Utetezi wangu wa wazi wa William Ngeleja - The use of Emergency Powers Act 1986

Kama umepata kazi ya upishi, inapita miezi na hata miaka kadhaa hujapika chakula chochote na bado unapata mshahara, inabidi ujiulize kama bado unastahili hiyo nafasi. Ngereja anastahili kuwajibika yeye mwenyewe kwa kushindwa kufikia matazamio ya nafasi aliyopewa.

hili halina shaka lakini Ngeleja anacho kile tu ambaco amepewa. Kumuwekea mtu malengo ya kufikia kitu fulani halafu humpi nyenzo za kufikia malengo hayo kunawanyima waliompa malengo hayo kumdai kwanini hajayatimiza. Lakini vile vile wale wanaoweka malengo wanamuwekea malengo ya namna gani? Huwezi kumwambia Ngeleja atatue tatizo la umeme wakati uhuru wa kufanya hivyo unaamuliwa na Baraza la Mawaziri.
 
Kutangaza hali ya hatari ni prerogative ya Rais. Halazimishwi na yeyote, na hashauriwi na yeyote. Bunge kama wawakilishi wa watu wanaweza kutoa tamko la kumtaka Rais kufanya hivyo. Rais akitangaza hali ya hatari anaweza hata kumteua Waziri wa Nishati wakati wa Dharura na kumwacha Ngeleja ashughulikie mambo mengine.

Whatever the case, Raisi wa Tanzania hafanyi kazi kwa kuibuka tu from nowhere!, ni lazima anafikia maamuzi kwa kuchanganya ufahamu wake na ushauri anaoupata kutoka kwa wasaidizi kama mawaziri wake ambao tuseme ni washauri wake kwa namna moja au nyingine, japo at the end the buck stops with him!
Hivyo ninategemea Ngeleja awe ameshaliona hilo la kutangaza hali ya hatari kama njia ya kutatua tatizo na kwamba atakuwa ameshamshauri raisi kufanya hivyo, na iwapo amemshauri hivyo lakini JK akagoma(maana raisi hafungwi na ushauri) basi Ngeleja hana budi aachie ngazi.
Lakini pia at the same time kama hajampa ushauri huo raisi basi pia ni wa kuwajibika kwa kujiuzulu kwa kushindwa kuona solution ya tatizo.
Sitegemei Kikwete atangaze hali ya Hatari bila kupewa information nzima ya hali ya umeme nchini, pamoja na option kadha wa kadha za kusolve hilo tatizo kutoka kwa waziri mwenye dhamana husika, ambaye this time ni Ngeleja.

Bunge linaweza kumtaka raisi atangaze hali ya hatari, lakini mpaka lifike huko ni lazima lijiridhishe kwamba option zote zimekuwa exhausted na imeshindikana, Kwa Wakati huu inaonekana Tatizo ni Uongozi mbovu wa Ngeleja, inabidi kwanza aondoke
 
Gamba la Nyoka... unafikiri Rais anajua uzito wa tatizo la upungufu wa nishati au anahitaji kupewa ushauri na watu wengine juu ya uzito huo?
 
Bw Mwanakijiji,

Japo ninaamini ni mfuatiliaji mzuri wa masuala yanayohusu hii nchi kuna kitu kimoja nataka kukufahamisha, japokuwa huyu Ngeleja amekuta hayo matatizo wizara ya Madini na nishati ukijumuisha na Tanesco; huyu bwana hawezi kukwepa fagio la chuma! sababu kubwa ni ameshindwa kuja na jawabu la kuondoa hali hiyo na zaidi ya hilo matatizo tuliyo nayo sasa yamesababishwa (kwa kiasi kikubwa) na uzembe (negligence) yaani kuna mitambo miwili imekosa mafuta mmoja wa IPTL na mwingine ni Symbion (tunavyoongea sasa)!

