OR-Utumishi na Utawala Bora inavyotekeleza kwa vitendo ilani ya CCM na kurejesha tabasamu kwa watumishi umma/wananchi 2021

JOYOPAPASI

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
250
408
OFISI YA RAIS UTUMISHI na UTAWALA BORA INAVYOTEKELEZA KWA VITENDO ILANI YA CCM NA KUREJESHA TABASAMU KWA WATUMISHI UMMA/WANANCHI 2021 .
(HEKO Mhe. Waziri Mchengerwa)

Na KASSIM MPINGI Rufiji-Pwani.

Kwa muda mrefu kilio Cha watumishi wa umma kilikuwa ni kupanda madaraja, Kulipwa Malimbukizo ya mishahara na stahiki zao nyingine.

Muda mfupi toka Rais Mhe. Samia atoe agizo kuwa watumishi wapandishwe madaraja na Kulipwa stahiki zao Waziri mwenye dhamana na wizara husika Mh. M . O . Mchengerwa na Wasaidizi wake walipambana usiku na mchana kuhakikisha agizo hili muhimu linatekelezwa na hatimaye katika historia ya Tanzania jumla ya watumishi wa Uma 178,000 wa kada mbalimbali nchi nzima walipandiashwa madaraja( Haijawahi kutokea Toka tupate Uhuru )
Sio tu kupandishwa madaraja bali pia kuidhinishwa kwenye mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara na wakati huo huo kuanza Kupokea mishahara mipya jambo ambalo lilirejesha tabasamu na hali ya uchapakazi Kwa watumishi.

Haikuishia hapo Mh.Waziri #Mchengerwa na wasaidizi wake walipambana usiku na mchana na kuhakikisha watumishi wa uma 37,388 wanalipwa malimbukizo ya mishahara.

Hapa katika hitoria ya nchi Yetu ikaandikwa jumla ya Shilingi 69,141,217,747.35 zikalipwa Kwa watumishi hawa na Kurejesha tena tabasamu lililopotea.

Wakati hayo yakifanyika ndani ya miezi mitatu tu ya uongozi wa Mh. Samia.
Kuna orodha Kubwa ya Watumishi wapatao 17,699 wanahakikiwa ili nao walipwe malimbikizo ya mishahara yao takribani 37,474,809,031.55

Ukiacha hili la kupandishwa madaraja, Kutoa mishahara mipya na Kulipa malimbikizo ya mishahara Kwa watumishi.
Juhudi za Mh.waziri na wasaidizi wake zimefanya Utumishi wa uma kuwa rahisi mno.

Leo hii imekuwa jambo la kawaida Kwa Afisa Utumishi wa Halmashauri kumpigia simu mtumishi na kutaka kujua changamoto zinazomkabili na kama ana madai au la Hili si jambo la kawaida hakika, kwani maafisa Utumishi katika halmashauri zetu walikuwa ni" Miungu Watu "

Kule kwenye Ajira nako mambo yakawekwa sawa upatikanaji wa vibali na Ajira umesimamiwa ipasavyo, vibali vya Ajira na mbadala vyenye nafasi 11,064 Kwa kada mbalimabali vimetolewa(Ndani ya muda mfupi) huku halmshauri Kadhaa na Taasisi zikapewa vibali vya kuajairi.

Na tamisemi kupewa kibali cha Ajira katika sekta ya Afya na Elimu .

Bila kusahau Jitihada za kuandaa mwongozo wa ikama na bajeti ya mishahara ya watumishi wa Umma 2021/2022 ambao umepelekea ka waajiri wote Tanzania.

Katika Kuhakikisha suala la utumishi na Mishahara inakuwa Salama,vwaziri na timu yake wanasimamia kikamilifu kukagua mfumo Wa taarifa za kiutumishi na Mishahara (HCMIS) nchi mzima Kwa idara na taasisi zote.

Idadi ya Watumishi wa Umma wanaopewa mafunzo katika chuo Cha utumishi wa uma imeongezeka ndani ya muda mfupi.

Hapo jumla ya Watumishi Wa uma 1,081 wanapewa mafunzo ya awali ya utumishi katika vyuo vya serikali( Homboro ),Chuo Cha uongozi wa mahakama (IJA) ili kujua misingi ya utumishi wa uma nakuongeza tija katika kuwatumikia watanzania.

Waziri na timu ya wasaidizi wake wameratibu utaratibu wa ajira Kwa watanzania Ili wapate fursa ya kupata kazi katika tasisi za kikanda .

