SoC01 Utegemezi wa nchi za Afrika barani Ulaya, umeendelea kuwa tatizo sugu. Maoni haya yenye tija yatasaidia kupunguza utumwa huu

Stories of Change - 2021 Competition
Sep 6, 2021
24
111
Na Elivius Athanas.
0745937016.

Nchi nyingi za Kiafrika zimeendelea kuwa tegemezi Barani Ulaya, Amerika, Asia na Mataifa mengine toka Mabara ya nje.
Serikali nyingi za Afrika, zimeendelea kutegemea mikopo, misaada na sera za kiutawala na kiuchumi kutoka Mataifa hayo.
Utumwa huu usiokoma, unachagizwa na ukweli kuwa, Nchi nyingi za Afrika bado ni masikini na viongozi wake hawachukui hatua muhimu kukomesha utumwa huu, licha ya Nchi hizi kuwa na rasilimali na miundombinu inayojitosheleza kukomesha umasikini unaozikabili Nchi zao ili kuondokana na 'pepo' hili la utegemezi.

TANZANIA.
Hadi kufikia Januari 10, 2021, Deni la Taifa lilifikia Sh. Trilioni 60.
Hii ni hatari kwa mama Tanzania.

KENYA.
Hadi kufikia Januari 5, 2020, Deni la Taifa la Jamhuri ya Kenya, liliongezeka kwa asilimia 15 na kufikia Sh. 6.8 Trilioni.
Hili siyo jambo la kufurahia!

UGANDA.
Hadi kufikia Mei 11, 2021, Deni la Taifa la Uganda, lilitarajiwa kuongezeka hadi asilimia 49.9 ya pato la Taifa ifikapo mwisho wa mwaka (2021) ~ BBC.
Hii siyo habari nzuri kwa Waganda!

Mifano hiyo michache ya madeni ya Nchi za Afrika na misaada isiyo na ukomo, ni uthibitisho tosha kuwa, Afrika bado ni tegemezi Barani Ulaya, Amerika na Asia.

MAONI YENYE TIJA YATAKAYOSAIDIA KUPUNGUZA UTEGEMEZI WA AFRIKA BARANI ULAYA.

Moja, kutumia fedha za ndani katika miradi yake. Serikali za Afrika zianze kujifunza kutumia fedha zake za ndani kuendesha miradi yake ya maendeleo na mahitaji yake muhimu. Hili litafanikiwa endapo kutakuwa na ukusanyaji mkubwa wa mapato ya Serikali kwa kuzingatia sheria na taratibu.

Serikali ibuni mbinu muhimu zitakazosaidia kukusanya fedha nyingi bila kuwaathiri wananchi. Fedha hizo zitumike kugharamia miradi ya Serikali na mahitaji mengine muhimu.

Tunapokopa na kuomba misaada ili kuendesha miradi ya ujenzi na uchaguzi, tunaendeleza utegemezi na kuongeza deni la Taifa.
Hivi kweli hatuwezi kutumia fedha zetu za ndani kuendesha uchaguzi?
Hatuwezi kutumia fedha zetu za ndani kujenga miundombinu?

Tunaweza. Tuongeze wigo wa ukusanyaji mapato na kuwe na usimamizi mzuri, tutaweza kutumia fedha zetu za ndani kugharamia miradi yetu na mahitaji muhimu.
Hongera kwa Serikali ya awamu ya tano, iliweza kuendesha uchaguzi kwa kutumia fedha za ndani. Kumbe inawezekana!

Mbili, tusomesha wataalamu nje kisha warudi nyumbani kusaidia na kulitumikia Taifa.
Tunapotumia wataalamu wa nje katika shughuli na miradi mbalimbali, tunaongeza utegemezi na kutumia fedha nyingi. Ni mara mia kutumia fedha kusomesha wataalamu wetu nje kisha warudi kulitumikia Taifa letu.

Ni aibu ya karne, kiongozi kwenda kutibiwa Ulaya wakati tuna uwezo wa kusomesha madaktari na wanafunzi wetu nje wakaja kutoa matibabu hayo hapa hapa nyumbani.

Tusomeshe Daktari mmoja Ulaya, aje atibu watu miamoja hapa nyumbani kuliko watu miamoja wakatibiwe na Daktari mmoja Ulaya. Hesabu gani hizi?

Kutegemea wataalamu wa nje kunaongeza utegemezi wa Afrika nje na kusababisha upotevu mkubwa wa kodi za raia masikini.

