Biblia inavyosema juu ya kuinuka kwa Uislam

Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
2,301
3,411
Unabii huu unaupata kwenye kitabu Cha UFUNUO 9.

1 Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu.

2 Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni.

3 Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi.

4 Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, ila wale watu wasio na muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao.

Ufunuo wa Yohana 9:1-4
Hapa dini mpya inaoneshwa, ikiwa na baadhi ya mafundisho mazuri, NI NYOTA ILIYOANGUKA KUTOKA MBINGUNI, lakini ilikuwa imechanganyikana na MAFUNDISHO MACHAFU, moshi kutoka lile, "SHIMO LA KUZIMU"

Uislam ulianza kwa kulaani uovu wa ibada ya sanamu iliyokuwa inaendeshwa na kanisa la Roman Catholic, (NA HAPA ULIKUWA SAWA).

Kwa hakika kuna Mungu mmoja, na hakuna astahiliye kuabudiwa isipokuwa yeye. Lakini mafundisho ya Uislam yaliyokuwa yanahitajika kwa kanisa asi, YALILETA "MOSHI" KATIKA ULIMWENGU.

"SHIMO LA KUZIMU" katika kiyunani lina maana ya JANGWA au NYIKA yoyote iliyo ukiwa, na hivyo linafaa kabisa KUWAKILISHA JANGWA LA ARABUNI walikotokea wavamizi Waislam wa Kiarabu, KATIKA WINGI UNAOFANANA NA NZIGE.

Abyssos ni neno la Kiyunani linalomaanisha, "SHIMO LA KUZIMU"
na hilo ndilo linalotupatia neno la sasa la kiingereza, linalomaanisha KUZIMU. Waandishi wa kisasa wa Kiislam wanalitumia neno hilo kuielezea jamii ya Kiarabu alikotokea Muhammad:

ARABIA SHIMO LA GIZA.
Katika enzi hizo za ujinga uliokithiri, kulikuwa na eneo ambalo giza zito tena totoro lilikuwa limetuwama... ARABIA... Nalo lilikuwa pweke likiwa limetengwa na bahari kubwa sana ya mchanga. Wafanya biashara wa Kiarabu walikuwa wanasafiri mwendo mrefu kwa kujikokota wala hawakupata punje yoyote ya maarifa katika safari zao. Katika nchi yao hawakuwa na taasisi yoyote ya elimu wala maktaba. Hakuna aliyekuwa anaonekana kuwa na shauku ya kukuza ama kuendeleza elimu.

Fikra zao zilikuwa zimejaa miiko, akili na jadi yao ilikuwa ni unyama na ukatili mkubwa, maadili na ufahamu wao vilikuwa vya kishenzi na visivyo staha.

"...Hakukuwa na sheria isipokuwa ile ya ukatili. Uporaji, mashambulizi na mauaji ya watu dhaifu wasio na hatia ilikuwa ndio kawaida... Tukio lolote dogo lilikuwa linaweza kusababisha vita kulipuka kwa hasira za kikatili...
Dhana yoyote waliyokuwa nayo juu ya maadili, utamaduni, na ustaarabu vilikuwa vinaonekana vya kizamani na ushenzi... Walikuwa wakiabudu mawe, miti, sanamu, nyota na mizimu, na kiufupi walikuwa wanaabudu chochote walichokuwa wanakifikria isipokuwa MUNGU. (Rejea ABDUL A'LAMAUDUDI TOWARDS UNDERSTANDING ISLAM, UK. 41, 42, NAIROBI: THE ISLAMIC FOUNDATION, QUR'AN HOUSE 1973)

Siku moja mfalme Chosroes II wa Uajemi alipokea barua kutoka kwa raia mmoja wa Maka asiyefahamika, ikimtaka amtambue Muhammad kuwa ni nabii wa Mungu. Mfalme aliichana ile barua kwa dharau na akakataa madai ya nabii. Yeye hakujua kuwa, mapema, yeye mwenyewe ataangamia kabisa na ufalme wake pia kuangamizwa, NA KWAMBA NABII HUYU WA AJABU KUTOKA MAKA ANGETAWALA ULIMWENGU. Kuanguka kwa mfalme Chosroes kunafikriwa na wengine kuwa kulikuwa ndio, "UFUNGUO WA SHIMO LA KUZIMU", kwa sababu Muhammad asingeweza kuinuka katika kutawala isipokuwa kwa kuuangusha kwanza ufalme wa Waajemi.

