Utaratibu wa kujengea makaburi zamani walimudu wachache wengi waliweka alama za miti kwenye makaburi ya wapendwa wao

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,587
215,179
Miaka ya hivi karibuni imekua ni wajibu kujengea kaburi. Mpaka miaka ya 60, si wengi walimudu gharama za kujengea kaburi. Baada ya mazishi mlisubiri mvua na kupanda tawi au shina la mti pale kwenye kaburi. Mvua zikikatika mti unakua umeshaota na kushika. Hii ndiyo alama ya kukumbuka kaburi la mpendwa wako.

Frangipani tree ambayo ilijulikana kama mi bono kaburi ndiyo miti iyliyotumika sehemu nyingi hasa za Pwani.

1638570685860.png


Katika historia, Wamissionary waliokufa Afrika kueneza Injili walitengeneza jiwe la kaburi liliandikwa jina, tarehe ya kuzaliwa na kuacha nafasi ya tarehe ya kifo. Wengi walifariki kwa kukosa huduma bora za matibabu.
 
Na inamfanya marehemu asiwe comfortable na nyumba yake ya milele. Hapo ndio utasikia ' nyumba ina maruweruwe' kumbe marehemu anapigania haki yake.
Kila tunapotembea chini lilikuwa kaburi. Kumbuka babu zetu walihama kutafuta malisho na maji ya mifugo. Hakuna alyejengea makaburi watu walizikwa tu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom