Utetezi wangu wa wazi wa William Ngeleja - The use of Emergency Powers Act 1986

hili halina shaka lakini Ngeleja anacho kile tu ambaco amepewa. Kumuwekea mtu malengo ya kufikia kitu fulani halafu humpi nyenzo za kufikia malengo hayo kunawanyima waliompa malengo hayo kumdai kwanini hajayatimiza. Lakini vile vile wale wanaoweka malengo wanamuwekea malengo ya namna gani? Huwezi kumwambia Ngeleja atatue tatizo la umeme wakati uhuru wa kufanya hivyo unaamuliwa na Baraza la Mawaziri.

Pia inawezekana uhuru wa kugawa rushwa Ngeleja kapewa na Baraza la mawaziri?
 
Mzee Mwanakijiji umemaliza yote kuwa CCM ndiyo chanzo cha matatizo ya umeme. Wamekuwa wakitumia hela kibao kuingia madarakani lakini wanasahau kuwa wanapoingia wanatakiwa kufanya kazi. Pili nawashangaa wabunge wa CCM kupiga kelele sasa wakati wamekuwepo Bungeni miaka yote ikiwepo hii sita ya utawala wa Kikwete. kuwepo kwao bungeni kwa idadi kubwa ilikuwa ni kwa hasra na si faida. Wamekuwa na kazi moja kupitisha miswada kwa ushabiki wa kisiasa wakijifanya kukomoa upinzani sasa leo wanafifanya kutopisha budget. wanafiki wakubwa.
 
Mimi kwa kweli I don't subscribe na illusion kwamba leo wabunge wa CCM wamepata nuru ya kupigania utatuzi wa upungufu wa umeme. I really don't buy that.
 
Haya ni matokeo ya maamuzi yetu watanzania wote kushindwa kujua nini maana ya kiongozi . Kuanzia balozi hadi rais.
Tunaochagua ndo tuwajibike. Kama tulipewa rushwa na tukachagua, kwanini tuwalaumu walio fanya biashara wakafanikiwa kuingia mjengoni.

Hii adhabu inatustahili. Labda tutapata akili. Kampeni za matusi ndio tunazishangilia. Hatuangalii mtu kafanya nini, bali katoa nini. Ccm no.1 . Posho posho posho.

Wasomi nao wanafurahia kuitwa maprofesa, madokta, lakini mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmm.

Mitambo yote ife, tupate akili. Viwanda vishindwe kuzalisha.

Umeme umekatika, kwaherini.
 
Mimi kwa kweli I don't subscribe na illusion kwamba leo wabunge wa CCM wamepata nuru ya kupigania utatuzi wa upungufu wa umeme. I really don't buy that.
Nilishangaa juzi Mh Sitta aliposema suala la RicmMond ni lazima wahusika wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria. Ni Sitta huyu ambaye alitumia rungu la CCM kuzima hoja ya Richmond na kuifunga akisema itajadiliwa na kamati husika hadi leo ni kimya. Ni wabunge wa CCM waliokaa kimya kuhusu Dowans n.k. Hata pale wapinzani walipotaka kumsulubu Ngeleja mapema kabisa CCM walitumia wingi wao na nguvu ya Spika kuzima hoja. Kama sitakosea kuna hoja ya mbunge wa upinzani kuhusu umeme ilizimwa na Spika wa CCM. Dhati ya kushughulikia umeme ipo wapi.

Bajeti ya Ngeleja ilipita katika kamati licha ya tuhuma za bahasha, kwa maneno mengine ilikubalika na kamati inayoongozwa na January Makamba.
Ni jambo la kushangaza January huyo huyo anapomhoji ngeleja wakati alishampa go ahead. Dhati ipo wapi!
Bajeti hiyo ilipita baraza la mawaziri, sijui hawakuona mapungufu! dhati ya kushughulikia umeme ni ya kuhoji.

Kwa mtazamo wangu kilichotokea ni zao la makundi ndani ya chama ambayo yamezaa kitu kingine.
Pesa za Jairo hazikufikia walengwa wote bali kuzima midomo ya vinara.
Ukizingatia Ngeleja ni kijana wa mzee RA kundi hasimu halikunufaika na mgao. Ndipo wakaamua kumwaga maharage. Ndani ya bunge wapo wasiofaidika na mgao na wanaoamini uwepo wao bungeni ni kutokana na kuwa ndani ya CCM. Hawa wakabaini kuwa kama ilivyo Richmond ndivyo Jairo gate itakavyopeleka chama pabaya zaidi. Wanajua ubunge ni sehemu ya kazi na maisha yao na kwa kutofaidika na mgao huenda wakaenda na maji. Ndicho kinachoonekana kuleta sintofahamu ndani ya bunge.
Ukweli unabaki pale pale, ni masilahi na si umeme kama wanavyotaka tuamini.

Kama wabunge wa CCM wangetaka suluhu ya tatizo hili tusingefika hapa tulipo. Wakati akina AL Adawi wanakuja, Ngeleja anaendeleza porojo, Symbion inabadilishwa jina kutoka Punda kuwa farasi, Songas wanazua ya kuzua n.k hakuna mbunge wa CCM aliyekuwa tayari ku-intervene. Leo ujasiri wameupata wapi? Wote wanasema Ngeleja na Jairo wajiuzulu lakini hawasemi washtakiwe.
Umeme aongelee mwingine sio CCM.
 
