Mbunge Bahati Ndingo Aishukuru Kamati Kuu ya CCM Taifa kwa Kumteua Kuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Mbarali

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

BAHATI NDINGO AISHUKURU KAMATI KUU YA CCM TAIFA KWA KUMTEUA KUWA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBARALI

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mhe. Bahati Ndingo ameishukuru Kamati Kuu ya CCM Taifa kwa kumteua kuwa Mgombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Mbarali ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika tarehe 19 Septemba, 2023.

Itakumbukwa kuwa, Mhe. Bahati Ndingo kabla ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya CCM Taifa alikuwa na mpaka sasa ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya alipochaguliwa katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Mwaka 2020.

"Ninapenda kuishukuru Kamati Kuu ikiingozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuniteua kuwa mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Mbarali, Mkoani Mbeya kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge uliopangwa kufanyika tarehe 19 Septemba, 2023" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya

"Ni heshima kubwa sana kuona imani yenu kwangu kwa kuchaguliwa kupitia wapiga kura wa maoni ambao ni wanachama wa CCM. Nawashukuru kwa kunipa fursa hii muhimu ya kuwakilisha na kujitolea kwaajili ya Maendeleo ya wananchi wetu" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya

"Natambua jukumu hili ni kubwa na nipo tayari kukiwakilisha Chama na Ilani yake katika uchaguzi huo mdogo ufuatao. Asanteni tena kwa imani yenu. Kazi Iendelee, CCM Imara" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-08-18 at 18.41.52.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-18 at 18.41.52.jpeg
    113.7 KB · Views: 5
Tunashukuru tunaongeza mzigo mwingine wa kuhudumia usioweza kuleta impact katika nchi.

akaungane na wale wapiga makofi wenzake tu
 
Back
Top Bottom