Tatu, Viongozi wenye maono na wabunifu wanahitajika Afrika.
Tatizo kubwa 'linaloitafuna' na kuimaliza Afrika ni viongozi wabovu.

Afrika imejaaliwa rasilimali nyingi kama vile madini, vivutio vya kitalii, ardhi yenye rutuba na kadhalika. Tatizo kubwa ni kuwa, tumekosa viongozi wenye maono na wabunifu ambao wanaweza kusimamia rasilimali zetu vizuri ili kukuza uchumi na kuondoa umasikini, ambao unatufanya tuendelee kuwa tegemezi.

Viongozi wengi wa Afrika, 'wananuka' rushwa na ufisadi.
Wanatumia rasilimali za Nchi kujineemesha wao na vitambi vyao.
Wanatunza pesa Ulaya, wanajenga Ulaya na kufaidi kodi za wananchi.
Ufisadi huo wa rasilimali za Afrika, unaongeza umasikini wa Nchi za Afrika unaoendelea kusababisha utegemezi.

Nne, tukomeshe vita vya wenyewe kwa wenyewe na migogoro ya ndani kwani huleta uvamizi unaosababisha utegemezi.
Nchi nyingi za Afrika zinaandamwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na migogoro ya ndani inayosababishwa na machafuko ya kisiasa na ukabila.

Nchi kama Congo, Sudani, Burundi na kadhalika, zinaandamwa na vita na migogoro ya ndani.
Migogoro hii husababisha Mataifa haya kuvamiwa na wageni kwa mwamvuli wa kusuluhisha, matokeo yake kusababisha utegemezi mkubwa wa chakula, silaha, mikopo na kadhalika.
Mbali na hapo, vita na migogoro ya ndani, huchochea utengano na umasikini wa Taifa ambao husababisha Taifa hilo kuanza kutegemea misaada na mikopo.
Tukomeshe vita na migogoro ya ndani ili tusiwe tegemezi.

Tano, Waafrika tuwe wazalendo kwa Nchi zetu.
Waafrika tupende vya kwetu, tupende na kununua bidhaa zetu, tununue nguo zetu, tupende miziki yetu, tupende utamaduni wetu na kadhalika.

Tunapopenda na kununua vitu vya kwetu, tunaongeza kipato kwa Nchi zetu, tunaongeza kipato kwa watu wetu. Tunaponunua vya nje, tunawaneemesha wa nje bila sababu.

Uzalendo huu utasaidia kuongeza pato la Taifa na kusaidia kupunguza utegemezi kwa njia moja au nyingine.
Ni muhimu sana kuthamini vya kwetu.

MWISHO. Umoja wa Afrika ulio imara na usio na uoga. Ili Bara la Afrika liwe huru na liepuke utegemezi, tunategemea pia Umoja wa Afrika ulio imara na usio na uoga.

Umoja wa Afrika uwe na sauti ya kukemea na kuwawajibisha viongozi wa Afrika, wanaosababisha machafuko ya kisiasa yanayosababisha vita.
Umoja wa Afrika uwe na sauti ya kuwalinda viongozi wazalendo wa Afrika, wanaochokozwa au kuingiliwa kiutendaji na Mataifa ya Ulaya bila sababu za msingi.

Umoja wa Afrika uwe na uwezo wa kuwaunganisha Waafrika pamoja na kusimamia kwa pamoja sera za kiuchumi, zitakazosaidia kuwakwamua kiuchumi na kuepuka utegemezi.

Umoja wa Afrika wenye sifa hizo, utasaidia sana kupunguza utumwa wa Nchi za Afrika Barani Ulaya, Amerika na Asia.

Ahsante kwa kusoma makala haya.
 
Wewe bado kanafunzi ka secondary!! unajribu jaribu tu!! kuwa pamoja na wasomi! ........au km ni mtu mzima ulikomea sec. tu! tena ulikuwa failure!! divison six! sasa una copy kazi za wenzako waliokuwa wanajifunza somo la siasa!!! hukuendelea mbele!

na km ulifaulu vizuri sec. na kuendelea mbele!!! nina Mashaka na ufaulu wako!! au utakuwa umenunua mitihani! kabisaaaa! hizi ni siasa za std seven! kabisaaaa!
 
Mataifa makubwa hatawakubali kuona umoja wa Africa ukipata nguvu, ili waendelee kututawala...
 
Afrika inakwama sababu ya wananchi wake na siyo viongozi tu. Waafrika wote tunazingua.
 
Back
Top Bottom