NDIPO WAISLAM WA ZAMANI (SARACENS) KUTOKA UARABUNI, "WAKAPEWA NGUVU", NA KUONGEZEKA SANA MPAKA WAKAWA WENGI MNO KAMA NZIGE.

Bila ya kuwa na dhana ya kitabu cha Ufunuo akilini mwake, mwandishi mmoja alisema hivi juu ya hawa wafuasi wa Muhammad kuwa, " Wa-Osmanlis walisongamana kama NZIGE pande zote, na hakuna kijiji ambacho hakikuwafahamu, mpaka hata kuta za Constantinople". Kama vile nge anavyogonga, ndivyo walivyolipiza kisasi kwa ukatili katika vita.

Muhammad alipokufa, alirithiwa na Abubakari katika mwaka wa 632 B.K, ambaye aliwakusanya makabila ya kiarabu ili kufanya vita. Aliwaamuru wafuasi wake kuheshimu imani za watu wale waliokuwa wanazishika kwa uaminifu amri za Mungu. Ilikuwa inawapasa watu wake kuwaadhibu wale tu waliokuwa wanaabudu sanamu.

Akiwaamuru askari wake: "MSIUCHAFUE USHINDI WENU KWA DAMU ZA WANAWAKE NA AU WATOTO. MSIHARIBU MITENDE, WALA KUCHOMA MASHAMBA YO YOTE YA NAFAKA. MSIKATE MITI YO YOTE YA MATUNDA, WALA KUFANYA UHARIBIFU JUU YA MIFUGO, ISIPOKUWA WALE MTAKAOWAUA KWA CHAKULA.

Kadiri mtakavyoendelea mtawakuta baadhi ya watawa ambao wamejitenga na kuishi katika nyumba za watawa, wakiazimia wenyewe kumtumikia Mungu hivyo, MSIWASUMBUE NA WALA MSIWAUE WALA KUANGAMIZA MAKAZI YAO, na mtakuta aina ya watu wengine walio wa sinagogi la shetani, walionyoa utosi wao, hakikisheni mnapasua vichwa vyao, na msiwape nafasi mpaka ama wamegeuka kuwa Waislam au walipe " ushuru".

Ni watu gani waliokuwa na muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao ambao askari wa Abubakari waliamuriwa kuwaacha?

Katika siku za Muhammad na Abubakari kulikuwa na waaminifu kama hao. Inaonekana kuwa mwenye mamlaka kuu kuliko Muhammad watu wake waaminifu walindwe! Waarabu walitumia mno Farasi katika vita vyao. Na "TAJI" inaweza kuwa kilemba, ambacho kwa muda mrefu kilikuwa ni kilemba cha taifa la Waarabu.
Askari walikuwa na nywele ndefu.

Mafungu 5-11
5 Wakapewa amri kwamba wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao yalikuwa kama kuumwa na nge, aumapo mwanadamu.

6 Na siku zile wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe. Nao watatamani kufa, nayo mauti itawakimbia.

7 Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu.

8 Nao walikuwa na nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya simba.

9 Nao walikuwa na dirii kifuani kama dirii za chuma. Na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya magari, ya farasi wengi waendao kasi vitani.

10 Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.

11 Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.

Ufunuo wa Yohana 9 :5-11

Hapa tunalo jaribio juu ya usahihi wa unabii na kutimilika kwake kihistoria.

KATIKA UNABII WA BIBLIA SIKU MOJA NI MFANO WA MWAKA MMOJA, (Tazama maelezo ya sura 2:10). Kuna siku 30 katika mwezi wa unabii wa Biblia (linganisha mwanzo 7:11, 8:4 na 7:24 na pia linganisha miezi 42 ya Ufunuo 11:2 na siku 1260 za 11:3 na 12:6). Hivyo "MIEZI MITANO" ya kipindi cha unabii ni sawasawa na miaka 150.

Waislam hawa wa zamani, (SARACENS) "WALIPEWA AMRI", kuutesa " UTAWALA WA KIRUMI WA MASHARIKI KWA MIAKA HII 150, lakini siyo "KUWAUA", yaani siyo KUWASHINDA. Miaka 150 inapasa kuanzia wakati ule, " WATAKAPOKUWA NA MFALME WAO".

Kitabu cha Mithali kinasema, "NZIGE HAWANA MFALME, LAKINI HUENDA WOTE PAMOJA VIKOSI VIKOSI"
Mithali 30:27

Lakini, "NZIGE" wa Waislam, wavamizi walipangwa vizuri sana katika kazi ya kuangamiza, maana walikuwa na mtawala waliyekuwa wanafuata amri zake. Kwa mamia ya miaka baada ya kifo cha Muhammad, wafuasi wake waligawanyika katika makundi mbalimbali hasimu bila ya utawala wowote au mfalme. Lakini karibu na mwisho wa karne ya 13, Othman alianzisha na kuimarisha serikali iliyokuwa inajulikana kama ufalme wa Ottoman (Ufalme wa Kituruki).

