Utabiri wa TMA kila siku ni huu

Utabiri wa TMA kila siku ni huu

Kama hii ya Elnino, Mie nafikiri mvua zitanyesha lakini sio kwa kiwango kikubwa kama walivyotangaza na precautions kibao
 
Hizo mvua za maembe tu ni kawaida ,walivyosema elninyo tukajiaandaa kwa elninyo lakini olaaaaaaa.
Kwanza; El-Nino haimaanishi LAZIMA kunyeshe mvua kubwa kila sehemu duniani, Africa au Tanzania kwa wakati ule ule!

Kisayansi El-Nino ni hali ya ongezeko lisilo la kawaida la joto ndani ya bahari ya Pacific hasa upande wa mashariki. Kwa kuwa ni hali inayotokea kuelekea Christmas (kuzaliwa kwa Kristo) basi wenyeji wanaotegea bahari ya Pacific waliipa jina kitoto-cha kiume - EL-NINO!
Kinyume cha Elnino ni La-Nina (kitoto-cha kike) ikiambatana na kushuka kwa joto ndani ya Pacific.

NB: Kumbuka bahari ya Pacific ni kubwa (eneo lake ni kubwa zaidi ya jumla ya ardhi kavu ya mabara yote duniani).
Hivyo mabadiliko ya joto ndani ya Pacific yanaweza kusababisha mabadiliko ya joto dunia nzima.
Ili mvua inyeshe ama isinyeshe joto ni kiungo kimojawapo! Lakini pia kuna uoto wa asili, umbali kutoka vyanzo vikubwa vya maji, milima, n.k

Kiasili mzunguko wa El-Nino na La-Nina unaitwa El-Nino Southern Oscillation(ENSO) na hutokea kila baada ya miaka 2 hadi 7. Mzunguko wa miaka 7 pia umeandikwa hadi kwenye Biblia Takatifu (Soma Mwanzo 41 - Ndoto ya Pharao na tafsiri yake).

Mara nyingi athari za El-Nino ni pamoja na mvua...maeneo fulani ya Dunia... Na wakati huo huo ukame maeneo fulani ya Dunia.

Mabadiliko makubwa yanayoendelea ya tabianchi (climate change) yanaathiri vile vile mzunguko wa ENSO.
Kubwa zaidi ni kwamba mabadiliko ya tabianchi yana athari kubwa hata models/formula/mahesabu yanayotumika kwenye utabiri wa hali ya hewa.

In short things are no longer the same!
 
Japan wanakuambia kwa mfano mvua kubwa yenye kimbunga (typhoon) itanyesha mwezi December tarehe 16 maeneo haya, nakweli inakua.
Japan ipo kwenye ukanda wenye matukio makubwa ya majanga ya asili (natural catastrophies)!
Hivyo ili waishi ni sharti uwekezaji kwenye sayansi na teknolojia ya emergency preparedness iwe ya hali ya juu sana!

Tofauti kabisa na Tanzania utakuta uwekezaji kwenye siasa za visasi na kulaghai wananchi ni mkubwa kuliko kwenye sayansi na teknolojia ya emergency preparedness.
Ukweli ni kwamba TANZANIA; vifaa vya kukusanya taarifa za awali za hali ya hewa zipo kwenye viwanja vichache vya ndege ambako pia hakuna instantaneous online synchronization.

Hivi mtu upo Tabora ama Shirati huko unatarajia upate utabiri unaoeleweka wa hali ya hewa kwa kutegemea vifaa vichache vilivyopo Dar au Dodoma?
Wekezeni kwenye sayansi na teknolojia badala ya hafla zenye hotuba nzuri nzuri kipindi cha majanga!
 
Lakini huu utabiri sio TMA tu waliosema, hata BBC mara kwa mara wametoa tahadhari, let's not put blame kwa hawa jamaa, utabiri unabaki kuwa ubashiri japo kisayansi
We want assurance mkuu.
Japo wasiwasi ndio akili...

Walisema week la pili la oktoba mambo yatakuwa mazuri...

Paka sasa tunasubiri


Au Yule Mungu wa Mh makonda aliyemtaja amezuia mvua??
 
Back
Top Bottom