Hili limefanikiwa Kwa watanzania kupata Ajira kwenye mashirika kama shirika la Utalii Duniani( UNWTO ), Jumuiya ya Madola, Jumuiya Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC) na Benki Ya Maendeleo Afrika( AfDB )

Waziri na Timu yake hawakubaki hapo hata wageni wanaofanya kazi Kwenye utumishi wa umma wameratibiwa na kupewa vibali katika namna ambayo watanzania watafaidika na maarifa/utaalamu wao( Knowledge Transfer ) ili kuwaongeza ujuzi watanzania .

Ili kuhakisha utumishi wa uma unakuwa na wataalamu wa kutosha wizara imeeingia Makubaliano na vyuo vikuu 13 Ili kunoa bongo za watumishi Wa Umma hasa kwenye Tehama ambayo ni nguzo ya Maendeleo ya Nchi.

Jitihada hizi zimepelekea Ujenzi Wa makataba Mtandao ukamilike Kwa 90% na kuingiza majarida na machapisho muhimu katika utumishi wa Umma bila kusahau ujenzi wa Maabara ya Kielectroniksi( e - laboratory ) na kukamilishwa Pamoja na kuweka vifaa mbalimabali vya electroniksi .

Kuboresha na kufungua mifumo ya kurahisisha utendaji kazi wa Serikali.
Mfano.e- Dodoso (Ukusanyaji taarifa na tathmini).
e-mikutano na e-bodi inayohusika na kuendesha mikutano Kwa njia ya video/Mtandao hapa tumeokoa mabilioni ya pesa ya kukusanya Watumishi/viongozi nakufanya mikutano Pamoja na pia tumesaidia sana katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa uviko 19 .

Bila kusahau e-malalamiko hapa mtanzania anaweza kutoa malalamiko yake Kuhusu huduma zitolewazo na taaisisi za uma.Tazama. ( )

Kule kwenye serikali Mtandao(e- government ) waziri na timu ya wasaidizi wake hawakubaki nyuma katika Kuhakikisha utendaji kazi wa Idara/taaisisi/wizara nyingine mfano Kwa kushirikiana na Wizara ya maji mfumo wa taarifa za maji " Maji Information System " na kuwezesha mamlaka zaidi ya 26 nchi nzima kusimamia huduma za maji kielektroniki.

Wameongeza Idari ya taaisi za uma zinazotumia huduma ya simu za mkononi nakufikia 176 na kurahisisha watanzania kupata huduma hasa ile ya malipo( GePG ) Kupitia simu zao.

Kule Kwenye mfuko wa Maendeleo ya jamii TASAF Mh.Waziri na timu yake wameendesha utambuzi na uhakiki Ili kubaini walengwa stahiki wa mradi huo Kwa Maendeleo ya Nchi. Hapa waligundua kuwa kaya 165,000 zimeboresha maisha na kaya na kaya 1992 zikijitoa Kwa hiari na kuokoa kiasi kikubwa cha pesa.

Huku TASAF ikitenga trilioni 2.03 kuzikwamua kaya zote masikini Tanzani katika Kipindi Cha pili awamu ya tatu 2020-2023(Haijawahi Kutokea Tanzania )

-Baada ya uhakiki ruzuku bilioni 135 zimegawiwa Kwa kaya 883,194 katika halmashauri zote 184 na kuanzisha utaratibu mpya wa malipo Kwa njia ya kietroniksi Simu/akaunti ya benki na hapa kuokoa kiasi kikubwa Cha pesa.

Takukuru imeboresha Jitihada zake za kuapambana na Rushwa na taarifa ya Transparent Internation ya mwaka 2021 Tanzania imepata alama 38 na kushika nafasi ya 94 kati ya nafasi 180 ilingamishwa na alama 37 na kushika nafasi ya 36 mwaka 2019 .

Takukuru pia inatajwa kuokoa bilioni 28.65 nchi nzima kwenye ufuatiliaji miradi ya Maendeleo.

Haya ni mfano tu wa baadhi ya Mambo ambayo Waziri Mh.O.Mchengerwa na timu ya wasaidizi wake wameyasimamia na kuyaboresha ndani ya muda wa mfupi tangu ateuliwe kuwa Waziri Ofisi ya Raisi Utumishi na utawala Bora.

Na hivi ndivyo wizara hii Inavyotekeleza ilani ya chama Cha Mapinduzi CCM na Kurejesha matumaini makubwa na Tabasamu Kwa Watumishi Wa uma na watanzania Kwa ujumla.

#KaziIendelee.
#HekoUtumishiNaNtawalaBora.
#UtumishiUliotukuka.
#KaziIendeleeNaRSSH
FB_IMG_1632219340066.jpg
 
#KaziIendeleeNaRSSHView attachment 1947036
Utafikili Nchi ilikuwa inaongozwa na chama kingine.
Haya bwana. Wajinga sisi.
 
Haya ofisa tumekupata. Ni wakati sasa wa kwenda ofisini, kuandikia per diem yako.
 
Back
Top Bottom