"MALAIKA WA SHIMO LA KUZIMU" anaitwa "MALAIKA" katika fasili ya neno la kiyunani ambalo pia linamaanisha "MJUMBE" au "MHUDUMU". Sultani akawa mkuu wa dini ya Kiislam. Jina kwa Kiebrania "ABADONI", na kwa Kiyunani "APOLIONI" lina maana ya "YEYE AANGAMIZAYE". Hivyo ndivyo ilivyokuwa tabia ya watawala wa Kituruki (Ottoman).

Tunajiuliza ni lini Othman, kama mfalme wa kwanza wa Waislam alipofanya mashambulizi yake ya kwanza, "KUUTESA" ulimwengu wa kiistarabu wa Ufalme wa Mashariki?

Edward Gibbon, mtu ambaye aliandika historia lakini hakuamini katika Biblia, ametuachia tarehe ya usahihi zaidi kuwa Julai 27, 1299, ndiyo Othman alifanya mashambulizi yake ya kwanza juu ya Nicomedia.

Gibbon anasema kuwa, "USAHIHI" wa ajabu unaonekana kudhihirisha njozi fulani ya mbio na ukuzi wa uharibifu wa ubwana (Ufalme wa Kituruki).

Tunauliza tena. Je Waturuki "walitesa" ufalme wa Rumi wa Mashariki kwa miaka 150? Ndiyo, historia inatuambia kuwa waliendeleza vita kuusumbua na kuutes ufalme huo tangu mwaka 1299 mpaka 1449 kwa miaka 150 kamili bila kuuteka kabisa. Halafu badiliko kuu lilitokea. Wafalme wa Rumi ya Mashariki waliendelea kudhoofika na kuwa wapotovu zaidi mpaka ikawa dhahiri kwa kila mtu kwamba muda kitambo wangepoteza uhuru wao.

Wakati mfalme Yohana alipofariki taehe 31 Oktoba, 1448, ndugu zake kwa unyenyekevu, ndugu zake waliomba idhini kwa Sultani wa Uturuki, Murad II, ili kumchagua ndugu yao mkubwa kutawazwa kama mfalme mpya katika mwezi Januari, 1449. Hivyo kwa kumnyenyekea Sultani wa Uturuki, walikiri kuwa uhuru wao ulikuwa umefikia mwisho. Kumbuka kuwa maelezo haya ni ya maana na yaliyo wazi kabisa.

Mafungu 12-15
12 Ole wa kwanza umekwisha pita. Tazama, bado ziko ole mbili, zinakuja baadaye.

13 Malaika wa sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyo mbele za Mungu,

14 ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue nao malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati.

15 Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu.

Ufunuo wa Yohana 9 :12-15
Ule "OLE WA KWANZA" ilikuwa ni kuinuka kwa nguvu ya Uislam. Baadaye ilikuwa ufuate "OLE WA PILI", na kuwa taabu kuu katika Ulaya. (Sura 11:14). Na "OLE WA TATU" ulikuwa uwe hasira ya kuogofya ya mataifa, pamoja na ghadhabu ya hukumu ya Mungu, itayoleta mwisho wa historia ya ulimwengu wetu (sura ya 11:18).

Katika mwaka 1449, "MALAIKA WA SITA" alifungulia kizuizi kilichokuwa kimewazuia Waislam kuuteka ufalme wa mashariki uliokuwa wenye utajiri na nguvu. Wale "MALAIKA WANNE WALIOFUNGWA KWENYE MTO MKUBWA FRATI" NI KIELELEZO KINACHOTAJA MAJIMBO MANNE TOFAUTI YA WAISLAMU YA ALEPPO, IKONIO, DAMESKI, NA BAGHDAD.

Na hivyo njia ilifunguliwa kwa Sultani ili baadaye aendeshe vita vya ushindi dhidi ya Ulaya. Mji wa Constantinople (sasa Istanbul) ulitekwa na majeshi ya Uturuki katika mwaka 1453.

Lakini zingatia hili: Miaka 150 ilipotimia katika mwaka 1449, uhuru wa mfalme wa Ulaya ulipotezwa siyo kwa mapigano, bali kwa mfalme kuusalimisha kwa hiari uhuru wao mikononi mwa Waturuki. Maana yake alisema. "SIWEZI KUTAWALA MPAKA KWANZA MRUHUSU". Kumbuka kwamba, kadiri tunavyosonga mbele, karibu utaona jambo muhimu mno.

