Utetezi wangu wa wazi wa William Ngeleja - The use of Emergency Powers Act 1986 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utetezi wangu wa wazi wa William Ngeleja - The use of Emergency Powers Act 1986

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 18, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Na. M. M. Mwanakijiji

  Utangulizi
  Tatizo la upungufu wa nishati nchini linatafutiwa kisingizio. Naam, limetafutiwa kisingizio na kisingizio hicho kinazidi kukuzwa mbele ya macho yetu na kufanywa ndio sababu. Kwamba, hali ya upungufu wa nishati ya umeme nchini inatokana, imesababishwa, imeongezwa na kudumishwa na Waziri wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleja. Hivyo - hitimisho linapendekezwa - kwamba Waziri Ngeleja awajibishwe na hata wengine wamefikia mahali pa kutaka baraza zima la mawaziri lijiuzulu.

  Utetezi wangu huu una lengo moja nalo ni kutaka sababu ya tatizo la upungufu wa nishati nchini iwekwe wazi, ikubaliwe na iwajibishwe. Badala ya watu kuzunguka mbuyu na kuuimbia kama wanga, wasimame na kuung’oa mbuyu huo. Utetezi huu haumhusu Ngeleja kama mtu - kwani sina ujamaa, undugu, au hata urafiki wa karibu - bali yeye kama Waziri mwenye dhamana ya Nishati na Madini. Kwamba, ninachosema na kupendekeza kwako msomaji ni kuwa wakosoaji wa Ngeleja wanataka kumkosoa na kumbembesha mzigo ambao mwenye kuustahili haugusi wala kuonesha anawajibika kwao.

  Sitojaribu hata kidogo kuingia kwa undani kuchambua historia, sera mbalimbali au hata kuingia kufafanua mambo mengine mengi yanayohusiana na tatizo hili kwani ninayachukulia kwamba msomaji wangu atakuwa ana uelewa wa kutosha na anaweza kufanya mwenyewe utafiti kudogo kujibu maswali mbalimbali ambayo yanaweza kubakia katika fikra zake.

  Ngeleja amekuta tatizo la umeme Tanzania.
  Kwa mtu yeyote ambaye amewahi kuchukua muda kidogo kufanya utafiti wa hali ya nishati nchini na hususan nishati ya umeme atakuwa ametambua jambo moja dhahiri kuwa tatizo la nishati hiyo nchini halikuanza mwaka 2011. Naam, halikuanza mwaka 2005 au hat amwaka 2000. Ni tatizo ambalo kukua kwake kumekujalikana kwa karibu miaka ishirini sasa. Upungufu wa nishati ya umeme haujatokea nchini kama mvua ya jua kali ambayo inatokea bila kuwa na mawingu! Kweli, tatizo hili halijatokea kwa sababu kuna mtu alitupiga dawa ya usingizi taifa zima na tulipoamka tukakuta kuna upungufu wa umeme

  Hadi tumefika mahali taifa zima tunapigishwa magoti mbele ya hali mbaya ya tatizo la nishati tujue kuwa imechukua karibu miaka 25 kufika hapa. Tumefikishwa hapa siyo na njama toka kuzimu bali kutokana na maamuzi mbalimbali na kati ya maamuzi hayo hakuna ambalo lilifanyika bila kujua hali ya umeme nchini.

  Ninachopendekeza ni kuwa hatuwezi kutenganisha tatizo la nishati nchini leo hii, matokeo yake mabaya katika maisha ya kiuchumi ya taifa letumna athari zake za moja kwa moja katika kupiga hatua kubwa mbele (The Great Step Forward) ya maendeleo kwetu sisi wa kizazi hiki na uzao wetu huko mbeleni na uongozi wa sera na kisiasa pamoja na utawala wa Chama cha Mapinduzi. Kwamba, matatizo ya nishati nchini yana uhusiano wa moja kwa moja na sera pamoja na utekelezaji wa sera hizo katika miaka thelathini iliyopita. Naomba mniruhusu nipitie tu baadhi ya sera na miongozi ya kisiasa chini ya Chama cha Mapinduzi.

  Mwongozo wa CCM wa 1981
  Mwaka huu ni miaka thelathini ya mojawapo ya nyaraka muhimu za kisiasa nchini. Kama Azimio la Arusha lilipanga miaka ya sitini, na Siasa ni kilimo pamoja na Ujamaa vijijini vilipamba siasa za miaka ya sabini, naweza kusema kuwa Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 ulipamba sehemu kubwa ya nusu ya kwanza ya miaka hiyo. Ni nyaraka ambayo hata leo bado nguvu ya hoja zake inasimama.