Sasa hata kama hatuna vyanzo toshelezi kukidhi haja, je hata kuagiza mafuta (heavy fuel) nalo ni tatizo? hebu tuwe wakweli hizi siasa hazitupeleki popote kama watu hawatekelezi majukumu yao! Kenya pia huwa ina matatizo ya umeme kama sisi lakini wao angalau wana watu wanaoelewa umuhimu wa nishati kwa uchumi wa nchi yao na kila mara tatizo hili linapotokea huletwa meli zilizofungashwa jenerata toka Italy kuja kuuza umeme tokea Bandari ya Mombasa (hizi meli huwa zinakuwapo baharini kwa ajili ya tenda kama hizi)! Je sisi tunashindwa nini kufanya hivyo kama hata kununua mafuta ni shida (yapaswa watu fulani wapewe tenda hizo sio?)? Huu ukiritimba utaisha lini? Mie nashauri Ngeleja, Malima, Jairo, Tanesco board plus the whole planning and technical team waondoke! maana wamekosa maarifa na uzalendo wa kuiliokoa Taifa letu toka janga la kiuchumi ambalo madhara yake tunayaona na si rahisi kufutika! we fikiria kwa kipindi kisichozidi miezi mitano mfumuko wa bei umepanda toka 5% mpaka 10.9%! Tuache utani jamani Ngeleja na wahuni wenzake wanapaswa kuondoka!
 
Watu tuna kumbukumbu fupi sana na ukweli huu umejidhihirisha hivi sasa kwenye haya matatizo ya umeme. Waziri Ngeleja anaoneka ndiye kama vile amesababisha matatizo yote haya wakati ukweli wa mambo umeme wa uhakika umekuwa tatizo sugu Tanzania.

Sasa iweje Ngeleja leo abebeshwe msalaba wa lawama na shutuma wakati mawaziri wa nishati na serikali zilizopita zimemrithisha tatizo? Hiyo si haki hata kidogo. Jaribuni tu kurudi nyuma miaka 20 iliyopita muone ni kina nani waliweza kupata fursa ya kuongoza wizara hiyo na walifanya nini kuhakikisha tatizo linakuwa historia.

I cut him some slack!!

Hapa kwenye red ndipo watu wanataka jamaa awajibike, kama mtu amerithishwa tatizo inamaana kuwa walimwamini kuwa atalitafutia ufumbuzi, sasa kukaa kwake kimya kunaonesha dhahiri kuwa hili tatizo limemshinda na anahitajika mtu mwingine tumkabidhi tuone atatufikisha wapi. Kama kamba ni ngumu ni heri ukampisha na mwingine naye aone ugumu wake na si kung'ang'ana nayo huku unalalamika wenzio watajuaje kuwa kweli ni ngumu na ndo maana watu wanamuona huyu jamaa kuwa ni kituko tu.
 
Bw Mwanakijiji,

Japo ninaamini ni mfuatiliaji mzuri wa masuala yanayohusu hii nchi kuna kitu kimoja nataka kukufahamisha, japokuwa huyu Ngeleja amekuta hayo matatizo wizara ya Madini na nishati ukijumuisha na Tanesco; huyu bwana hawezi kukwepa fagio la chuma! sababu kubwa ni ameshindwa kuja na jawabu la kuondoa hali hiyo na zaidi ya hilo matatizo tuliyo nayo sasa yamesababishwa (kwa kiasi kikubwa) na uzembe (negligence) yaani kuna mitambo miwili imekosa mafuta mmoja wa IPTL na mwingine ni Symbion (tunavyoongea sasa)!

Nani anayetengeneza sera ya Nishati nchini? Kuna ubaya gani kwa Rais kutangaza hali ya dharura hata kesho na kutumia madarka aliyonayo kutatua tatizo la umeme?
 
Okay hata tukikubaliana kwamba wizara ni kubwa, wizara ni ngumu, matatizo mengi ameyakuta sawa, basi naomba mwanajamii yoyote aniambie hivi ni jambo gani zuri moja tu ambalo tunaweza kusema limeletwa au limefanyika katika kipindi cha madaraka ya huyu mweshimiwa..

Alafu nadhani ni Tanzania pekee ambapo deputy anaweza akapatwa na kashfa ya kutaka kuwaonga MPS ili bajeti ipite alafu Waziri mwenyewe asipoteke kazi yake (yaani kwa hii kashfa ingebidi huyu muheshimiwa apigwe marufuku kusogelea shughuli zozote za umma..)
 
Gamba la Nyoka... unafikiri Rais anajua uzito wa tatizo la upungufu wa nishati au anahitaji kupewa ushauri na watu wengine juu ya uzito huo?

