HelcopterChopa
Member
- Sep 13, 2023
- 35
- 46
Ushindi mkubwa wa kishindo walioupata CCM katika jimbo la mabara-Jijini Mbeya, ni ishara njema ya kukubalika, kuimarika na kuaminika kwa chama cha mapinduzi kwa wananchi na uhakika wa kushinda chaguzi zijazo.
Lakini pia uchaguzi huo ni fursa muhimu zaidi kwa upinzani kujipima, kujitathimini, kujipanga na kubuni na kuibua mbinu na mikakati kabambe dhidi ya CCM inayoimarika kila uchwao na kuikabili vilivyo tena kisayansi na kwa sera madhubuti za kuwavutia na kuwashawishi wanachama wengi zaidi hususani vijana ili hatimae kuibuka na kura nyingi zaidi na kushinda mitaa mingi zaidi, Kata nyingi zaidi, majimbo mengi zaidi na Inshaalah Urais katika chaguzi zijazo.
Niwapongeze sana wote walioshiriki uchaguzi huo muhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya jimbo la Mbarali.
Niwapongeze mno waliopata ushindi, na ambao hawakupata ushindi kwa ungwana na ustaarabu wa kiwango kukubali matokeo. Hakika asie kubali kushindwa huyo si mshindani.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Bariki Demokrasia Tanzania.