  Mwongozo ulisema hivi “Suala la nishati ni la msingi kwa maendeleo ya Taifa letu. Pamoja na kuendelea kutafuta mafuta, Chama kitahakikisha kuwa serikali inazidisha mipango thabiti itakayoliwezesha Taifa kuanza kutumia nguvu za maji, makaa, upepo na jua. Pamoja na miradi mikubwa ya nguvu za maji kuna haja ya kutia maanani miradi midogo midogo ya nguvu za maji. Suala la kuni itabidi lipewe umuhimu mkubwa kwa kuwa na mipango kamambe ya kupanda miti vijijini na miradi ya Mikoa na Taifa. Chama kiihimize Serikali kuendelea na kutafuta mbinu za kutumia makaa ya mawe tuliyonayo kusukuma uchumi wetu. Umuhimu wa suala la nishati utahitaji sera maalum”

  Ni wazi kuwa haja ya kuendeleza vyanzo vya nishati si jambo ambalo limeanza wiki iliyopita Bungeni. Lina miaka thelathini chini ya watu wale wale, chama kile kile chenye sera zile zile. Inashangaza watu wanashangaa kukutana na matokeo yale yale.

  Azimio la Zanzibar 1991
  Kama kuna maamuzi ya kisiasa ambayo mrindimo wa mwangwi wake unaendelea kusikika hadi leo hii ni maamuzi ya Zanzibar ya mwaka 1991. Maamuzi yale yalibadilisha mwelekeo wa kiuchumi wa taifa letu na kwa namna moja au nyingine (nitawaacha wengine waamue hili) ulikoleza kuibuka kwa mgongano kati ya watawala na watawaliwa, na kuibuka kwa tabaka la kinyonyaji la mafisadi. Maamuzi ya Zanzibar hayakuanisha sana suala la haja ya kushughulikia tatizo la nishati. Yalihusu zaidi umiliki wa mali za uchumi na kulegeza masharti ya uongozi ikiwemo kutengeneza msingi wa ubinafsishaji wa mashirika ya umma ambao ulikuja kufanyiwa kazi sana na Rais Mkapa baadaye.

  Sera ya Nishati ya 1992
  Tukiwa njiani kutoka mfumo wa chama kimoja cha kisiasa kwenda vyama vingi na tukiwa chini ya uongozi wa chama hicho kimoja tuliandaliwa sera ya nishati ya taifa. Sera hii ilitolewa na Wizara ya Maji, Nishati na Madini ambayo wakati huo ilikuwa ikiongozwa na mmoja wa viongozi wasomi ambao walikuwa wameingia tu umri wa kati lakini mwenye sura na mvuto wa Ujana Jakaya Kikwete. Sera hiyo ya nishati ilisema mambo mengi lakini hakuna lolote mabalo linasemwa kwenye sera hilo ambalo laweza kuwa geni kwenye masikio ya Watanzania.

  Sera hiyo ilitudokeza jinsi mpango wa Kufufua uchumi wa miaka ya themanini ulivyokuwa na malengo makubwa matano. Malengo yote matamu hayakuhusisha moja kwa moja kuongeza nishati kama njia ya kusisimua uchumi zaidi. Kwa kiasi kikubwa mipango yote ya wakati ule ilikuwa na lengo la kutimiza kile tulichokiita “ruksa” ambapo mikopo ya kigeni iliweza kuingia zaidi, uchumi kufunguliwa n.k. Chama cha Mapinduzi wakati huo hakikuweka msingi wa kuongeza uzalishaji wa nishati kama Mwongozo wa 1981 ulivyodokeza.

  Kwa ufupi utawala wa Rais Mwinyi, japo unasifiwa kwa kufungua uchumi na kuwezesha vitu vingi kufurika kwenye maduka yetu (kufuatia uhaba wa bidhaa wa mwanzoni mwa miaka ya themanini) ulishindwa kulifanyia taifa jambo moja kubwa na la msingi kuliruhusu kuwa na uhuru wa kiuchumi. Hakukuwa na ruksa ya kuzalisha umeme na ziada. Chama cha Mapinduz hakikusimamia serikali yake wala kuisukuma kutekeleza sera ya uhuru wa nishati.