Je ni kwa muda gani ufalme wa Waturuki Waislam ungeendelea kutawala kwa uhuru?

"Mwaka" mmoja wa siku 360 ni miaka halisi 360

Mwezi mmoja wa siku 30 ni miaka 30

Siku moja ya saa 24 ni mwaka 1

Saa 1/24 ya mwaka X 360 ni sawa na siku halisi 15

Jumla tutapata miaka 391 na siku 15

Ni lini hiki kipindi cha miaka 391 na siku 15 kilipoanza?

Ni dhahiri kuwa ni baada ya mwisho wa miaka 150 Waislam walipokoma "KUTESA" ufalme wa Mashariki maana waliutwaa. Baada ya kuongeza hiyo miaka 150 katika tarehe yetu ya kuanzia ya Julai 27, 1299, ni wazi kuwa tutafikia julai 27, 1499. Halafu ikiwa tutaongeza miaka 391 katika julai 27, 1499 tunafikia julai 27, 1840 Kisha ni lazima tuongeze siku nyingine 15.

Tunapata nini kama jibu kamili na la mwisho? Julai 27 ukiongeza siku 15 inapatikana Agost 11, 1840.

Je, Sultani wa Uturuki alipoteza Uhuru wake katika siku hiyo hasa kwa kujisalimisha kwa unyenyekevu na kwa hiari yake kwa watawala wa Ulaya kwa namna ile ile mfalme wa Rumi Mashariki alivyopoteza uhuru wake kwa Sultani mwaka 1449? Tutaona baadaye.

Ikiwa historia itasema ndiyo kwa swali hilo, tutakuwa na ushahidi wa hakika na kustaajabisha kwa mambo mawili:
Kwanza, kwamba utaratibu wa mwaka kwa siku wa kufasili unabii wa Biblia ni sahihi kabisa, na pili, kwamba kidole cha kuogofya cha Mungu kinaelekeza kwa jambo fulani pana na lenye maana kuliko kujifunza juu ya kuinuka na kuanguka kwa falme:

Kitabu cha Ufunuo ndio ufunguo Mungu aliotupatia kufungulia siri ya hukumu yake juu ya ulimwengu wetu wa siku hizi ulio mkaidi.

Pale msomaji asiyejali anapokuwa haoni kitu bali tu jangwa lisilofaa, katika kitabu cha Ufunuo sisi tunapata utajiri uliofichwa na wenye maana kubwa mno kwa watu wa Mungu. Kitambo kidogo tutaona ni nini historia inasema kilichotokea siku ya Agosti 11, 1840.

Kwanza, hebu na tuangalie kwa muda tu vipi Yohana anaelezea namna majeshi ya Kiislamu ya Uturuki yalivyowahi kutia hofu mataifa ya Ulaya kwa karne nyingi:

*Linganisha Maandiko Matakatifu yanavyouhesabu wakati katika UFUNUO 13:5, 12:6,14. Ni dhahiri kuwa "mwaka" wa Biblia ni siku 360 na "mwezi" wa Biblia ni siku 30.

Mafungu 16-19

16 Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi; nilisikia hesabu yao.

17 Hiyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti.

18 Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao.

19 Kwa maana nguvu za hao farasi ni katika vinywa vyao, na katika mikia yao; maana mikia yao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, nao wanadhuru kwa hivyo.

Ufunuo wa Yohana 9:16-19

HAPA KUNATAJWA MATUMIZI YA BARUTI KWA MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA YA MWANADAMU.

Kwa Yohana, ambaye kwa kweli hakuwahi kuona bunduki au baruti, mashujaa wa Kiislam wakiwa wamepanda farasi wakipiga bunduki zao wataonekana katika upeo wa macho yake kana kwamba, "KATIKA VINYWA VYAO HUTOKA MOTO NA MOSHI NA KIBERITI"

Mpaka mwaka 1453 B.K. kuta za mji wa Constantinople zilikuwa zimestahimili mashambulizi ya majeshi mengi, na hivyo ufalme ulikuwa umeokoka na hatari. Lakini sasa Waturuki wa Ottoman wakatumia kwa mara ya kwanza mizinga mipya na mikubwa pamoja na baruti katika kubomoa zile kuta zilizokuwa hapo awali haziingiliki. Kutumiwa kwa baruti na mizinga kulimaliza ulinzi wa mwisho wa jeuri ya ufalme wa zamani wa Warumi. Ubinafsi na ubadhirifu ulikuwa umeangamiza ustaarabu wa zamani.

