Rais Samia, ulitaka wananchi tukataaje tozo za miamala ya simu?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa, umenifikirisha na kunisikitisha sana. Nimekusikiliza na kukutazama kwenye mahojiano yako na mwandishi na mtangazaji nguli Salim Kikeke. Nimekufuatilia hadi nikalia ulipokuwa ukijibu maswali bila kujali athari.

Juu ya tozo za miamala ya simu, nimekusikia na kukuona ukisema kuwa wananchi hatukukataa tozo husika. Sijakuelewa;sitakuelewa na sikuelewi juu ya kauli hii. Zilipoanza tu tozo zilizua mzozo. Wananchi walisema kwa kuhema; waliandika na kusikika kupinga tozo husika. 'Walimsema na kumlaani' hata mwanzilishi wa hoja ya tozo. Yupo hadi aliyetinga mahakamani kupinga tozo hizo.

Tuliambiwa na Waziri Mwigulu kuwa wewe Rais umesikia kilio chetu na kinafanyiwa kazi. Ulisikia kilio kipi kama si malalamiko na masikitiko yetu wananchi yanayoonesha kuwa tunazipinga tozo hizo? Ulitaka na kutamani wananchi wapingeje zaidi ya hivyo?

Labda ulitaka wananchi tuandamane. Labda ulitaka wananchi tuache kutuma na kupokea pesa kwa njia ya miamala ya simu. Labda ulitaka wananchi tuanzishe vurugu na kupafanya mitaani kuchafuke. Lipi hapo lingekuonesha kuwa tumezipinga na kuzikataa tozo za miamala ya simu? Kauli yako siwezi kuielewa kirahisi.

Rais Samia, sisi watanzania tunazipinga na kuzikataa tozo za miamala ya simu kwa ujumla wake.

Pumzika kwa amani mtani na mdogo wangu Elias Kwandikwa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mwanza Mjini)
 
Alisema tozo za simu ni kwamatatizo yenu ili kuharakisha maendeleo vijijini
 
Mkuu imetoka hiyo..tuizoee tuu hakuna namna. Hivi kwa akili yako, unaamini kweli Mwigulu angeweza kuweka hiyo tozo bila baraka za Magogoni?

Nadhani wadanganyika tufike mahali tukubali kwamba tumeshakabishi maisha yetu kwa wanasiasa wa CCM na tutafanya lolote watakalotuamrisha! Sad but true.
 
Kama kungekuwa na vyama imara vya upinzani hili lilikuwa tundu la kutokea.
 
Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa, umenifikirisha na kunisikitisha sana. Nimekusikiliza na kukutazama kwenye mahojiano yako na mwandishi na mtangazaji nguli Salim Kikeke. Nimekufuatilia hadi nikalia ulipokuwa ukijibu maswali bila kujali athari.

Juu ya tozo za miamala ya simu, nimekusikia na kukuona ukisema kuwa wananchi hatukukataa tozo husika. Sijakuelewa;sitakuelewa na sikuelewi juu ya kauli hii. Zilipoanza tu tozo zilizua mzozo. Wananchi walisema kwa kuhema; waliandika na kusikika kupinga tozo husika. 'Walimsema na kumlaani' hata mwanzilishi wa hoja ya tozo. Yupo hadi aliyetinga mahakamani kupinga tozo hizo.

Tuliambiwa na Waziri Mwigulu kuwa wewe Rais umesikia kilio chetu na kinafanyiwa kazi. Ulisikia kilio kipi kama si malalamiko na masikitiko yetu wananchi yanayoonesha kuwa tunazipinga tozo hizo? Ulitaka na kutamani wananchi wapingeje zaidi ya hivyo?

Labda ulitaka wananchi tuandamane. Labda ulitaka wananchi tuache kutuma na kupokea pesa kwa njia ya miamala ya simu. Labda ulitaka wananchi tuanzishe vurugu na kupafanya mitaani kuchafuke. Lipi hapo lingekuonesha kuwa tumezipinga na kuzikataa tozo za miamala ya simu? Kauli yako siwezi kuielewa kirahisi.

Rais Samia, sisi watanzania tunazipinga na kuzikataa tozo za miamala ya simu kwa ujumla wake.

Pumzika kwa amani mtani na mdogo wangu Elias Kwandikwa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mwanza Mjini)

Tuikatae vipi wakati tumieridhia na tulipenda iwe hata maradufu?!
 
Mungu mjalie afya njema Rais Samia, aendelee kuupiga mwingi.

Sisi watanzania ni wepesi wa kusema, ila vitendo ni sufuri..

