Mifumo ya kikabaila na kibwenyenye katika utumishi wa umma ndio chanzo kikuu cha Rushwa na ufisadi

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,701
36,121
Habari!
Rushwa si tabia ya mtu ya kuzaliwa nayo, Rushwa inatengenezwa na mazingira.

Hapa nazungumzia rushwa katika level ya utumishi wa umma.

Kijana anaanza kazi ofisi ya umma analipwa laki 5 huku akibahatika kuona salary slip ya bosi wake anakuta imeandikwa 7 million.
Na marupurupu juu.

Hata kama ni interval ya kielimu ndio mshahara ndani ya taasisi moja mtu apigwe gape la zaidi ya 1000% ?

Kijana umemaliza chuo mwaka mmoja na rafiki yako na mkaajiriwa mwaka mmoja wewe unalipwa 720k kwenye ofisi Y , yeye analipwa 1.4 kwenye ofisi X. na wote mko busy kujenga taifa. Je , ukiona mpenyo mpenyo wa pesa hutapita?.

Haya mazoea ya rushwa yakikua kwa kijana baadaye hata akiwa Waziri wa wizara au katibu mkuu wa wizara ataendelea kuiibia serikali kwasababu ameshajengwa katika mizizi ya rushwa na ufisadi.

Mfano: Kuna rafiki yangu alinikuta kazini, nilimtangulia mwaka mmoja. Tukalipwa sawa baadaye akahamia taasisi nyingine, kule mshahara wake uliongezeka karibu mara 2 na points kadhaa na posho iliongezeka kama mara 3 na points kadhaa ya ile aliyoiacha kazini kwetu. Hivi nini tutakiwaza sisi?

Kuhangaikia uhamisho kwenda kwenye neema au kuiibia serikali ili nasisi tuonekane watumishi wa umma. Haya yote ni mabaya kwa utumishi wa umma.

Ukiibia serikali umewaibia mpaka mafukara wa vijijini, ukitaka kuhama kisa pesa haitoshi pia ni tatizo hilo.

Within a year akanunua mkoko kama wa 20ml. Mimi natumia kigali cha third sijui second hand. Tena afadhali ya Mimi, kuna watumishi dhohofu lhali zaidi.

Serikali iachane na mfumo wa kibwenyenye katika utumishi wa umma.

Kuna watumishi wenye diploma ndani ya serikali hii ya Tanzania wanawazidi mishahara watumishi wenye degree licha ya kuajiriwa miaka sawia.

Ushauri. Ukiona tangazo la kazi usishobokee tu kufuata njaa zako, utaishia kuwa fukara au uwe mwizi ufungwe
 
Back
Top Bottom