Lakini sasa katika mwaka 1840, ubinafsi na ubadhirifu ulikuwa umepoozesha jeuri ya utawala wa Kiislam katika mwaka 1838, vita vikali vililipuka kati ya masultani wa Uturuki na Misri, Misri ikiwa mshindi.

Katika mwaka 1840, mataifa yenye nguvu manne ya Ulaya yaliingilia kati kwa kuhofia kwamba Misri ingeweza kwa muda mfupi kuchukua kiti cha enzi cha Sultani wa Uturuki katika kuhangaika kwake. Sultani ambaye alikuwa amedhoofishwa kwa hiari ALISALIMISHA UHURU WAKE MIKONONI MWA HAYA MATAIFA MANNE YA ULAYA, akiwaachia kumwendeshea mambo yake. Alimtuma mjumbe wake kwenda kwa mtawala wa Misri kutoa ujumbe kutoka kwa Mataifa manne ya Ulaya, ujumbe ulioweka mikononi mwao mambo yake.

Ilikuwa ni Agosti 11, 1840, ndiyo huyo mjumbe alipowasili Alexandria, na siku hiyo alikabidhi ujumbe mikononi mwa mtawala wa Misri.

Katika siku hiyo, uhuru wa Sultani ulikuwa wapi? ULIKUWA UMETOWEKA! Na "tangu siku hiyo. Uturuki ya Kiislamu imebakia tu kwa ruhusa na kutegemea kuungwa mkono na mataifa ya Ulaya".

Jambo hili lilipofahamika kwa umati wa wapenda Biblia walisadiki usahihi wa kanuni ya mwaka kwa siku ya kufasili unabii wa Biblia. Kilichoonekana kuwa si jambo la muhimu kihistoria kilitoa kwa dhati ushahidi wa kuridhisha kuwa vitabu vya Danieli na Ufunuo viliandikwa kwa uongozi wa Mungu, na vinatoa ujumbe muhimu sana kwa wakazi wa dunia ya sasa.

Wanazuoni na watafiti wa leo wanaweza kutofautiana katika kuhesabu wakati kipindi hiki cha miaka 391 kilipoanza na kumalizika. Jambo la kushangaza ni kwamba matukio makuu ya historia ndefu ya himaya ya Ottoman yanasimuliwa kwa usahihi kabla hayajatukia katika unabii. Kama tulivyoona katika Danieli mwitikio wa historia ni kama jiwe lililovunjwa linaloweza kurudishwa lilivyokuwa. Wapagani wengi waliongoka miaka ya 1840 kwa kushuhudia kutimizwa kwa unabii unaofuata kanuni ya MWAKA-SIKU na imani watu mamilioni wasiojulikana wamekuwa wakitiwa nguvu na unabii huu. Kwa hakika ndiye BWANA aliyekuwa ameutoa.

Mafungu 20, 21

20 Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda.

21 Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao.

Ufunuo wa Yohana 9:20-21

Ingawa makundi ya Waislamu yaliachwa huru juu ya ulimwengu wa Kikristo ulioasi, watu walikataa kujifunza somo la toba. Kwa hiyo tunaona kuwa Mungu huwa anaruhusu, "OLE" kuujia ulimwengu ili kuwafanya wenye dhambi kuzinduka, na kuwaongoza kuiendea toba. Ole baada ya ole zilifuatana, lakini bado wanadamu walikuwa wanazipenda dhambi zao. Je, "OLE WA TATU" utawaongoza kwenye toba? Wakati ule utakapofika, watakuwa wamechelewa mno!

Mpendwa unayesoma, Je, utajitoa moyo wako kwa toba leo?

*MSOMAJI AMBAYE ANGEPENDA KUONA DONDOO KUTOKA KWA MAGAZETI YA AGOSTI NA SEPTEMBA, 1840, YAKITOA MAELEZO KAMILI JUU YA MATUKIO YA AGOSTI 11, 1840, ANAWEZA KUANGALIA KATIKA KITABU CHA, "DANIEL AND THE REVELATION", KILICHOANDIKWA NA URIAH SMITH, KURASA 513-516.

MUNGU AWABARIKI
 
Samahani , Unaweza Muelezea OLE WA TATU atakayo yafanya juu ya Dunia ?
 
Samahani , Je hicho kitabu kilichoandikwa na Smith juu ya Ufunuo na Daniel je kipo cha kiswahili ?
 
Back
Top Bottom