Utajiri wa kufa na kuoza ndio pesa ije

Utajiri wa kufa na kuoza ndio pesa ije

Aliyefufuka in Yesu pekee hakuna mwingine. Jaribu uone
Upo sahihi sana Mkuu, nimekupenda bure, Mtu yeyote anayemsifia Yesu Kristo Mimi huwa ninampenda kupita Maelezo japo Mimi ni mtu mwenye dhambi nyingi. Hao anaosema kuwa wanakufa sio Kufa kwa maana tunayoijua Mimi na wewe, Bali ni Kufa kimazingara.
 
Ni aina mojawapo ya uchawi wa kupata utajiri ukiacha huu wa ;
kuua ndugu
Kuwafanya wanafamilia ndondocha
Kuwekwa kidonda mwilini
Kupewa masharti ya chakula nguo na magari nk nk
Huu una mambo yake ya ajabu, unapewa dawa ambayo utamshirikisha mkeo tuu....ukishakunywa hiyo dawa unakufa na kuoza kabisa mpaka kutoa funza wengi
Sasa mkeo kazi yake kila siku itabidi awafagie hao funza na kuwaweka kwenye ndio kwa mpaka siku ya saba utakapofufuka..... utajiri wako utategemea na wingi wa funza watakaokusanywa kwa siku
Ukishamaliza siku Saba utafufuka na biashara zako zitaanza kuchanganya
Onyo na tahadhari
-hutakiwi kuwa na mwanamke mwingine
-mkeo hapaswi kushtuka mara ya kwanza akiwaona funza utakufa moja kwa moja
-so wewe wala mkeo mnapaswa kutoa siri hii kwa yeyote hata chini ya mtutu wa bunduki
-Ishu ya kufa wiki nzima na kuoza utaifanya kila biashara zinapoyumba
Kama bado unataka utajiri kwa njia za mkato fikiria mara mbili kabla hujamua
niliwahi kusikia kuwa aina hii ya utajiri ndio ilikuwa inatumiwa na wanamuziki nguli wa kikongo akina madilu system na pepe kale. na inasemekana vifo vyao vilitokana na wake zao kuvunja masharti, so wakafa moja kwa kwa moja.

NB
katika biashara ya mziki, mkongomani anaweza tumia mbinu zozote almradi tu afanikiwe na awe maarufu.
 
KAMWE, KWAMWE, KAMWE, usikae ufikirie kwenda kutafuta uchawi ili kutajirika. Ni ujinga mtupu. Hata ukipata pesa nyingi saaaana, unadhani utabadilika nini? Kitanda utalala kimoja tu, hata ukila chakula kitamu kuliko vyote, bado ukishashiba huwezi kuendelea kula tena. Na chote kitatoka baada ya masaa kadhaa. Hata ukimchukua mwanamke unayemwona ndio bora kuliko wote, utakuwa tu sawa na mtu mwingine yeyote aliye na mwanamke anayempenda. Hata ukinunua magari kumi ya bei mbaya, bado utaendesha moja tu kwa wakati mmoja. Ukijenga majumba lukuki, watalala wengine.

Sana sana , tafuta tu kipato ujenge nyumba, usomeshe watoto, uwe na kausafiri kako kanakoridhisha, na wewe na familia yako muwe mnavaa vizuri na kula vizuri. Zaidi ya hapo ni UBATILI TU.
 
Utajiri kazi !!! Hiyo kali ila watu hawataki kuumia ni kuwatesa wengine bila huruma . Jamaa kampachika ndugu yake likidonda kama la moto , hakioshi ila usaha kwa wingi ni mafanikio kwa jamaa , we acha tu !!
Jamani,unless Science nayo ni uchawi,BUT should we not even loose our precious time talking about witcheries...THERE is a lot in science to make each of us/most of US Rich!Najua yako mambo ya hivo ambayo ni primitive science ambayo kimsingi wengi wameya embrace...very poor way thinking especially we Africans..!
 
Mshana naona unafundisha "forbidden knowledge" naamini katika Mali ya jasho, ingawa nina maswali mengi kuhusu njia ya kuzipata (atoapo Mungu vs atoapo mfalme wa giza)....sitovunja matakwa ya maisha ili niwe tajiri. Maana sio malengo yangu na hata ikitokea itakua ni ajari tu, sina upekee wala lineage ya utajiri. Naamini utamu wa maisha ni matunda ya kuhangaika na kuyafurahia, hata watoto wangu nitawasimulia "nilijaribu kutafuta utajiri kwa ajiri yao na sio yangu, na hapa nilipofika ndipo nimekomea" ni zamu yao kushika kijiti hadi pale wao watakapo wapa watoto wao.
Baada ya Chalinze njia ya kwenda Tanga kaka
 
Nafikiri sayansi ni uchawi unaoonekana na kuna isiyoonekana ambayo ni 'UCHAWI" mwenye Phd katika sayansi inayoonekana anaweza kuruka na ungo ?? Mafanikio makubwa duniani ni uchawi uliokubuhu . Vitu unavyoviona sivyo vilivyo !! Utaniona na prado nzuri kumbe ni fisi !
 
Back
Top Bottom