Kama wabunge wa CCM wangetaka suluhu ya tatizo hili tusingefika hapa tulipo. Wakati akina AL Adawi wanakuja, Ngeleja anaendeleza porojo, Symbion inabadilishwa jina kutoka Punda kuwa farasi, Songas wanazua ya kuzua n.k hakuna mbunge wa CCM aliyekuwa tayari ku-intervene. Leo ujasiri wameupata wapi? Wote wanasema Ngeleja na Jairo wajiuzulu lakini hawasemi washtakiwe.
Umeme aongelee mwingine sio CCM.

Absolutely. Thats exactly my point. Kwamba watu wanaiangalia CCM kutatua tatizo hili haingii akiilini. Wengine wanasema ati viongozi vijana wa leo wana mwanga zaidi? Really? Kikwete alipoteuliwa kuwa Waziri wa Nishati (akiwa Naibu kwanza) alikuwa na miaka 40! Miaka ishirini baadaye - tunaambiwa ni mzee - lakini anatushakizia viongozi vijana! Sina tatizo na ujana as ujana - ni uwezo. Lakini leo wabunge hawa wa CCM ambao wamekuwa wakija na mipango mbalimbali isipokuwa ya kutekeleza suluhisho la umeme.

a. Walipitisha mifuko ya Jimbo - licha ya ukweli kwamba Jimbo ni sehemu ya Manispaa, Wilaya, Mkoa sehemu ambazo zinatengewa fedha kila mwaka! Tukapiga kelele lakini wakapitisha kwa mbwembwe na cha kusikitisha wakiungwa mkono kwa kiasi kikubwa na upinzani.

b. Ni hawa hawa CCM waliotunga sheria zote tunazotumia nchini! Leo wanakuwa wa kwanza kulalamikia Mikataba; ati wanashangazwa mambo yasipoenda vizuri. Hivi, mlimsikia Chenge akitoa maoni yake kuhusu Tatizo la umeme nchini? Wakati tunapigia kelele kutowalipa Dowans mwenzetu akaenda na kuwatetea kwa maandishi! - mbona hajatoa maoni yake kuhusu hili la umeme?

c. Leo hii IPTL imeamuriwa kufilisiwa. Kwa miaka karibu ishirini sasa sakata la IPTL tunalijua. LImeandikwa vizuri lakini hadi kampuni hii inafilisiwa CCM na wabunge wake wamefanya nini?

Leo katika kushindwa kwao Marekani imeanza kuwasaidia. Leo Wamarekani wanasambaza nyaya (na kukusanya intelligence za nchi of course); wameingia katika uzalishaji wa umeme - na nitakuwa mtu wa mwisho kushtuka nikisikia Marekani imeingia Mkataba na RUBADA kuendeleza SG. Lakini utashangaa wakija hawa hawa walioshindwa kutaka kupewa credit!

You said it - kwenye suala hili la umeme CCM wakae pembeni watu wengine wazungumze.
 
Leo Wamarekani wanasambaza nyaya (na kukusanya intelligence za nchi of course); wameingia katika uzalishaji wa umeme - na nitakuwa mtu wa mwisho kushtuka nikisikia Marekani imeingia Mkataba na RUBADA kuendeleza SG. Lakini utashangaa wakija hawa hawa walioshindwa kutaka kupewa credit! .
Mzee Mwanakijiji, nimeipenda hii - (na kukusanya intelligence za nchi of course)
" I fear the Greeks, especially when they bring gifts!". Kumbe sasa not only the Greeks, hata "marafiki zetu" Wamerekani!.

It is very unfortunately for my beloved country Tanzania as beggars as we are, ("Beggars can not be chooses") ,we can not choose, we just has to swallow the bitter with the sweeter!.

Pasco
 
Watu tuna kumbukumbu fupi sana na ukweli huu umejidhihirisha hivi sasa kwenye haya matatizo ya umeme. Waziri Ngeleja anaoneka ndiye kama vile amesababisha matatizo yote haya wakati ukweli wa mambo umeme wa uhakika umekuwa tatizo sugu Tanzania.

Sasa iweje Ngeleja leo abebeshwe msalaba wa lawama na shutuma wakati mawaziri wa nishati na serikali zilizopita zimemrithisha tatizo? Hiyo si haki hata kidogo. Jaribuni tu kurudi nyuma miaka 20 iliyopita muone ni kina nani waliweza kupata fursa ya kuongoza wizara hiyo na walifanya nini kuhakikisha tatizo linakuwa historia.

I cut him some slack!!

mzee safi sana, kwa sababu makosa yalifanyika miaka 10 iliyopita ndani ya wizara hii basi na huyu aliyekaa miaka 4 wizarani hapo hana hoja ya msingi ya kujibu kwa wananchi kuhusu hili GIZA tulilonalo?

Kwa hiyo wewe ukipata kazi ku manage project A, unaendeleza strategic plan ulizozikuta hata kama ni mbovu? Baada ya kufika wizarani alitakiwa kufanya maamuzi na kuishauri serikali kuu - hakufanya hivyo kwa sababu zake ndiyo maana tunasema AENDE ZAKE.
 
Back
Top Bottom