Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,275
Katika kumbukumbu za ukoloni, sifa kubwa ya Hispania ilikuwa ujenzi. Walibuni na kujenga majengo ya kupendeza kama vile sifa ya Uingereza ilivyokuwa katika utawala bora.
Katika Afrika, Hispania ilitawala Equatorial Guinea, mpaka sasa hivi Kispaniola ndiyo lugha rasmii ya nchi hii.
Wakati Hispania inatawala Equatorial Guinea, walijikita zaidi katika kilimo cha cocoa. Equatorial Guinea ilizalisha cocoa zaidi ya nchi jirani kama Ghana, Nigeria na Ivory Coast licha ya nchi hizo kuwa na ardhi kubwa kuliko Equatorial Guinea. Taarifa hizi zilitoka baadae sana kwani Hispania hawakuziweka wazi wakati wa utawala wake. Inasemekana walitumia utaalamu mkubwa katika kilimo cha cocoa.
Ugunduzi wa mafuta Equatorial Guinea ulitokea baada ya kupata uhuru wao kutoka Hispania mwaka 1968.
Amerika ya Kusini, Hispania ilitawala Cuba, Puerto Rico, Caribbean na nchi zote zinazoongea Kispaniola. Kumbukumbu walizoacha katika sehemu hizi nidini ya Ukatoliki na majengo nadhifu.
Majengo ya Equatorial Guinea pia ni tofauti ingawa inaonekana tangu Hispania ilipoondoaka miundo mbinu iliyoendelezwa ni michache pamoja na utajiri wao wa mafuta.
Majengo ya ki historia yaliyoachwa na Hispania mjini Sao Paul
Kanisa Katoliki Equatorial Guinea
Hispania pia ilitawala Philippines, jina hili lilitolewa kama zawadi na kumbukumbu ya mfalme wa Hispania wa wakati huo Mfalme Phillip.