mazaga one
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 2,463
- 3,932
Habari wana bodi!
Mimi nikiwa mmoja ya vijana mtafuta ajira, mnaweza kuwa mashahidi wa ajira za utumishi zikifanyikia Dodoma zinakuwa fair sana kuliko zikifanyikia kwenye taasisi husika. Mfano ajira za vyuo vingi, zimefanyikia kwenye taasisi husika. Watu wengi nimesikia wakilalamika ya kuwa kuna upendeleo kwa waliosoma kwenye vyuo husika.
Mimi binafsi nashauri usaili Uendelee kufanyika Dodoma, kwani sio kwa ubaya. Dodoma ni rahisi kwa kila mtu kufika na gharama pia sio kubwa. Msailiwa yeyote anaweza kulala hata Chuo Kikuu cha DODOMA pale bure.
Lakini pia mazingira ya usaili yanakuwa ni fair kwa kila msailiwa. Yale mambo ya kusema kikanda, sijui usaili ufanyike kwenye taasisi husika iliyoajiri kama saili za vyuo zilivyofanyika, binafsi naona hayana afya kabisa.
Kiufupi nimefuatilia hata mahudhurio ya saili zilizofanyika kwenye taasisi husika mahudhurio ya wasailiwa yamekuwa hafifu sana. Mfano usaili wa SUA, Mzumbe, OUT na kwingineko wasailiwa wengi hawakufika kwenye saili na hii ni ishara tosha ya wengi wao kukata tamaa kutokana na usaili kufanyika kwenye taasisi husika kuliko Kufanyikia Dodoma.
Mimi napendekeza Dodoma saili za ajira ziendelee kufanyika kutokana na sababu nyingi nzuri na ambazo zinaweka mazingira ya usawa kwa wasailiwa wote.
Lakini pia ule utaratibu wa Utumishi kufanya usaili siku za weekend, labda Jumamosi na Jumapili, ikienda sana basi ni Jumatatu, ungeendelea kuliko sasa wanavyofanya siku za kazi.
Nawasilisha,
Ni mazaga One,
Kwa Sasa Dodoma,
Wale mnaokuja Dodoma kwenye usaili tukutane, nami Utumishi wameniita usaili Dodoma.