Taifa Gas yaipa Serikali Mitungi 10,000 ya Gesi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Serikali ya Tanzania imekabidhiwa mitungi 10,000 ya gesi, ikiwa ni juhudi ya kuunga mkono kampeni ya matumizi ya nishati safi nchini.
Mitungi hiyo imekabidhiwa kwa Serikali jana Jumamosi, Machi 9, 2024 na Kampuni ya Taifa Gas.

Makamu wa Rais, Dk Phillip Mpango alipokea mitungi hiyo kutoka kwa Meneja mkuu wa Taifa Gas, Devis Deogratius kwa kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa kongamano la wanawake la kuhimiza matumizi ya nishati safi jijini Dodoma.

Akizumgumza katika kongamano hilo, Deogratius aliipongeza Serikali kwa juhudi za kupambania Watanzania, ili wawe miongoni mwa nchi zinazotamba duniani katika kutumia nishati safi ya kupikia.

Katika kongamano hilo lililoandaliwa na Wizara ya Nishati na kuhudhuriwa na mamia ya kinamama kutoka pembe zote za nchi, Deogratius alieleza mikakati ya kampuni hiyo inayolenga kuhakikisha kwamba gesi inapatikana katika kila mlango wa Mtanzania.

Alisema Taifa Gas katika mikakati yake, itaendelea kufanya kazi na wadau wote, wakiwemo Serikali kupitia Wizara ya Nishati , wabunge , Serikali za mikoa, wilaya na ngazi nyingine, ili kufanikisha agenda ya matumizi ya nishati safi nchini.

Makamu wa Rais, Dk Mpango alipongeza hatua ya Taifa gesi ya kutoa mitungi hiyo 10,000 na kusema itasaidia pakubwa katika kuhakikisha makundi yanayostahili kupata gesi yanafikiwa.
 
Amegawiwa nani hiyo mitungi
 
Hivi Mwenezi si alishamwambia huyo mwenye mitungi aondoke nchini kutokana na ufisadi!!! Sasa mbona chama kinapokea mitungi yake
 
Mitungi wapewe walimu, japo hawatoweza kuilipia, inabidi twafa gesi , wawalipie
 
Gesi ya kwetu, ardhi ya kwetu,pesa za kwetu lakini gharama za gesi zipo juu sanaa.. Hii nchi haina maana
 
Hivi Mwenezi si alishamwambia huyo mwenye mitungi aondoke nchini kutokana na ufisadi!!! Sasa mbona chama kinapokea mitungi yake
Kwenye kila misafara ya mama yumo, kuondoka yule sio rahis labda watz wao ndio wa kutoka
 
Back
Top Bottom