Raisi pamoja na ufahamu wake anafanya kazi na watu, "correct information" zitakazo mfanya afikie uamuzi hazipati kwa mganga wa kienyeji, bali anzipata kutoka kwa timu yake aliyoiteua imsaidie kazi wakiwemo mawaziri.
Mathalani, Raisi anaweza akawa anfikiri option X kwa ajili ya tatizo Y, lakini wataalamu na washauri wake wakampa ushauri kwamba option X inaweza kuleta matatizo mengine huko mbeleni au isiwe effective n.k na hivyo basi wakapendekeza solution Z, lakini iwapo washauri na wataalamu hawatampa raisi option yoyote ya kutatua tatizo na raisi akaendelea kutumia option X basi mambo yakija kuharibika huko mbeleni Washauri watakuwa hawakutimiza wajibu wao ipasavyo wa kumshauri presidaa na hivyo wanapaswa kuwajibika. au kama washauri wamempa raisi ushauri Z na mambo bado yakaharibika basi Washauri hawana budi kuwajibika.

Ninachotaka kusema ni hiki, Raisi anaweza kuwa anajua kabisa uzito wa Tatizo, lakini akawa hana majibu yote ya hayo matatizo, hapo ndipo atakapotegema Wasaidizi wake waje na majibu ya hayo matatizo, sasa unaweza kuniuliza salama ya Wasaidizi ni nini basi?, Salama ya Wasaidizi iwapo wanampa raisi option za kufuata kuondoa tatizo lakini Raisi hazifuati ni kwa Wao kujiuzulu tu. Mtei alijiudhuru alipompa Mwalimu ushauri ule maarufu lakini mwalimu hakuufuata.

Na pia hatutegemei Mshauri akawa anampa raisi ushauri halafu anageuka geuka, mara aukane ushauri huo, mara amshauri tena raisi ushauri wa namna hiyo hiyo then baadae aukane tena, ikitokea hali ya namna hii basi ni jukumu la raisi kumfuta kazi mshauri huyo na kutafuta mwingine.

So far Ngeleja hana jibu lolote la Tatizo la Umeme nchini, Siwezi kumhukumu Raisi kwanza kabla ya Waziri mwenye dhamana kwa maana tukifanya hivyo, udhaifu wa Waziri mmoja mmoja utakuwa associated na Raisi kwa kusema eti "kwani raisi hajaliona mbona hajafanya chochote?", kila waziri ni lazima awajibike kwa wizara anayoiongoza!.
Na kwa kweli iwapo tatizo lingekuwa ni Raisi na si ngeleja, tayari tungeshaona Ngeleja ameshajiuzulu toka zamani!, mtu makini utafanyaje kazi na mtu ambaye unadhani ni kikwazo?. kama Ngeleja anadhani ameshafanya homework yake vizuri lakini kikwazo ni raisi, anasubiri nini kujiuzulu? kwa maana hata akikaa hapo wizarani hawezi kufanya chochote kwa kuwa raisi hamsikilizi, si ndivyo ingetakiwa kuwa?

Ngeleja should Go
 
Nani anayetengeneza sera ya Nishati nchini? Kuna ubaya gani kwa Rais kutangaza hali ya dharura hata kesho na kutumia madarka aliyonayo kutatua tatizo la umeme?
Unajua tukianza kukimbilia collective responsibilities tutaanza kuondoa dhana nzima ya uwajibikaji tusisahau wizara ni organ yenye sub-organs (departments et al) zenye systematical hirearchical divisions of responsibilities zenye specific individuals that oversee the organ smooth functioning! Sasa unapoanza mambo ya sera ina maana unaanza kuongelea the whole system that is party+government (chama Magamba (NEC) + serikali (including the whole ministries) + bunge)! Sasa nikuulize kwanini Magufuli under his ministry of Works awe accountable na kukosekana umeme? Tuache cheap politics na ku-victimize kila mtu kwa uzembe wa watu waliokuwa costitutional bestowed power ila waka-misuse!

