Sensei Tai
Senior Member
- May 26, 2022
- 126
- 359
Hili suala kiukweli linafikirisha sana
Hii inakua ni kama upendeleo kwa wakazi wa Dodoma pekee na kuwanyima nafasi ya kushiriki watoto wa masikini wanaotokea mikoa mingine
Juzi juzi niliona Waziri Jenister Muhagama akiongelea kwamba wameona ni bora kila mtu afanye usaili kwenye mkoa wake ili kupunguza gharama lakini hatuelewi huu mchakato umefikia wapi mana watoto wa masikini ndio tunaoumia kwa kukosa nauli za kwenda Dodoma pamoja na hela za accommodations.
Kuna haja serikali kuangalia kwa jicho la tatu hili suala mana wanaoumia ni watoto masikini, kushiriki usaili tunataka lakini tunakwamishwa na ukosefu wa nauli za kwenda na kurudi Dodoma.
Sijajua kama kupeleka saili Dodoma ni moja tu ya mbinu ya kupunguza watu au la, kama ni mbinu ya kupunguza watu basi hawatendi haki sababu written interview peke yake inatosha kabisa kupunguza watu kuliko hiki wanachokifanya cha kulazimisha saili zote zifanyikie Dodoma.
Serikali tunaomba muangalie upya hili suala la saili zote kufanyikia Dodoma mana dunia ipo Digital lakini sisi bado tunaendelea kukumbatia analog.
Tekelezeni kwa vitendo hili suala la kila muomba ajira kufanyia kwenye mkoa wake mana kwa kufanya hivyo mtakua mmempa kila muombaji haki ya kushiriki.
Asanteni