Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 8,988
- 11,862
Utakuta Mtu Ameajiriwa Tayari Serikalini Lakini Bado Anafanya Maombi ya Ajira: Hawa Nao Wanasababisha Upungufu wa Ajira Nchini
Kuna watu ambao tayari wamepata ajira serikalini, wamepangiwa vituo vya kazi, na wanaendelea kupokea mishahara kila mwezi. Lakini jambo la kushangaza na la kusikitisha ni kwamba bado wanaendelea kutuma maombi ya kazi mpya kila mara nafasi zinapotangazwa.
Hawa si watu wasiokuwa na kazi ni watu waliomo ndani ya mfumo, lakini bado hawaridhiki. Kila nafasi mpya serikalini ikitoka, nao ni wa kwanza kutuma maombi kana kwamba hawajawahi kuajiriwa.
Kwa tabia hii, wanaziba fursa kwa vijana wengine wengi waliomaliza masomo yao na hawajawahi kuonja hata senti moja ya mshahara wa serikali. Wanatumia nafasi zao, uzoefu wao, na uelewa wao wa mifumo ya ajira kuwazidi nguvu wale ambao ndio wanatafuta fursa kwa mara ya kwanza.
Kwa kufanya hivyo, wanajenga kikwazo cha kimya kinachowazuia wengine kuingia kwenye ajira. Mzunguko huu unakuwa wa watu walewale, wakihamahama taasisi kwa maslahi binafsi, huku wengine wakizidi kusukumwa pembezoni mwa soko la ajira.
Kama hilo halitoshi, tabia hii ya kutokutosheka inachochea mgawanyo usio sawa wa rasilimali za ajira. Katika muktadha wa Theory ya Resource Allocation, nafasi za ajira ni miongoni mwa rasilimali adimu zinazopaswa kugawiwa kwa usawa kulingana na mahitaji halisi. Lakini unapopata watu wachache wanaozichukua nafasi nyingi kwa wakati tofauti, wanaharibu mfumo mzima wa usawa wa fursa.
Hali hii inachangia pia kuendeleza Viscous Circle of Poverty kwa wale ambao hawajawahi kuajiriwa. Watu wasio na kipato wanashindwa kupata uzoefu, kukosa fedha za kujiendeleza, na kuendelea kuwa kwenye mzunguko wa umasikini. Wakati huo huo, waliopata kazi wanazidi kujiimarisha zaidi, huku wakiwazuia wengine kupata nafasi ya kuingia kwenye mfumo.
Kwa hiyo, ni muhimu sana kwa waajiriwa wa serikali kutafakari kwa kina athari ya tabia yao. Kama tayari umeajiriwa, ni vyema kutimiza majukumu yako kwa uadilifu na uvumilivu badala ya kugeuza ajira kuwa daraja la kuruka kutoka nafasi moja hadi nyingine.
Na kwa mujibu wa kanuni rasmi, jambo hili tayari limewekewa miongozo. Applicants employed in the Public Service are strictly not allowed to apply, they should adhere to Circular No. CAC. 45/257/01/D/140 of 30th November, 2010.
Waraka huu ni muhimu sana, kwani unalenga kuhakikisha nafasi za ajira zinawafikia waliostahili hususan wale ambao hawajawahi kuajiriwa. Ni wajibu wa kila mtumishi aliyeajiriwa kuzingatia miongozo hii kwa nia ya kujenga jamii yenye usawa na haki ya kiuchumi kwa wote.
Ajira si mashindano ya kukimbilia zaidi ni nafasi ya kutoa huduma. Na nafasi moja ya kazi unayoiziba bila sababu ya msingi, inaweza kubadilisha maisha ya kijana mmoja asiye na msaada. Tafakari.