Therefore katika hili hamna cha sera wala collective uwajibikaji! Procurement procedures zipo na zinaeleweka! unatangaza tender na kampuni zina-bid tender inachukuliwa na mafuta yanaletwa! Tatizo au ugonjwa uliopo kwa Ngeleja na co. ni aidha hawajui chakufanya au wana maslahi yao katika ku-secure a procurement company to supply the heavy fuel! ndo mambo ya 30% ile wizara imeoza maana ukame upo kila mwaka na hata vipindi hujulikana sasa nashangaa kama kitu rahisi kama kununua mafuta kinawashinda! Je wataweza nini katika wizara muhimu kama ile? Basi waende kulala ile wizara si ya baba yao! tumeshapoteza over a bio. US$ so far kutokana na mgawo ukiachilia mbali vijana wengi waliopumzishwa majumbani bila malipo kutokana na viwanda kusimamisha uzalishaji kwa kukosa umeme! Cha ajabu soma the East African uangalie mradi mpya wa machimbo ya Uranium in Selous unaoshughulikiwa kwa sasa! utachoka mwenyewe.. yaani hii nchi itapata US$ 5 mio. kati ya US$ 250 mio. zitakazopatikana kila mwaka kwa mwekezaji! mzee, suala la ubadhirifu wa Ngeleja halikwepeki! Huyo jamaa ni mwizi kuanzia yeye, Malima, Jairo na bodi nzima! woote waende nyumbani kulala! Alaah!
 
Hii hali tuliyokuwa nayo hivi sasa laiti Wizara ingetangaza Tenda Mapema wala tusingefikia hatua ya leo kumtaka "Raisi atangaze hali ya Hatari", Majira ya ukame nchini yanajulikana, Mabwawa yetu yana Tope inajulikana, Tuna mgawo toka mwaka 2005 inajulikana,tuna upungufu wa megawatt inajulikan, sasa unajiuliza ni kitu gani cha ajabu "Kutangaza hali ya hatari" itakifanya kile kilichoshindwa kufanyika kwa kufuta kanuni na sheria zetu za procurement toka mwaka ule wa 2005 mgawo ulipoanza!.
Hapa hauhitaji kuwa mtaalamu wa Nyuklia kuona Wizara inaoyoongozwa na Ngeleja ni Incompent!!!
 
MEN LIE , WOMEN LIE...NUMBERS DONT LIE


MALAYSIA:

POPULATION: 28 million
ELECTRICITY CAPACITY (AVAILABLE) : 21,000 MEGAWATTS



TANZANIA:

POPULATION: 45 million

ELECTRICITY CAPACITY:(AVAILABLE)
630 MEGAWATTS
 
Nani anayetengeneza sera ya Nishati nchini? Kuna ubaya gani kwa Rais kutangaza hali ya dharura hata kesho na kutumia madarka aliyonayo kutatua tatizo la umeme?
Sera ya nishati 1992,ililetwa chini ya Jakaya Mrisho Kikwete,ikafanyiwa marekebisho chini ya Yona nadhani.Juzijuzi nilisikia kwamba wawekezaji hawaifagilii tanzania kwenye nishati kwa sababu ya masharti magumu,wengine wakasema bei ya umeme hairidhishi.
Kwa hiyo,serikali inabidi irudie uwekezaji kwenye umeme,kwa kuwa hawa wawekezaji(siwalaumu) hawawezi kutupeleka popote zaidi ya motoni.Kiwira ifufuliwe chini ya STAMICO,tutumie rasilimali yetu ya makaa ya mawe Ngaka na kiwira,we will be alright.....mafuta yanaboa sana,ila inaonyesha Ngeleja hasikii hilo,kwa kuwa ana mkono fulani nadhani kwenye biashara ya mafuta.
Thats why he gots to go...lets not be against it just because CCM MPs wants him to go.
 
Mwanakijiji unaongea kana kwamba Rais wa Tanzania (kama taasisi) ni mnyonge asiyeweza kuagiza umeme wa upepo utengenezwe kula Singida na pale kwetu Makambako; wa maji utengenezwe kule kwetu milimani Upare na hapo kwenye Stiegler's Gorge. Au anaogopa Wanaharakati wa Mazingira waliombana kwenye suala la barabaraba ya Serengeti? Hivi kweli kabisa Sheria zetu za kusimika madaraka katika Dola ndio chanzo cha kuwa na taasisi dhaifu ya Urais hivyo kupelekea hitaji la kutangaza hali ya hatari? Basi na atangaze na hali ya dharura kuhusu njaa. Na kuhusu elimu. Pia na kuhusu vifo vya wajawazito mahospitalini. Kwa ujumla atangaze Marshal Law kisha nchi iendeshwe ki-benovelent dictatorship; kulala saa 4 usiku hakuna kutembea giza likishaingia, amri (decree) ndio ziwe sheria za nchi, mijadala ya kidemokrasia ikome mara moja, lengo liwe moja tu: kuitumikia dola tuendelee!
 
