Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,270
- 9,716
Ndugu zangu Watanzania,
Marais na viongozi wetu wote wa jumuiya ya Afrika mashariki wamekubaliana kwa kauli moja kumuunga mkono waziri mkuu wa zamani wa kenya wakati wa utawala wa mwai kibaki Mheshimiwa Raila Odinga katika nafasi ya Uwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika.
hayo yamesemwa na Rais wa kenya Mheshimiwa William Ruto kuwa kwa pamoja viongozi wa EAC walijadili kwa kina na kufikia muafaka wa kuamua kumuunga mkono mgombea Raila Odinga ambaye anatokea ukanda huu wa Afrika mashariki.
Nimeona niwaletee habari hii kwa kuwa awali watu walivumisha habari na taarifa kuwa Mheshimiwa Rais wetu mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa anawania nafasi hii. Lakini ukweli ni kuwa kama Mheshimiwa dkt Jakaya Mrisho Kikwete angeamua kugombea nafasi hii Basi angezoa kura zooote za ndio za wajumbe, na naamini hakuna mgombea ambaye angependa kushindana na dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika sanduku la kura,maana katika siasa za kimataifa na Afrika kwa ujumla dkt Jakaya Mrisho Kikwete ni mwamba na Jabali kwelikweli na hana wa kushindanishwa naye wala kushindana naye kwa viongozi waliostaafu.
Anapendwa na kukubalika sanaa tena sana barani Afrika na hata nje ya Afrika.ndio maana mnaona namna ambavyo amekuwa akipewa majukumu mbalimbali hapa barani Afrika,kama vile kuongoza timu za uangalizi wa chaguzi mbalimbali zinazofanyika hapa barani Afrika kama ambavyo hivi majuzi alivyotoka kufanya majukumu hayo nchini Congo.
Kwa undani zaidi wa taarifa hiyo ya viongozi wa Afrika mashariki kuamua kumuunga mkono Mheshimiwa Raila Odinga, nunua na kasome gazeti la Mwananchi ambako ndiko niliko itoa habari hii .ndio maana nimeona nieleze ili ukitaka kuelewa kwa undani basi iwe rahisi kwako msomaji wangu wa jamii forum kwenda moja kwa moja ndani ya gazeti la Mwananchi.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.