  Sera ya Ubinafsishaji ya Mkapa
  Rais Mkapa, alipoingia na uongozi wake hasa ngwe ya kwanza alisimamia na kusukumiza ubinafsishaji wa mashirika mbalimbali ya umma. Nimepitia juzi orodha ya makampuni mbalimbali (makubwa na madogo) ambayo yalikuwa yametaifishwa na seriakali wakati wa Mkapa hadi ilipofika mwaka 2003. Hadi Juni 2003, kulikuwa na mashirika 138 yaliyobinafsishwa kwa Watanzania kwa asilimia 100; mashirika 20 yaliyomilikishwa wageni kwa asilimia 100; na mashirika 42 kwenye ubia.

  Mojawapo ya vitu vinavyonishangaza sana ni jinsi gani wataalamu wetu wa ubinafsishaji walivyopima hali ya nishati nchini kiasi cha kuweza kuuza makampuni mbalimbali ambayo walitarajia yangeweza kutengenezwa na kurudishwa katika uzalishaji karibu yote kwa wakati mmoja. Tukumbuke kuwa makampuni mengi yaliyokufa au kuwa na hali ngumu yalikuwa hayatumii nishati zaidi kama zamani. Kitendo cha kuyauza na kuhimiza kuyarudisha kwenye uzalishaji ni wazi kingesababisha ongezeko la mahitaji ya nishati ya umeme nchini.

  Kosa kubwa ambalo lilitokea katika sera ya ubinafsiji hususan suala la nishati linapokuja ni kutokuendeleza vyanzo vya nishati kukidhi mahitaji ya makampuni ambayo yalikuwa yanarudishwa kwenye uzalishaji au yaliyokuwa yanaanza kuzalisha bidhaa nyingine na kujipanua zaidi. Najenga nadharia (ningependa kuwaachia wataalamu wetu kupima kama ina ukweli) kwamba sera ya ubinafsishaji iliyotukuzwa kwa mafanikio yake na Dr. Kigoda mwaka 2004 imechangia kwa kiasi chake kusababisha upungufu wa nishati. Kwamba kisima cha nishati kilichokuwepo kilitosha watu wachache waliokuwepo na hasa wazee wachache, lakini tulipopata mwamko wa kuleta wanafamilia, jamaa na marafiki kijijini tulijikuta kisima chetu kikishindwa kuwahudumia vya kutosha.

  Serikali ya CCM wala Wabunge wake hawakuisukumiza serikali kuendeleza nishati ili kuzalisha zaidi na ziada kuweza kukidhi mahitaji ya viwanda vinavyobinafsishwa, vipya na vya uwekezaji.

  Sera ya Kikwete ya Uwezekaji

  Rais Kikwete alipoingia madarakani aliingia akiwa na “credentials” labda kuliko kiongozi mwingine yoyote nchini. Kati ya wizara nyeti nchini ni moja tu haikuishika yaani ile ya Ulinzi na JKT lakini kwa kuwa ni mmoja wa makamisaa wa zamani wa kijeshi naweza kusema hiyo pia ilikuwa ni sifa nyingine. Wizara alizoshikilia kabla ya Urais ni Wizara ya Maji, Nishati na Madini, Wizara ya Fedha, na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje.

  Sifa hizo zingemfanya kuwa kiongozi ambaye ana maono mapana ya kuelewa matatizo ya Watanzania na vile vile kuweza kuelewa baadhi ya masuluhisho. Alipoingia madarakani alitekeleza kile ambacho sisi wengine tumekibeza nacho nacho ni “kutukuza wawekezaji”. Ugomvi mkubwa kati yetu wakosoaji wake ni zile safari zake na mipango yake ya kualika “wawekezaji wa nje” kuja kuwekeza. Tatizo ni lile lile ambalo tunaliona kwenye sera ya ubinafsishaji ya Mkapa - wote wawili wakiwa ni wana CCM na wakiongoza Mabunge ya CCM na serikali ya CCM!

  Kwa kualika na kufungulia mlango kwa wawekezaji wa kigeni nchini CCM na serikali yake imeongeza tatizo la nishati. Tukumbuke kuwa kanuni za fizikia zinafanya kazi. Kuongezeka kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi za kawaida tu, na kuongezekana kwa viwanda na huduma nyingine mbalimbali kumesababisha ongezeko la mahitaji (demand) ya nishati nchini. Wengine wanasema “kukua kwa uchumi” ndio kumesababisha hali hii, naomba nitofautiane nao kiufundi tu - kwamba ni ongezeko la mahitaji ya nishati kutokana na sera za ubinafsishaji na uwekezaji zisizoendana na ongezeko la uzalishaji wa umeme ndio vimechangia sana tatizo la umeme la sasa.