Mwanakijiji unaongea kana kwamba Rais wa Tanzania (kama taasisi) ni mnyonge asiyeweza kuagiza umeme wa upepo utengenezwe kula Singida na pale kwetu Makambako; wa maji utengenezwe kule kwetu milimani Upare na hapo kwenye Stiegler's Gorge. Au anaogopa Wanaharakati wa Mazingira waliombana kwenye suala la barabaraba ya Serengeti? Hivi kweli kabisa Sheria zetu za kusimika madaraka katika Dola ndio chanzo cha kuwa na taasisi dhaifu ya Urais hivyo kupelekea hitaji la kutangaza hali ya hatari? Basi na atangaze na hali ya dharura kuhusu njaa. Na kuhusu elimu. Pia na kuhusu vifo vya wajawazito mahospitalini. Kwa ujumla atangaze Marshal Law kisha atangaze Marshal Law kisha nchi iendeshwe ki-benovelent dictatorship; kulala saa 4 usiku hakuna kutembea giza likishaingia, amri (decree) ndio ziwe sheria za nchi, mijadala ya kidemokrasia ikome mara moja, lengo liwe moja tu: kuitumikia dola tuendelee!

Una ushahidi gani kuwa Rais wa Tanzania, kwa madaraka aliyonayo leo hii angeweza "kuagiza umeme wa upepo utengenezwe kula Singida na pale kwetu Makambako; wa maji utengenezwe kule kwetu milimani Upare na hapo kwenye Stiegler's Gorge."? Je, hii sii ni tayari sawa na mfano wa "nchi iendeshwe ki-benovelent dictatorship"? Kwa hiyo kutakuwa na haja gani basi ya Rais kuchukua extra measures za kutangaza "Marshall law" wakati tayari kikatiba yuko empowered with requisite Dictatorial powers?
 
Hivi kama nchi ikiingia Vitani mngetaka Rais aoneshe uongozi kwa kuchukua madaraka aliyonayo kisheria. Ninavyowasikiliza ni kana kwamba Idi Amin alipovamia Kagera Nyerere alitakiwa aende kukutana naye kumbeleza aondoe majeshi yake au aamue kumwachilia tu. Sijui kama Kikwete angekuwa Rais wakati ule tungefanya nini.

Ndio maana naamini aidha hii hali ya dharura siyo mbaya jinsi ambavyo tunaaminishwa na yawezekana haina athari kubwa kwa uchumi wetu na maisha yetu kulinganisha na Vita ya Uganda. Maana ya Vita ya Uganda iligusa sehemu ndogo ya nchi, lakini nchi nzima ikawa mobilized. Tatizo la Nishati nadhani linawagusa watu wachache zaidi na halina athari kama kuvamiwa ardhi yetu. Ndio maana watu wanataka kukaa kamati, mijadala, mazungumzo ya siku 21! gademu!!!

Ndio maana wengine tunasema Uongozi ni uwezo! Si ujana, si elimu, na si sura!
 
Una ushahidi gani kuwa Rais wa Tanzania, kwa madaraka aliyonayo leo hii angeweza "kuagiza umeme wa upepo utengenezwe kula Singida na pale kwetu Makambako; wa maji utengenezwe kule kwetu milimani Upare na hapo kwenye Stiegler's Gorge."? Je, hii sii ni tayari sawa na mfano wa "nchi iendeshwe ki-benovelent dictatorship"? Kwa hiyo kutakuwa na haja gani basi ya Rais kuchukua extra measures za kutangaza "Marshall law" wakati tayari kikatiba yuko empowered with requisite Dictatorial powers?


Kwani anatumia madaraka gani anapoenda kuwaalika wawekezaji huko Sauzi na kwingineko?
 
Kwani anatumia madaraka gani anapoenda kuwaalika wawekezaji huko Sauzi na kwingineko?

Kulingana na hoja zako za awali, hilo swali lako siyo la msingi hata kidogo. Unachotakiwa ni kutoa ushahidi kadiri uwezavyo kutetea kauli na madai yako kama ulivyoainisha hapo juu.
 
