Miaka ya hivi karibuni imekua ni wajibu kujengea kaburi. Mpaka miaka ya 60, si wengi walimudu gharama za kujengea kaburi. Baada ya mazishi mlisubiri mvua na kupanda tawi au shina la mti pale kwenye kaburi. Mvua zikikatika mti unakua umeshaota na kushika. Hii ndiyo alama ya kukumbuka kaburi la mpendwa wako.
Frangipani tree ambayo ilijulikana kama mi bono kaburi ndiyo miti iyliyotumika sehemu nyingi hasa za Pwani.
Katika historia, Wamissionary waliokufa Afrika kueneza Injili walitengeneza jiwe la kaburi liliandikwa jina, tarehe ya kuzaliwa na kuacha nafasi ya tarehe ya kifo. Wengi walifariki kwa kukosa huduma bora za matibabu.
Mikoa ya kaskazini waliweka miti aina ya Isale katika kaburi, kwa hiyo hata kile kifusi cha juu kikiisha yale masale yanabaki kama utambulisho kuwa hapa kuna kaburi