Utajiri wa kufa na kuoza ndio pesa ije

Utajiri wa kufa na kuoza ndio pesa ije

Ndani ya maji,lazima iwe kuanzia siku Tatu na kuendelea, unaweza?
Kuna stori moja nilisikia kipindi sintosahu RFA, jamaaa alipewa sharti la kulala ndani ya kaburi nimesahau ni muda gani. Jaamaa anakwambia kilaa akiendaa kwenye maeneo ya makaburi ni lazma ajikwae ndy anajikuta yupoo ndani ya kaburi,... Kilaa akijaribu kujizuia hali ndy ile ile. Utajiri unamambo mengi.
 
Ni aina mojawapo ya uchawi wa kupata utajiri ukiacha huu wa ;
kuua ndugu
Kuwafanya wanafamilia ndondocha
Kuwekwa kidonda mwilini
Kupewa masharti ya chakula nguo na magari nk nk
Huu una mambo yake ya ajabu, unapewa dawa ambayo utamshirikisha mkeo tuu....ukishakunywa hiyo dawa unakufa na kuoza kabisa mpaka kutoa funza wengi
Sasa mkeo kazi yake kila siku itabidi awafagie hao funza na kuwaweka kwenye ndio kwa mpaka siku ya saba utakapofufuka..... utajiri wako utategemea na wingi wa funza watakaokusanywa kwa siku
Ukishamaliza siku Saba utafufuka na biashara zako zitaanza kuchanganya
Onyo na tahadhari
-hutakiwi kuwa na mwanamke mwingine
-mkeo hapaswi kushtuka mara ya kwanza akiwaona funza utakufa moja kwa moja
-so wewe wala mkeo mnapaswa kutoa siri hii kwa yeyote hata chini ya mtutu wa bunduki
-Ishu ya kufa wiki nzima na kuoza utaifanya kila biashara zinapoyumba
Kama bado unataka utajiri kwa njia za mkato fikiria mara mbili kabla hujamua


Mapesa niwe nayo alafu niwe na mwanamke mmoja??

Vipi nikitaka kumtangazia biashara mganga??
 
Back
Top Bottom