  Mfano mzuri wa kuelewa ni kushikilia rubber band kati ya vidole viwili - upande mmoja kuna uwekezaji mkubwa, upande wa pili kuna ubinafsishaji na makampuni ya ndani na katikati yake shughuli nyingine zote za uzalishaji mali. Kwa kadiri shughuli zinakua zinatanua mpira ule ambao unawakilisha uwezo wetu wa nishati. Ndugu zangu, rubber band unaweza kuitanua hadi kiasi kwamba kutanua zaidi kutasababisha ikatike. Ni jambo ambalo linaweza kuoneshwa kimahesabu (nitawaachia wengine kuweza kugundua ni kwa kiasi gani tunaweza kutanua uwezo wetu wa nishati kabla hatujashindwa). Ninaamini hali ya sasa imefikia mahali ambapo hatuwezi kutanua zaidi bila kusababisha matatizo kwenye uchumi.
  [​IMG]

  Hivyo basi, tunaweza kusema pasipo shaka yoyote ile, tatizo la nishati nchini limetokana, kutengenezwa na kudumishwa kwa muda mrefu na kutotekelezwa kwa sera bora za nishati nchini. Na hili lote linarudisha mzigo kwanza kabisa kwa Chama cha Mapinduzi kwani ndicho kwa miaka hamsini kimeshikilia utawala wa nchi, na ndicho ambacho kimepanga safu yote ya viongozi wa kisiasa na kutoka kwao viongozi wa serikali nchini. Lakini pili, lawama zinawaendea moja kwa moja wabunge wote wa Chama cha Mapinduzi - siyo Ngeleja peke yake - kwa kushindwa kusimamia serikali na kutoa uongozi unaostahili kwenye suala la nishati. Wabunge ndio wanatunga sheria, ndio wanatenga bajeti na ndio wanasimamia serikali.

  Inanishangaza kuona wabunge wa CCM wanakuja juu dhidi ya Ngeleja. Kama wangetaka kutatua tatizo la nishati wangeweza kufanya hivyo miaka ishirini iliyopita. Hata kesho wakitaka wanaweza kuondoa tatizo hili kwa kiasi kikubwa. Wabunge wa CCM na Chama chao hawana udhuru wala uwezo wa kukwepa lawama za moja kwa moja. Ngeleja katika hili ni ni punje tu ya mtama ghalani! Tatu, tukubaliane kuwa serikali imeshindwa kwa njia za kawaida kutatuta tatizo la nishati.

  Hivyo basi, tunabakiwa na kile ambacho naweza kusema kutumia njia zisizo za kawaida kupata ufumbuzi wa muda wakati tunajiandaa na ufumbuzi wa muda mrefu. Kwenye Kiingereza wanasema “desperate situation calls for desperate measures” yaani wakati mgumu unahitaji hatua ngumu. Ndugu zangu, tatizo la nishati nchini linaweza kuondolewa kwa njia ya dharura ndani ya kati ya siku 30 na 60. Lakini hili litahitaji uongozi na uthubutu hasa wa wanasiasa wa CCM.

  Hatua zifuatazo:

  Hatua ya Haraka ya Muda Mfupi


  Emergency Powers Act 1986

  1. Huu ni Uamuzi wa Nyuklia (Nuclear Option) - ninachokiita uamuzi wa nyuklia sizungumzii matumizi ya nishati ya nyuklia bali uamuzi wa kikatiba wa kutangaza hali ya hatari chini ya Sheria ya Madaraka ya Rais wakati wa Dharura ya Mwaka 1986 (Emergency Powers Act). Hivyo, la kwanza kufanyika ni kwa wabunge kumtaka Rais Kikwete atangaze hali ya hatari/dharura nchini chini ya Ibara ya 32 ya Katiba. Rais akitangaza hali ya dharura nchini kutakuwa na matokeo mbalimbali ya kisheria na kiutendaji kwani yeye pekee atakuwa na madaraka ambayo mtu mwingine au chombo kingine chochote hakina.

  2. Kutokana na hilo la 1 Rais Kikwete atakuwa mtu mwenye nguvu katika lile jambo aliloliamua yaani kushughulikia tatizo la nishati. Atakuwa na madaraka ya kusimamisha sheria na kanuni mbalimbali (suspending the law) na hivyo kuondoa haja ya kufanya mabadiliko ya sheria ya manunuzi ili kuruhusu mitambo iliyotumika kuingizwa nchini. Chini ya Ibara ya 18 ya Sheria ya Madaraka Wakati wa Dharura Rais ataweza kusimamisha sheria hiyo hadi tamko la hali ya dharura litakapoondolewa.

