Usomaji wa Biblia kila siku unaongeza IQ kuliko kusoma kitabu kingine duniani

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,586
15,369
Watu wengi wenye IQ kubwakubwa mindset zao zilishawishiwa na Biblia.

Newton, Galileo Galilei, Mendel na wanasayansi wengi walikuwa wanazi wa maandiko ya Biblia.

Paulo kwa usomi wake maandiko aliwaoutsmart wasomi majiniasi wa kigiriki Pale Aelopagas.

Daniel aliwazidi akili wachawi,waganga, wasomi na wanasayasi wa dunia nzima enzi zake kwa sababu ya maandiko ya Mungu. Ndiye aliyetoa wazo la mfalme dario atawaleje. Structure ya utawala wake ilikuwa ile ya Daudi wa kwenye biblia.

Yesu akiwa 12 kwa sababu ya ujuzi wake wa maandiko IQ yake ilikuwa kubwa kuliko wayahudi wote.

Yusuph alikuwa na IQ kubwa kuliko Misri yote na miungu yao. Aliwahi kubuni mfumo wa kutunza nafaka miaka saba bila kuoza.

Ukiona mtu anasoma biblia alafu anakuwa zoba, au mjingamjinga, au uelewa wake wa kuungaunga ujue anasoma kidini sio kifalme. Biblia ni maneno ya Mungu mfalme mwenye IQ kubwa kuliko viumbe vyake, ukiisoma kifalme unaambukizwa IQ ya mwenye hayo maneno.

Ni hayo tu.

Mbarikiwe
 
Hapa unawamba ngoma mkuu, sishangai unapovutia kwako.
Watakuja waislamu nao watasema biblia ni chamtoto, Quran ndiyo mwisho wa mambo.
Kama wanadhani ni sahihi uwanja ni wao. Maana hata chenyewe kinawaambia wakina na mashaka waulize biblia. Vitabu kabla yake.

Mtume mwenyewe alianzia mambo yake kwa Waraqa Ibn Nauful mtaalam wa Biblia. Hapo ndipo alipoelekezewa mambo ya Huo utume. Hata waarabu walijua biblia ndio kila kitu.
 
Amina Mtumishi

MaranAtha-Bwana Wetu Yesu Kristo Anakuja
2563ed0283e0e926b2770f0dd8c49846.jpg


Sent from my A37fw using JamiiForums mobile app
 
Bangi mbaya sana.
Stori za kutunga za Biblia ni neno la Mungu?
Halafu Biblia zipo nyingi, sisi Orthodox Biblia yetu ninyi Wakatoliki na Lutheran mnaikubali?
Mimi naomba unikumbushe mahali ambapo aliyegundua hesabu za Algebra alikua anasoma Biblia.
 
Minadhani ingekuwa Hivi ,si kusoma bibilia tu bali na kuyashika maagizo yake ndio kunakuwa na impact kwa maisha ya muhusika sio tu kwa swala LA IQ bali hata afya,uchumi,elimu,mahusiano ,utunzaji wa mazingira,uongozi ,upendo kwa wengine, amani katika nchi na mengine mengi.
 
Back
Top Bottom