Utumishi hapa mmeyumba ingawa ni mwanzo mzuri

Sensei Tai

Senior Member
May 26, 2022
126
359
Nimeona tangazo la kuitwa usaili TRA waombaji watafanyia Written Interview kikanda katika mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Mbeya na Mwanza.

Ni mwanzo mzuri katika utekelezaji wa agizo la serikali ili kuwapunguzia gharama waombaji wa hizo nafasi kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine kwaajiri ya kuhudhuria usaili.

Makali naona kidogo yamepungua kwa waombaji ambao always wanafanya tu interview mbili kwa maana ya Written na Oral ila kwa wale watu wa kada ya ICT ambao always wanafanya interview tatu bado naona shida ipo palepale

Mfano hai ni ile nafasi ya ICT OFFICER II (DEVELOPER/PROGRAMMER) ambapo ni interview moja tu ya written ndo inayofanyika kikanda lakini zinazofuata zote kwa maana ya practical na oral zote zimeelekezewa Dodoma katika chuo cha UDOM

Baada ya written interview tarehe 18 December muombaji wa nafasi ya ICT OFFICER II (DEVELOPER/PROGRAMMER) atatakiwa asafiri tarehe 30 December ili tarehe 31 ahudhurie practical interview kisha baada ya hapo akae Dodom kwa siku tatu ili tarehe 03 January ahudhurie usaili wa Oral

Sasa gharama za kukaa Dodoma kwa siku tatu sisi walalahoi tutazimudu kweli ??? mana kufika gari utapanda hata lori utafika ila kuishi ndani ya hizo siku tu kuanzia malazi, chakula na emergency za hapa na pale sio jambo jepesi.

Vyuo ambayo vimetengwa kwaajiri ya usaili wa written kwa kanda zote vyote vina mifumo ya computer sasa kwanini na practical interview isifanyike kikanda ?

Utumishi embu tuoneeni huruma watoto wa masikini ......hali ni mbaya sana mtaani

Najua hili mtaliona na mtaenda kulifanyia kazi haraka sana ili kuleta unafuu kwa watu wote especially waombaji wa kazi ambao wanatakiwa wafanye interview tatu.

Asanteni
 
Kama Mwanzo hata Usaili mmoja haukuwa kikanda na bado watu tukipambana tutashindwa hii ya Sasa mkuu..
Me naona wanakuja kidogokidgo ili kutusave watafuta Ajira.. na naamini hata Mimi niliyoko Huku Kigoma ndanindani siku moja nitafuatwa hukuhuku kufanya Usaili wangu
 
Back
Top Bottom