  3. Rais akishatangaza hali ya hatari na kusimamisha sheria kadhaa au vipengele kadhaa vya sheria hususana kwenye jambo hili la nishati (katika hoja yetu sheria ya manunuzi ya Umma -PPA na hata sehemu ya sheria ya fedha) Rais ataweza kujadiliana moja kwa moja na watengenezaji wa majenereta na kuagiza kutoka kwao moja kwa moja bila kusubiri kamati, vikao au baraka za Bunge - Bunge bado lina uwezo wa kupitia uamuzi huo baadaye. Kwa kutangaza hali hiyo ya dharura siyo tangazo lisilo na nguvu la “janga la kitaifa” Rais atakuwa amejipa jukumu ambalo Watanzania wanatamani waone analichukua nalo ni kuondoa tatizo la nishati. Kwa kususpend sheria hii Rais anaweza kuunda timu maalum kumshauri - ufundi na bajeti - kuweza kupata dili nzuri bila kutumia kuwadi yeyote. Wabunge wanaweza wakatoa wito huo na Rais afanye uamuzi badala ya kukaa pembeni kama vile hausiki au kuwaachia wengine. Hili ni jukumu lake kubwa na la msingi wakati huu. Badala ya kwenda kuwaita wawekezaji atumie muda kutatua tatizo la nishati vinginevyo anajitahidi kutanua rubber band yetu halafu anakaa pembeni kuangalia itakatika vipi!

  Hilo litaondoa tatizo la wakati huu kwani chini ya hicho nilichopendekeza tunaweza kuingiza majenereta ndani ya miezi miwili tu.

  4. Chini ya Sheria hiyo hiyo ikifanyika wakati wa dharura Rais anaweza kunegotiate bei na hata kuamua bei ya kulipa mafuta kwa sababu ni hali ya hatari badala ya kulipa bei ya soko - kwa vyanzo vya ndani. Hili linawezekana chini ya Ibara ya 12:1 ya sheria hiyo.

  Wanaposema kuwa wao ni watu wa “utawala wa sheria” wajue kuwa mojawapo ya sheria ni hiyo ya wakati wa dharura na ni maoni yangu ya muda mrefu kuwa Tanzania iko katika hali ya dharura na wakati umefika kwa Rais kuitangaza hivyo lakini akitanza hivyo analazimika kutumia madaraka yake ya kisheria ambayo yanamuangukia.

  Hatua za Muda mrefu
  Sasa tukishashughulikia hatua hizi za muda mfupi tunajikuta tunabakiwa na jukumu moja tu kubwa nalo ni kushughulikia tatizo la muda mrefu. Mapendekezo yangu ni kutupilia mbali kwa wakati huu miradi midogo midogo ya nishati. Hii miradi ya 100MW au 50MW ni kupoteza muda wa taifa hasa wakati huu. Miradi ya namna hiyo inatakiwa ije baadaye sana kama kuongezea mahitaji ya taifa na tunaweza kufanya wakati mzuri ziadi.

  Sasa hivi tunahitaji kutenga fedha za kutosha kuanza mradi wa ujenzi wa Stielger’s Gorge ambao sehemu yake ya kwanza inaweza kumalizika ikiwa na uwezo wa 500MW hivi. Ni kwa sababu hiyo wabunge wanaolalamikia nishati waamue baada ya kumtaka Rais afanye hayo ya hapo juu wao wenyewe watenge kuanzia kwenye bajeti hii fedha kwa ajili ya kuanza kwa mradi huu kwani hatua zote za awali zimeshafanyika.
  [​IMG]
  picha toka VijanaFM

  Kama kweli wabunge wa CCM wanauchungu na kwamba kweli wanataka hatimaye kujiokoa basi waamue - kwani wao ndio watunga sheria na ndio wanapanga fedha - kupeleka fedha zaidi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa mradi huu. Tukumbuka kuwa miaka mitano iliyopita ni Rais Kikwete aliyeahidi kwenye Bunge hilo hilo kuanza kwa mradi huu mkubwa ambao ungeweza kuzalisha zaidi MW 2000 za umeme na ukiongeza na vyanzo vilivyopo kuweza kujikuta tunazalisha umeme zaidi. Jukumu litakalobakia liwe la kusambaza zaidi na kuboresha zaidi mitambo na njia za umeme.

