- Source #1
- View Source #1
Wakuu nimekutana na hii Taarifa je ni ya kweli?
- Tunachokijua
- Balozi Humphrey Polepole ni wanasiasa na mwanadiplomasia kutokea nchini Tanzania ambaye amaye amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi (CCM), mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzani na Balozi wa Tanzania nchini Malawi na baadaye Cuba
Madai
Zipo taarifa zinazoeleza kuwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba ambaye amejiuzuru kuwa sababu ya kuenguliwa kwenye nafasi yake hiyo ni kutokana na utendaji mbovu uliosababishwa na hati chafu ripti ya CAG.
Taarifa hiyo imeambatana na grafiki inayoonekana kuwa na nembo ya Mwananchi ikiwa na tarehe ya leo Julai 14, 2025.
Uhalisia wa taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa si ya kweli.
Hakuna vyanzo vyovyote vya kuaminika vilivyotoa taarifa ya utendaji kazi mbovu wa Balozi Polepole ama kutajwa kuwa na hati chafu katika ripoti ya CAG. Aidha Balozi Polepole hajaenguliwa bali amejiuzuru mwenyewe.
Polepole alichapisha barua ya kujiuzuru kwake kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram na kueleza sababu za kufanya hivyo.
Miongoni mwa sabababu alizozitaja Polepole ni kuwa hawezi
kuendelea kuwa sehemu ya uongozi usiohamasika na utii wa misingi ya katiba ya nchi na chama, haki, maadili, utu na uwajibikaji kwa wananchi.
Grafiki inayoonekana kuwa ni ya Mwananchi pia ni ya kughushi kwani haijachapishwa na chanzo hicho. Hata hivyo grafiki hiyo ina mapungufu kadhaa ikiwemo kutumia aina tofauti ya mwandiko na mpangilio ukilinganisha na grafiki halisi za chanzo hicho.