Hivi kama nchi ikiingia Vitani mngetaka Rais aoneshe uongozi kwa kuchukua madaraka aliyonayo kisheria. Ninavyowasikiliza ni kana kwamba Idi Amin alipovamia Kagera Nyerere alitakiwa aende kukutana naye kumbeleza aondoe majeshi yake au aamue kumwachilia tu. Sijui kama Kikwete angekuwa Rais wakati ule tungefanya nini.

Ndio maana naamini aidha hii hali ya dharura siyo mbaya jinsi ambavyo tunaaminishwa na yawezekana haina athari kubwa kwa uchumi wetu na maisha yetu kulinganisha na Vita ya Uganda. Maana ya Vita ya Uganda iligusa sehemu ndogo ya nchi, lakini nchi nzima ikawa mobilized. Tatizo la Nishati nadhani linawagusa watu wachache zaidi na halina athari kama kuvamiwa ardhi yetu. Ndio maana watu wanataka kukaa kamati, mijadala, mazungumzo ya siku 21! gademu!!!

Ndio maana wengine tunasema Uongozi ni uwezo! Si ujana, si elimu, na si sura!

Dharura inapimwaje - kwa muda au ukubwa? Kama ni muda kila mwaka kuna mizunguko (cycles) za mgawo, mwanzo na mwisho wa mwaka!Re:

It has become so predictable. This thing we call ‘power rationing.' We had it in 2006, 2007 and 2008. It is here in 2009. If the yearly trend continues then we shall surely experience it in 2010.

If we have forgotten the past then we only have to glance at the dates of the following front page news stories from The Citizen to get a glimpse of how this power rationing is such a vicious cycle: "‘Tanzania 2006: Power' Crisis dominated headlines" (29 December 2006); "Another power crisis as Songas turbines collapse" (25 September 2008); "Power Crisis: Tough times ahead – No solution in sight as sabotage suggestions angers Tanesco boss" (13 October 2009).

For some strange reasons the major power crises tend to emerge toward the end of the year. Some claim it is because of delayed rains. The moment you blame it on ‘Mother Nature' you let humans off the hook. But isn't being human all about taming nature? And, as experts of climate change insists, aren't we the ones who affect those rain seasons with environmental degradation.

From what has been going on there is no way we can claim human agency is not behind this power tragedy. When we survey more cover stories from The Citizen this is what we get as evidence of why this is a man-made problem that needs humans to take responsibility: "Business want power shedding compensation" (19 March 2007); "Tanesco ordered to pay Sh190.8m to paper mill" (12 September 2007); "Emergency power supply contract that never was" (19 March 2008"; "Rationing ends as power supply normalises" (The Citizen 20 September 2008).

Chanzo: UDADISI: Rethinking in Action: Waiting for Power: Citizens' Plight during Energy Crises - As it was in 2008 and 2009 so it is in 2010!
 
Kulingana na hoja zako za awali, hilo swali lako siyo la msingi hata kidogo. Unachotakiwa ni kutoa ushahidi kadiri uwezavyo kutetea kauli na madai yako kama ulivyoakinisha hapo juu.

Nahisi hujasoma muktadha wa hizo hoja, suala la sheria ya hatari ni hoja ya Mwanakijiji ambayo napingana nayo - Rais uwezo na nguvu za kutatua tatizo la mgawo wa umeme anao, labda nia ndio hana. Mbona katika kipindi cha Urais wake walifanya maamuzi magumu ya kuleta umeme wa dharura japo kuna sheria ya manunuzi? Mbona katika kipindi chake walitaka kufanya maamuzi magumu ya kujenga barabara ya Serengeti japo kuna sheria za mazingira? Na mbona katika kipindi cha Urais wake walifanya maamuzi magumu ya kwenda bandarini kuagiza wamalize tatizo la msongamano wa makontena japo kuna sheria za uchukuzi? Tena mbona katika kipindi chake cha Urais walifanya maamuzi magumu ya kuwaalika wawekezaji waje kutwaa ardhi kwa ajili ya kilimo japo kuna sheria za ardhi za vijiji? Zaidi ya hayo mbona katika kipindi chake cha Urais walifanya maamuzi magumu ya kuleta barabara tatu jijini Darisalama japo kuna sheria za usalama barabarani?
 