  Wabunge badala ya kukubaliana kumlaumu Ngeleja, wakubaliane kumpa Ngeleja mzigo wa kuanza ujenzi wa Stielger’ Gorge kwa kushirikiana na RUBADA. Mradi huu umechelewa kwa miaka thelathini na wakati umefika kwa wabunge kuamua. Binafsi nashangaa kwanini wabunge wa upinzani hawasukumizi kuanza kwa mradi huo sasa hivi na nina uhakika wana CCM watawaunga mkono vile vile kwani vyama vyote vilikuwa na ajenda hiyo.

  Mwisho

  Ndugu zangu, nilichokisema ni kwamba tatizo la nishati nchini linatatulika na utatuzi wake hauitaji malaika kutoka mbinguni. Linaweza kutatuliwa kwa kuwepo kwa utashi wa kisiasa, uthubutu wa wabunge na ushiriki wa moja kwa moja wa Rais Kikwete. Badala ya kumsulubu Ngeleja na kumbana wabunge waamue kufanya kilicho ndani ya uwezo wao - wamtake Rais afanye sehemu yake (kwenye utatuzi wa muda mfupi) na wao wafanye kilicho sehemu yao.

  Ni matumaini yangu kuwa Ngeleja atakapozungumza kujibu hoja mbalimbali za Wabunge atawaambia jambo hili kama kweli wanataka wanachokitaka waidhinishe fedha za kutosha ili mradi wa Stielger’s Gorge uanze. Na katika kukubali huko wawe tayari kupunguza gharama nyingine za msingi ikiwemo posho, matumizi mengine ya anasa. Hapa ndio tutajua ni kina nani kweli wanataka tatizo la nishati liishe au liendelee. Wawe tayari kukatwa mishahara, posho na matumizi mengine ya anasa au yasiyo ya lazima ili Taifa liunganike pamoja kutatuta tatizo hili. Siyo wao peke yao bali na wananchi wote wawe tayari kukubali kutoa sadaka hiyo. Lakini, mfano lazima uanzie Bungeni!

  Haitoshi kuzungumza kwa jazba!

  Twende tupige hatua kubwa mbele - lets make the great step forward!

  We too Can! - Nasi Tunaweza Pia!

  Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
   

  Attached Files:

 2. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  I hate emergency power back up. Jamani serikali yangu tukubali infinite solution ya tatizo ni dedicated long run investment kwenye umeme mengine ni porojo tu .. Na hii inawezekana per phase mpaka tutatua hili tatizo.... Hii emergency power inaonekana ni njia nzuri ya mianya ya rushwa ndio maana wanaipenda sana ...
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tateeee naneeeee
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mkuu nakubaliana nawe kuwa SERA ZA NISHATI NA MADINI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI NA UTEKELEZAJI WAKE NI TATIZO,lakini ukiniuliza mimi bado WAZIRI HUYU HUSIKA ANADHAMANA NA WAJIBU WA KUJIBU MAPUNGUFU YA WIZARA YAKE HUSIKA.

  NAFIKILI UMEFIKA WAKATI SASA WIZARA NYETI ZOTE ZIPEWE WAZIRI MWELEVU NA MBUNIFU [INTELLECTUAL AND CREATIVE MINISTER].Tunajua Wizara ya UJENZI TANZANIA,Miaka ya Nyuma ilikuwa ni Wizara ovyo sana,wala hata umuhimu wake ulikuwa si chochote.

  Lakini alipokuja Mzee Mkapa na kumpa Waziri Mwelevu na Mbunifu JOHN POMBE MAGUFULI, ubunifu wake waziri huyu NDIO MOJA YA MAFANIKI MAKUBWA YA AWAMU YA TATU YA BENJAMIN WILLIAM MKAPA.

  Ilipokuja awamu ya NNE ya Mzee KIKWETE,akalishwa sumu na wapambe waliokuwa PEMBENI YAKE,Mzee Magufuli akawekwa pembeni toka wizara ya ujenzi au miundo mbinu.Tukategemea kupitia Waziri Mpya basi wizara hiyo iliyokuwaa bora kwa utendaji ikiwa na Mh Magufuri itaendeleza sifa yake.Ukweli mambo yalijionyesha Wizara ilipoteza sifa yake ya utendaji wenye tija na kuwa wizara ya mbinu za KUFISADI UMMA. Mungu si haba akamkumbusha Rais ukichelea mwana kulia utalia wewe chukua kifaa kikusaidie kwenye maendeleo ya Nchi yako, akamludia Mh Magufuli mwendo mdundo kama kawaida yake Maendeleo yakajionyesha wazi na kila mtu anajua bidii na ubunifu wa Wizara husika chini ya Mh Magufuli.

