Ushauri wenu, dunia naona mviringo!

uimalizie basi nkamu. Unatupa arosto
 
PART IV
Bibie Clara akajifungua mtoto mzuri wa kike baada ya miezi yake tisa kupita.
Muda wa msiba ulipita na hapo ikawa ajira yake alipokuwepo haipo.
Na utegemezi wake ikawa mimi.
Nami kwa kuiona umuhimu ikabidi nijitahidi kumsaidia kila hali, ili ayamudu maisha.

Lakini nikikaa peke yangu na kufikiria nikawa nawaza.
Nimemla huyu Clara kiduchu tu, na nimebeba majukumu yote ya mume.
Nimefikaje hapo?
Pamoja na uzuri wake, udogo wake kiumri, lakini kesha badili punda na sasa mimi ndio mume na nina mtoto naye.
Hata hivyo kwa kuajibika kiubinadamu tu, siwezi kumwacha sasa hivi, kwani yeye hakupanga kuugua mumewe.
Lakini muda wotehuo moyoni alijua mumewe ndo anaishia, hivyo akashikilia unyasi uliokuwepo, unyasi uliojileta wenyewe kwa kumtongoza.

Hata hivyo mimi nilikuwa na furaha moyoni, furaha ya mtoto.
Kwa mke wangu nyumbani nilikuwa na wavulana watatu, sasa nimepata kajike.
Nililiwazika moyoni, na hili lilinipa uwezo wa kuyakubali majukumu.

Hata hivyo huu ukawa mwanzo wa matatizo yangu ya muda mrefu.

Mtoto aliendelea kukua na nilipomwona baada ya miezi mitatu kupita nilifurahi sana.
Kwa kweli nilifanana naye kwa vitu vingi, nywele, macho, pua na meno yalivyojipanga na hata mdomo.
Na baada ya mwaka kupita ,hata rangi ya ngozi.

Clara mara nyingi akisema nina damu kali sana, kwani mtoto tumefanana.

Baada ya muda wa miaka miwili, kule bibie alikokuwa anafanyia kazi biashara ikayumba na kufungwa.
Hivyo akaniomba mtaji afungue ka Secretarial.
Nikamkubalia maana sasamahitaji yake niliyokuwa natuma kila mwezi yalikuwa makubwa, sasa inabidi aanze kujikimu kwa kiasi.

Biashara yake ikawa nzuri na kukua, nami safari za kwenda huko mkoani "kulea" zilikuwa haziishi.
Ghafla bibie akaanza kuugua tumbo la uzazi lililotokana na operation ya kujifungua.
Tatizo lilianza taratibu, na baada ya miaka mitatu au minne Clara alikuwa hata kukaa chini hawezi.
Madaktari walimwambia afanyiwe upasuaji mwingine, kuna mambo hayajakaa sawa tumboni.

Akafanyiwa upasuaji, na hapo ndio nikaonana na mama mkwe hospitali.
Niligharimia fedha zote za matibabu.
Mama mkwe alinitazama kwa makini tukisalimiana.
Mwisho nikajua tu, amenikubali maana mwanaye alikwisha muambia ninavyomhudumia.

Bibie alipona na kurudi kwenye biashara yake ambayo iliendelea kushamiri, na akaomba nimnunulie jenereta kutokana na kukatika katika umeme, nikamnunulia.
Na mtoto sasa akaanza nursery na
baada ya miaka miwili akaanza la kwanza, na sasa mkubwa.

Mahitaji ya bibie Clara yaliendelea kuwa makubwa, licha ya biashara yake kushamiri.
Bibie alinenepa na akawa mzuri zaidi, nami nikaendelea kujilia vitu taratibu, sasa nikimpa nauli aje Dar.
Hatimaye akaniomba nimnunulie gari dogo maana alisema anabanwa banwa sana kwenye usafiri wa umma.
Nami nikamkubalia, kwa wivu nilitaka niwe nambana mimi tu.
Maisha yakaendelea.
Ndugu zake wengi walitaka tufahamiane, mi nikakataa nilimwamnia Clara mradi nafahamiana na mama, inatosha!

Huku nyuma yangu mtoto kanawiri, na kwa kweli akivaa na kuonekana hadharani anapendeza.
Mijamaa ikaanza kumezea mate hukohuko mkoani.

Mimi sina hili wala lile, nina nyumba ndogi, sijaioa hivyo nikahisi huko naliwa vitu vyangu.

Nami nikaanza tena safari za kumtembelea huko mkoani.
Uhusiano haukuwa motomoto tena.
Nikawaza sana, nikajua ana mtu anamchukua.

Baada ya kwenda mara tatu mkoani na kuona kiwango cha penzi kikizidi kushuka ikabidi nimuulize tu kuwa kuna nini, umepata mfadhili mwingine?

Naye akashukuru kupata upenyo wa kuniambia.
Akaniambia kuwa anataka kuolewa.
Anaye jamaa wana uhusiano na wamepanga kuoana.
Ameshawaeleza ndugu zake na mipango imeshaanza ya ndoa.

Nilipigwa butwa, kama teke ni la tumbo basi lilikuwa hilo.

Nikamuuliza kama kweli alikuwa na uthubutu wa kunifanyia hivyo.
Akanijibu kuwa wajomba zake wameamua kuwa hawezi kuendelea kama alivyo, lazima aoelewe.
Iliniuma sana, nikamuuliza na mama kama yumo kwenye maamuzi hayo.
Akanijibu ndivyo familia ilivyokubaliana.
Nilisikitika, nikasononeka, lakini faraja pekee ni kuwa nina mtoto wangu.
Nikarudi Dar kwa majonzi ya kupokwa penzi.
Bibie nilimwinua toka hana kitu na hajulikani, sasa yuko matawi, kanipiga kibuti.
Nikakubaliana na hali, na nikajiambia kuwa yote ni yeye mwenyewe Clara, angeamua kubaki nami ni yeye.
Kaamua kuingiauhusiano mwingine ni maamuzi yake, si ya wajomba wala mama.

Nilikula vya watu, nikavifanya vya kwangu, nami vyangu vinaliwa na kuchukuliwa jumla.
Na bibie alikuwa mzuri kweli kweli, kachanua.
Ili nisiumie moyoni nikakubaliana na hali, nikakubali kuwa penzi langu na Clara limeishiwa vocha, na mimi inabidi nitembee.
Nikatembea
Itaendelea PART V
 
🙄🙄 sasa ulitaka uendelee tu kumega kisela hadi aote mvi wakati we una mke wako???...... ngoja nipunguze mdomo kwanza, leta vitu tuko pamoja baby ake Clara
 
Yaani wewe dada ndo unajua.
Wanaume wengi hawajui kuwa kimaisha wanawake huwa wanafikiria mbali zaidi na kupima mambo mengi zaidi.
Na ndiyo essence ya hii stori.
Mkuu......naomba nisaidie maana ya neno #. ESSENCE.,........hapa Nmepewa assignment ina msamiati huo
 
Usisahau kunitg part 5
 
Mkuu......naomba nisaidie maana ya neno #. ESSENCE.,........hapa Nmepewa assignment ina msamiati huo
Mkuu hapo neno essence nimelitumia kama jumuisho au mantiki ya hadithi nzima.
 
Maana yake halisi ni ipi
essence
n
1. the most important and distinctive feature of something, which determines its identity
2. a concentrated liquid used to flavour food
3. in essence essentially
4. of the essence vitally important
etymology Latin esse to be

Ref: Dictionary
 
Shukrani mkuu lkn



Usisahau kuleta mwendelezo
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…