Utata juu ya Rais Samia kuingilia kati tozo mpya za miamala

Rais Magufuli alisitisha kanuni iliyokuwa imeleta hicho kikokotoo kipya, hakikuwa kimewekwa kwenye sheria (correct me if I'm wrong) sina uhakika kama Rais ana mamlaka ya kusitisha sheria kufanya kazi...kama inawezekana naomba unisaidie kunionyesha ni wapi mamlaka hayo yameainishwa....
Sijaweza kukopi kipengele cha katiba kinachompa mamlaka hayo Rais ....lakin Nina uhakika asilimia mia kuwa ana mamlaka hayo ....harafu ile yarate Magufuli ilikuwa tayari sheria sio kanuni Mana ilipitishwa na bunge na kusainiwa na yy mwenyew
 
Muambieni mama asiivunje katiba, suala la tozo ni la kisheria...kama bunge lilijadili na kuridhia huo muswada, na yeye akatia saini basi sheria itekelezwe kama inavyosema. Mambo ya kupitisha kanuni ama kuisimamisha sheria ya hizi tozo ni kutunyima haki yetu ya msingi !
Bunge lipi lililopitisha hiyo sheria?. Hili hili genge la watu fulani?. Hivi hawa wanaojiita majitu wabunge kitu walichokipitishia,wananchi wanakigomea 100% huwa wanajionaje?,wanajisikiaje?
 
Kuna taarifa zinazopotosha kuwa Raisi eti kaingilia kati suala la Tozo, jambo hili si sahihi kuliweka au kulifanya lieleweke hivi.

Raisi alijua kila kitu na documents aliziona pia. Kwahio tukubali tu kuwa CCM walichemka na credit ziende kwa Upinzani

View attachment 1860029

View attachment 1860030
Hii ni typical Magu style, anaanzisha tatizo kisha analitatua kutafuta kiki kama ilivyokuwa kwenye sakata la kikokotoo
 
Sijaweza kukopi kipengele cha katiba kinachompa mamlaka hayo Rais ....lakin Nina uhakika asilimia mia kuwa ana mamlaka hayo ....harafu ile yarate Magufuli ilikuwa tayari sheria sio kanuni Mana ilipitishwa na bunge na kusainiwa na yy mwenyew
Hivi Rais ana mamlaka ya kufuta sheria iliyopitishwa na bunge baada ya yeye kuisaini?
 
Hahahaa hahhaahha
Basi piga hesabu ya hizo gharama alafu bado wanasema mwezi August na line za simu zitaanza kutozwa kodi ,yuko sawa huyu jamaa !
Uzuri haya mambo hayawapati wana CCM. Wapinzani tu ndio yanawapata.
 
Rais huwa anadanganywa sana na washauri ,usikute kwenye kikao chao cha baraza la mawaziri wamemwambia wamefanya tafiti na risk assessment zimefanyika kwahiyo waende kwenye implementation tu ,Rais anawategemea wataalam sasa hao wataalamu ndio wanamuangusha.
 
Tengeneza tatizo halafu litatue , mule mule kwa Mwendazake in copy and paste.

IMG_5749.jpg
 
Mi nimetafakari kwa kina sana ila nimeshindwa kupata jibu. Yafuatayo najiuliza

1. Mh. Rais alisaini au hakusaini hiyo sheria ya TOZO mpya?

2. Kama alisaini, je alikuwa anapima upepo wa wananchi?

3. Je, ni political tension?

4. Je, itakuwa imemuongezea asilimia za kuupiga mwingi?

Kama kuna mtu anaweza kuongeza maswali na majibu.

Asante.
Majibu HAYA HAPa

 
Back
Top Bottom