  IWEJE HILO LIWEZEKANE KWA WIZARA YA UJENZI CHINI WAZIRI HUSIKA,HUKU WIZARA YA NISHATI NA MADINI ISHINDWE CHIN1 YA WAZIRI HUSIKA.

  HOJA YANGU KUWA NGEREJA ANASTAHIKI,ADHABU HII AMEKOSA WEREVU NA UBUNIFU WA KUMUDU WIZARA HIYO KAMA ALIVYOMUDU MHESHIMIWA MAGUFULI.


   
 5. MANI

  MANI Platinum Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  MM heshima kwako ! Ni kweli panahitajika hatua za dharura lakini kutokana na experience tulioiona toka hapo nyuma hii miradi ya dharura inaharibiwa kwa maslahi binafsi naungana na Mganga Mkweli twende moja kwa moja hatua ya pili, mradi wa STIEGLER'S.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hilo linaturudisha kwa Kikwete.
   
 7. g

  guta Senior Member

  #7
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Pamoja na kwamba tatizo tunafahamu sio Ngeleja, lakini pia na yeye anahusika kwa hilo. maana yeye ni mshauri wa rais kwenye wizara yake. hapo ameshindwa kumshauri raisi nini cha kufanya, anapiga blaablaa tu. nadhani kama wewe mwanakijiji ungekuwa wizara hiyo ungemshauri rais afanye kama ulivyotoa mapendekezo. bado ngeleja anawajibika katika hili. ameshindwa kuonyesha njia. kama alivyosma lipumba, Makamba ametoa mapendekezo bora zaidi ya waziri husika.
   
 8. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mzee Mwanakijiji mawazo yako ni mazuri as always, na umemalizia katika Utetezi wako kwa Ngeleja hapo juu kwa maneno haya; Haitoshi kuzungumza kwa Jazba.
  Mzee Mwanakijiji huwezi kuwazuia Watanzania kuzungumza kwa Jazba, Watanzania wamechoka kusikia hadithi hizi za Viongozi na nyie mnaojua kuandika kila siku, Watanzania wanataka UMEME. Hio Mipango yote ulioiainisha hapo Juu ni vitu ambavyo vipo siku nyingi, tunavisoma kila siku na tunavisika kila siku ktk TV Set zetu. Watanzania sasa wamechoka kusikia hizi hadithi, wanataka Umeme ili waendeleze Ujasiriamali wao, wasomeshe watoto wao, wanataka Umeme ili wazalishe Viwandani na walipe kodi Serikalini na wajihahakishie uhai wa Ajira zao, Wanataka Umeme ili kazi zao maofisini zifanyike wapate chakula chao cha kila siku.
  Ni JAZBA pekee ndio itakayowatoa Watanzania hapa tulipo, Ni JAZBA itakayowaamsha Viongozi na Serikali legelege, Ni JAZBA itakayo leta UMEME katika Nchi hii.
  Kupanga ni Kuchagua, Watanzania wamechagua kutumia JAZBA ili kuiamsha Serikali legelege

   
 9. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Lakini Mkuu kama Bosi wake AWEZI KUMUWAJIBISHA NASI TUNAONA KUWA ANATUZAMISHA SISI KWENYE JANGA.Tunafanya nini sasa kujikwamuana huyu JAMAA asiye creative na hana uwezo wa kujitambua kuwa ameshikilia wizara muhimu kwa umma.

  Hivyo kupitia ushawishi wetu kwa BUNGE na dua zetu kuwa huyu jamaa APIGWE CHINI KUPITIA BAJETI HII.
   
 10. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Kila kitu kwenye Nchi hii kinaitwa dharura. Dawa ni kuwaondoa kwa Revolution
   
 11. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,147
  Likes Received: 3,335
  Trophy Points: 280
  Uongozi mbovu na mikataba mibovu ndo imetufikisha hapa tulipo..viongozi wako ki self-interest zaidi.
   
 12. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji umenikumbusha mahojiano yako na Ngereja mara ya mwisho alikuomba sana kuwatetea akiamini unaweza, nimeamini kweli unaweza!

  Lakini sijaona katika maelezo yako yote hata aya moja inayomtetea Ngereja? Badala yake umemuingiza kwenye moto zaidi, nadhani bado ana maswali ya kujibu kabla ya kuwajibishwa; Lakini la kumuondoa ni muhimu na haliepukiki sijui kwanini hukuliweka katika hitimisho lako?!

