwenye faili hakuna salary sleep, wewe umejuaje yote hayo?
Hivi kimantiki ruhusa ya kukopa na kuidhinisha mwisho wa kiwango cha kukopa si kinatolewa ns mwajiri?
Hapo mfanyakazi maskini ana kosa gani?
kumbuka anaeomba mkopo ana influence kwa mwajiri wake
 
Back
Top Bottom