Mpe Rais moyo mgumu zaidi na wepesi wa maamuzi ili upigwe mwingi zaidi..

1 Timotheo 2:1-2​

Kwanza kabisa, nawasihi muombe dua, msali na kumshukuru Mungu kwa ajili ya watu wote, kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema.
 
Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa, umenifikirisha na kunisikitisha sana. Nimekusikiliza na kukutazama kwenye mahojiano yako na mwandishi na mtangazaji nguli Salim Kikeke. Nimekufuatilia hadi nikalia ulipokuwa ukijibu maswali bila kujali athari.

Juu ya tozo za miamala ya simu, nimekusikia na kukuona ukisema kuwa wananchi hatukukataa tozo husika. Sijakuelewa;sitakuelewa na sikuelewi juu ya kauli hii. Zilipoanza tu tozo zilizua mzozo. Wananchi walisema kwa kuhema; waliandika na kusikika kupinga tozo husika. 'Walimsema na kumlaani' hata mwanzilishi wa hoja ya tozo. Yupo hadi aliyetinga mahakamani kupinga tozo hizo.

Tuliambiwa na Waziri Mwigulu kuwa wewe Rais umesikia kilio chetu na kinafanyiwa kazi. Ulisikia kilio kipi kama si malalamiko na masikitiko yetu wananchi yanayoonesha kuwa tunazipinga tozo hizo? Ulitaka na kutamani wananchi wapingeje zaidi ya hivyo?

Labda ulitaka wananchi tuandamane. Labda ulitaka wananchi tuache kutuma na kupokea pesa kwa njia ya miamala ya simu. Labda ulitaka wananchi tuanzishe vurugu na kupafanya mitaani kuchafuke. Lipi hapo lingekuonesha kuwa tumezipinga na kuzikataa tozo za miamala ya simu? Kauli yako siwezi kuielewa kirahisi.

Rais Samia, sisi watanzania tunazipinga na kuzikataa tozo za miamala ya simu kwa ujumla wake.

Pumzika kwa amani mtani na mdogo wangu Elias Kwandikwa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mwanza Mjini)
Endeleeni kuupiga mwingi si ndio nyie mlipiga vigelegele kuwa sasa mumempata mtu wa watu, msikivivu na misifa kibao, leo kulikoni? sisi wengine bado tuko kwenye maombolezo ya mwendazake, enzi zake haya mambo yasingetokea asilani. Kama mwendazake aliweza iweje sasa huyu ashindwe? jua kuna kitu hapa, mngeanza kwanza kumkataza kuruhusu ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambayo haina tija na kuna watu wanufaika na hiyo kandarasi ya kitapeli na ndio sasa wanakomaa ili wao na familia zao wazidi kuneemeka, pamoja na ukwasi walio nao lakini bado tamaa zimewazidi, sasa wamekuwa ndio Alfa na Omega wa nchi hii, enzi za mwendazake waliwekwa kapuni. Kwa haya yanaoendelea tutazidi kumkumbuka jabali mwendazake.
 
Dah! Rais kwenye maswali ya mtego, na yanayo hitaji umakini mkubwa kwenye kuyajibu, yeye anatiririka tu 😁😁😁!

Yaani anajibu kiwepesi wepesi tu! Kama ilivyokua enzi za JK! Na yeye alikuwa anajibu huku anacheka na kutabasamu muda wote!! Watu wa Pwani tuna mambo kweli kweli.
 
Endeleeni kuupiga mwingi si ndio nyie mlipiga vigelegele kuwa sasa mumempata mtu wa watu, msikivivu na misifa kibao, leo kulikoni? sisi wengine bado tuko kwenye maombolezo ya mwendazake, enzi zake haya mambo yasingetokea asilani. Kama mwendazake aliweza iweje sasa huyu ashindwe? jua kuna kitu hapa, mngeanza kwanza kumkataza kuruhusu ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambayo haina tija na kuna watu wanufaika na hiyo kandarasi ya kitapeli na ndio sasa wanakomaa ili wao na familia zao wazidi kuneemeka, pamoja na ukwasi walio nao lakini bado tamaa zimewazidi, sasa wamekuwa ndio Alfa na Omega wa nchi hii, enzi za mwendazake waliwekwa kapuni. Kwa haya yanaoendelea tutazidi kumkumbuka jabali mwendazake.
Pamoja na mapungufu mengi ya Mama lakini ni bora mara mia kuliko yule muuaji
 
Mpka tuushambulie msafara wake kwa mawe ndo atajua hatutaki tozo.
 
Back
Top Bottom