Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,545
- 2,175
Kazi inaendelea vizuri,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Mbarali kufuatia kifo cha Mbunge Marehemu Francis Mtega (CCM) pamoja na Kata 6 za Tanzania Bara utakaofanyika kesho tarehe 19 Septemba mwaka 2023.
Kwa mujibu wa NEC kata zitakazofanya uchaguzi mdogo hiyo kesho ni; Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, mkoani Dodoma, Mwaniko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, Old Moshi Magharibi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi na Marangu Kitowo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Mtyangimbole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na Mfaranyaki iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma.
Pia, Kwamujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi huo Bw Misana Kwangura Wagombea walioteliwa na vyama vyao ni 13 ambao ni Halima Abdalah Magambo (AAFP), Osward Joseph Mndeva (DP), Zavely Raurent Seleleka (UDP), Exavery Town Mwataga (CCK), Morris Thomas Nkongolo (TLP) na Modestus Dickson Kilufi (ACT Wazalendo).
Wengine ni Mary Moses Daudi (UPDP), Fatuma Rashidi Ligania (NLD), Bahati Keneth Ndingo (CCM), Bariki Oswald Mwanyalu (Demokrasia Makini), Hashim Abasi Mdemu (ADC), Mwajuma Noty Mirambo (UMD), na Husseni Hasani Lusewa kutoka Chama cha ADA- TADEA.
Chama cha Mapinduzi CCM kitahitimisha kampeni zake hii leo Katika Viwanja vya Stendi Mpya kata ya Chimala chini ya Makamu Mwenyekiti wake Crde Kanali Mstaafu AbdulRahman Kinana,
Kinana aliyepiga kambi Mbarali ili kuhakikisha CCM inapata ushindi mnono katika mikutano yake mbalimbali amewataka Wananchi wa Mbarali wasipoteze kura zao bali wampigie Mgombea wa CCM Crde Bahati Kenneth Ngingo mwanamama mzuri wa sura na vitendo ili akashirikiane na mwanamama mwenzake Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ili kuifanya Mbarali kuzidi kuwa kitovu cha uzalishaji na usamabazaji wa Mchele Tanzania.
Upinza mkali ni kati ya CCM na chama kikuu cha Upinzani nchini cha ACT-Wazalendo.
Stay tuned,