Ni heshima kwa Tanzania kuwa mwenyeji mkutano wa wakuu wa nchi Afrika Mashariki

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
Leo ndo ile siku imewadia ambapo Mkutano wa Wakuu wa Nchi Afrika Mashariki wa siku mbili utaanza huko Jijini Arusha ambao awali ulipaswa nchini Burundi, kura imeiangukia Tanzania ambayo imetajwa kung’ara katika Masuala ya Diplomasia za Kimataifa.

Ni wazi kuwa kwa Afrika Mashariki Tanzani inaendelea kuwa na raia wanaoishi kwa amani na kudumisha hisia za umoja na utaifa mmoja bila kuwa na mgawanyiko wa udini, rangi au ukabila licha ya kwamba kuna makabila zaidi ya 130.

Juhudi zinazofanywa na Rais Samia kuijenga nchi kwa Serikali kuwa sikivu, kupokea maoni mbalimbali ikiwamo ya kuboresha mazingira mazuri ya kibiashara na uwekezaji zimefungua fursa nyingi za wageni kuitembelea Tanzania

Mkutano huo wa Viongozi Wakuu wa nchi hizo utakuwa chini ya Mwenyeji wao Rais Dk Samia Suluhu Hassan, William Ruto wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda, Evarist Ndayishimiye wa Burundi, Felix Tshisekedi wa DRC, Salva Kiir wa Sudan Kusini na Yoweri Museveni wa Uganda.

#Mguukwamguu2025
 
Heshima ya Nini kwa huo mkutano wa matapeli? Kipi huwa kinatekelezwa labda? Waulize sarafu ya pamaja imefikia wapi mwaka zaidi ya 20 huu?
 
Amani ipi unayoiongelea mama mwenye watoto 4 amekutwa na vipande 12 vya nyama ya swala kafungwa miaka 22 wengine wanakula urefu wa kamba zao.
Udini upo
Ukabila upo
 
Back
Top Bottom