Chimbuko la Ngeleja ni King Maker ambaye alinishinikiza mtu wa kulinda maslahi. Hana uwezo bali anaweza kutumika.
Tatizo ni la muda mrefu, Ngeleja anachokifanya ni kuficha ukweli kulinda wahalifu. Amekusanya wataalamu na kuwaagiza watengeneza upuuzi na kutumia muda na pesa za umma kuuwasilisha.
Ngeleja na Jairo wametoa rushwa ili tukubali matumizi ya kipuuzi ya fedha zetu. Hasara aliyolitia taifa kwa uzembe wa bajeti tu ni kubwa sana.
Huyu ni mshika pembe ili wengine wakamue, hafai si leo tu miaka mingi iliyopita. Aondoke!!

Rais anaijua vema wizara ya nishati na madini, hasa tatizo la umeme(alileta IPTL) hakupaswa kuwa safarini wakati nchi ina tatizo kama hili. Inatosha kukupa sura kwanini nishati haijapiga hatua miaka 30 iliyopita. Wakati nchi inakufa kiuchumi halafu rais yupo ziarani (by the way happy birth mandela) na kumwachia Ngeleja alete porojo inaeleza bila kificho kuwa tatizo si sera bali nani anajua sera na asimamieje sera hizo.

Kwa resource za nchi yetu kama maporomoko, makaa na upepeo kushindwa kuzalisha umeme wa kuuza nchi jirani ni fedheha na aibu kubwa.
Sera zote za nyuma zimeingiliwa na kukwamishwa na hujuma. Tusitegemee kuwa Dowans na IPTL au Kiwira ya Mkapa wangependa kuona vyanzo vingine vya umeme.Hizi zote ni hila ili waendeshe miradi yao.

Ilipotokea hujuma ya nishati ni rais aliyewakingia wahalifu kifua . Vyombo vinavyohusika kama Polisi, PCCB na DCI vyote havina kazi. Mambo yaKawekwa chini ya kapeti huku DCI akidai mwenye ushahidi apeleke kwake, PCCB wakiandika taarifa za kipuuzi na Polisi wakikimbizana na wapinzani.

Hitimisho: Ngeleja aondoke tu ili tusisikiea hadithi zake zinazotukera kila asubuhi. Yeye ni kasehemu tu ka tatizo kubwa sana, aliyoyafanya na Jairo yana baraka zote kutoka ndani, lakini aondoke tusisikie sauti yake tu yenye kutia hasira na machungu.

Rais ameshindwa kulisimamia suala la nishati. Nchi haina nishati na rais yupo bize akishawishi wawekezaji!.
Asikimbie tatizo kwasababu yeye ni mkuu wa nchi na ni sehemu ya tatizo hili kwa miaka 25 iliyopita.

Ngeleja na Jairo ni wateuliwa wake, uvundo wao ni sehemu ya uvundo wa serikali na wala hatuhitaji apigiwe simu kwa hili, arudi nchini kusimamia tatizo la nishati linaloathiri huduma za kiuchumi na kijamii. Inflation inaongezeka, unemployment inazidi, watu wanakufa mahospitali n.k
Arudi kushughulikia tatizo la nishati kwa dharura.Kumfukuza Jairo hakutaleta umeme, yeye aje atueleze anafanya nini kuhusu hili tatizo.

Hujuma kubwa katika sekta ya nishati inafanyika kwa msaada wa viongozi waandamizi serikalini. Hatuwezi kuendeleza sekta hii katika hali ya mfumo wa siasa uliopo. Suluhisho la nishati na madini litapatikana tukiwa na mfumo mwingine wa utawala sio huu ulioshindwa miaka 30 iliyopita.
Hatuhitaji sera, zipo nzuri sana, tunahitaji msimamizi wa sera za nishati na madini, mkweli mwenye maono, asiye na tamaa na anayeipenda hii nchi.

Kwa dharura iliyopo, hatuhitaji kusikia Ngeleja au Jairo. Tunataka mkuu wa nchi arudi nyumbani kushughulikia tatizo hili la kitaifa.
Ugumu wote wa maisha ni kutokana na kutokuwepo msukumo wa serikali hasa Rais katika tatizo la nishati. Tusifanye Ngeleja au Jairo kuwa ni mada kubwa, not! Kubwa ni rais wa nchi kutojali tatizo hili kwa miaka 6 ya urais wake. Rais arudi nyumbani kutatua tatizo sio safari kila asubuhi.
 
Back
Top Bottom