  Nakubaliana na maono yako na ushauri wako juu ya nini kifanyike kukabiliana na tatizo la Umeme, lakini nabaki na swali moja Ngeleja amefanyanini tokea aingie ndani ya Wizara hiyo mpaka tusimwajibishe? Umenishangaza wewe mtu wa pembeni kuwa na mawazo hayo mazuri ambayo yanaweza kuwekwa mezani na kuboreshwa! Yeye mbona hana mawazo yoyote? Kwanini wewe unayefikia strategy mbadala ndiye husiwe Waziri wa Nishati nawe Ngereja ambaye amelala tu?

  Yes tatizo halikuanza leo lakini jibu lazima lianze leo; Ngereja awajibishwa na aondoke kwasababu hana uwezo wala akili ya kuanzisha majibu ya kukabiliana na ukubwa wa tatizo;ameshindwa kuleta majibu hilo ndilo kosa lake, siyo kuwa tunataka awajibishwe kwasababu kuna tatizo! au husidhani kuwa tunafikiria kuwa yeye ndio kaleta tatizo! la asha! yeye kashindwa kutatua tatizo!

  Nadhani kaingia hapo kama matunda ya Richmonds na Dowans sasa aondoke tu maana hata waliomuweka hapo walishaondoka siku nyingi ndani ya Serikali, hawezi ku-sychronise na mbinu za kutatuwa tatizo la Umeme kwasababu nadhani yeye aliwekwa hapo kuliongeza zaidi ili Kampuni yao ya Richmond na Dowans ipate kazi zaidi.
   
 13. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2011
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Umenena vyema mwanakijiji. "poor planning" ndio iliyotufikisha hapa
   
 14. t

  threadcritic Member

  #14
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Leo hii ni siku ya 3 hatuna umeme hapa kwetu.

  Nishachoka. Kama huo umeme unaletwa na Rostam au sijui Symbion..mimi I care less. Nataka umeme that's it


  mengine mtajuana wenyewe na nakala zenu ndefu
   
 15. t

  threadcritic Member

  #15
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Juzi Rev Kishoka kaandika thread humu na usomi wake wote yule bwana hesabu zake eti kwa miaka kumi ijayo walau tuwe na 1200 megawatts

  Nikaona huyu jamaa anawazimu au ndio upeo wa kufkiria umefika kikomo?

  I mean in 10 yrs time tutakuwa na watu milioni 48 , huku tunataka na viwanda vifunguliwe hivyo matumizi yatakuwa na makubwa mno

  Vyanzo vya umeme kama Jua , Upepo na maji tunayo...why not kupiga hesabu za 40,000 megawatts ?
   
 16. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu hapo kwenye red bold. MKJJ anamaanisha Rais atangaze "Hali ya Hatari" Ili apate madaraka ya kutatua hili tatizo yeye kama yeye; maana akitanga hilo, any other laws seizures!!
   
 17. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu Results... RESULTS.., thats all that matters....
  na ukweli ni kwamba it is undisputed kwamba now tuna mgao wa GIZA..(under Ngeleja), therefore tunaangalia the man in power, the one responsible for Wizara..., and that man should be responsible..., mambo ya matatizo yameanzia wapi we can look at it when the man in power has stepped down...

  Mkuu always Kiongozi has to take responsibilities either it credits he does not deserve or lawama which he is not directly responsible.....

  Tunachokiona ni This Janga la Taifa has occurred under whose leadership
   
 18. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #18
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  It will take ages for a nigga to make it broda.
   
 19. t

  threadcritic Member

  #19
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi hizi makala siwezi kuzisoma zote kwani nina mambo mengi ya kusoma humu na umeme wenyewe utakatika at any time.

  Dawa hapa ni kupetition these bastards in the cabinet to resign.


  Mwanakijiji tushachoka na makala tunataka umeme...je unayo any radical idea ya kupata huu umeme?
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Jul 18, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Watu tuna kumbukumbu fupi sana na ukweli huu umejidhihirisha hivi sasa kwenye haya matatizo ya umeme. Waziri Ngeleja anaoneka ndiye kama vile amesababisha matatizo yote haya wakati ukweli wa mambo umeme wa uhakika umekuwa tatizo sugu Tanzania.

  Sasa iweje Ngeleja leo abebeshwe msalaba wa lawama na shutuma wakati mawaziri wa nishati na serikali zilizopita zimemrithisha tatizo? Hiyo si haki hata kidogo. Jaribuni tu kurudi nyuma miaka 20 iliyopita muone ni kina nani waliweza kupata fursa ya kuongoza wizara hiyo na walifanya nini kuhakikisha tatizo linakuwa historia.

  I cut him some slack!!
   
Loading...