Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,506
- 113,626
Mzee Mwanakijiji, nakubaliana na utetezi wako kwa kiasi fulani kuwa Ngeleja anacho tuu kile alichopewa, jee wakati anapewa hicho alichopewa, alipangiwa malengo?, kama alipangiwa malengo na akanyimwa nyenzo za kuyatekeleza, aliwaambia hao wapanga malezo jee nyenzo vipi?.hili halina shaka lakini Ngeleja anacho kile tu ambaco amepewa. Kumuwekea mtu malengo ya kufikia kitu fulani halafu humpi nyenzo za kufikia malengo hayo kunawanyima waliompa malengo hayo kumdai kwanini hajayatimiza.
Hapa sasa ndipo tulipotaka Ngeleja aonyeshe uwezo, unawekewa malengo na unakubali kuyatekeleza only kama unao uwezo huo, serikali yetu inatumia utaratibu wa OPRAS, unakaa na mkubwa wako (rais), unapangiwa malengo, mnajadili utekekelezaji within specific time frame. Mkifika katikati, mnafanya MTR (Mid Time Review) na hapa ndipo una determine kama utatimiza malengo at the end of the time kama hutatimiza unasema na unatoa na sababu, Ngeleja aliyafanya haya?.Lakini vile vile wale wanaoweka malengo wanamuwekea malengo ya namna gani?
Ni kweli ni Baraza ndilo huamua, lakini Ngeleja alikwenda with a plan huko baraza na ikakataliwa?. Kwa mwananchi wa kawaida, we don't care about the means, we want results, kwetu sisi ni "The end, justify the means", at the end of the day, hatuna umeme, tunataka uwajibikaji, kwa maoni yangu sio Ngeleja tuu, wananchi tunamtaka JK awajibike kwa hili, 2015 is too far!.Huwezi kumwambia Ngeleja atatue tatizo la umeme wakati uhuru wa kufanya hivyo unaamuliwa na Baraza la Mawaziri.
Kama huko cabinet wana vichwa vyote hivyo, kina Magufuli, kina Mwandosya, kina Sitta, etc. etc wamefanya nini kwenye hili?. Aren't they are all nothing?!.