Ushauri wenu, dunia naona mviringo!

Ushauri wenu, dunia naona mviringo!

Heri wewe dunia unaona mviringo na hivyo ndivyo ilivyo,sisi je tunaoiona pembe tatu tusemeje..?

Ukimla tu huyo mke wa mtu basi utaona dunia inavyokubadilikia na kuwa mstatiri wenye mizingo na vipenyo vimvuli!.
Kweli dunia mviringo.
Jamaa kaanza na muke ya mutu, kamuokoa maisha, huyo bibi bado muke ya mutu.
Muke ana matatizo.
Lakini jamaa aingie mitini.
 
kiufupi umepigwa........

yaani umetumika unatumika na utatumika kutimiza malengo ya mcheps ........

hapo bado mkeo hajajua....

pole sana....
 
ushauriwe nini?

wewe ni reserve wa clara

anajua udhaifu wako ni utupu wake na anaendelea kukutumia kwa faida zake

umeamua kutumika

endelea tu!!!!!!
PART V
Wana MMU, haka kastori ni ka mtiririko wa miaka mingi.
Na nakaleta ili walimwengu muone mwanaume anavyoweza kuwa mjinga kwa penzi.
Mwanamke anakufunga kamba kwa kukupa uroda unaoweza kukupumbaza, wewe ukawa unampenda lakini yeye anakupenda just enough kupata kile anachokipata kwako.
Kama amekuchoka au ndo unaelekea down, kuna wanawake ni wajanja sana ku jump a sinking ship na kudandia nyingine.

Kitendo cha Clara kuolewa kilinikera haswa.
Lakini kabla hajaolewa niliongea naye kinaga ubaga.
Nilimwambia wewe Clara nilikutongoza ukiwa huna hili wala lile huko mkoani, ila ulichokuwa nacho ni ule uzuri wako natural ulioufunika katika nguo zisizo na hadhi.

Nikakuanzishia biashara, nikakununulia gari, umenona umependeza sasa unaniacha.
Nilimwambia mimi simjui na sitaki kumjua anayetaka kukuoa, ila ujue amekuona baada ya mimi kukuibua.
Na vile vile kwa wewe mwanamke nimekuinua sana kimaisha, kwa vile nakupenda.
Nikaendelea kumwambia kuwa nitaendelea kumpa support kwa elimu ya mtoto wangu.
Ila nikamsisitizia, ili nisiumie moyo sitamsumbua kwa lolote.
Na nikamwambia kumtakia heri, hata ndoa yake nitachangia, na nilifanya hivyo.

Maneno yalikuwa ni mazito na hata Clara alikuwa na masikitiko, ila hakuweza kujibu lolote la maana bali kusema wajomba ndivyo walivyo amua.
Clara alikuwa na mama yake tu, baba yake alifariki kitambo.

Tukaachana, na mimi nikaendelea na hamsini zangu.
Clara alioana na kijana mwenziwe na mimi wala sikutaka kwenda harusini licha ya kualikwa.
Niliona ndoa yao kwenye Facebook, wenyewe wakiwa na furaha tele.

Baada ya ndoa alinitumia ujumbe kuwa wanahamia Dar, lakini nikaona hayanihusu.

Mimi nikaendelea kufukuzia shilingi katika mishe mishe zangu jijini na kimsingi mambo yangu Alhamdulillahi yalianza kuwa poa.
Mimi kubadili fashion ya gari ilikuwa kama kawa, na kwa kweli nilimshukuru Mungu.
Ikapita zaidi ya mwaka na nusu, mie sina hili wala lile, mara nikapata simu, namba siifahamu.
Nikatuma ujumbe wa sms kuwa atume ujumbe, niko mkutanoni.

Ikapita saa nzima simu ile ikaita tena, nikaona hebu niipokee.

Ikaanza"mwanangu hujambo"
Nikamjibu "sijambo mama shikamoo , ninani anaongea?"

Akanijibu "mimi mama yako, mama yake Clara"
Nikaitazama simu na kushangaa!
Nikamuuliza kama ni wazima wa afya pamoja na mtoto wangu.
Akanijibu kuwa ni wazima, ila Clara alikuwa anaumwa tumbo lake lile alilofanyiwa operation.
Nikataka ampe pole Clara na kumtakia apone haraka.

Hapo ndipo mama Clara akafunguka.
"Mwanangu mimi mama yako nakuomba radhi kwa yote. Uniwie radhi sana, Clara ana matatizo makubwa na nisipokuarifu ili utusaidie tutampoteza. Uniwie radhi mwanangu hatukuelewa.
Mimi naongea na wewe ndugu zangu hawafahamu, naomba baba, naomba utusaidie"
Nikamwuliza mama sasa itakuwaje mimi kumhudumia mke wa mtu, na mumewe yupo.

Mama akasema yule kijana hana uwezo wowote, na ugonjwa wa Clara unahitaji specialist wa magonjwa ya wanawake, na kuwa hivi tunavyoongea kalazwa, na wako pamoja hospitali moja binafsi.

Duh...nikapigwa mkanganyiko.
Clara hatujaonana zaidi ya mwaka na ushee!
Sasa napata simu toka kwa mama yake!
Lakini nikasema nitaenda kumwona.
Nilipoingia chumba alimolazwa nilimkuta binti ambaye alitoka nje ,na mama Clara yeye kakaa pembeni .
Nikamsalimia mama na nikaenda kitanda alipo Clara.
Nikambusu shavuni, kwa upande nilimwona mama anainama huku akitabasamu.
Clara alifurahi ila uso ulikuwa na hali ya kuonyesha maumivu.
Nikaomba bili ya matibabu na nikawapa fedha zote.
Haraka haraka nikamwambia mama siwezi kukaa zaidi hapo maana nisijeshikwa ugoni!
Mama ajacheka akasema nisijali sana.
Nikaondoka.

Clara alikuja toka hospitali ila hakupona.
Tumbo liliendelea kumsumbua.
Sasa alipungua mwili akawa kama ufito.

Ilibidi kuwaona madktari bingwa ambao walisema tatizo kubwa ni ile operation ya kujifungua na operation iliyofuatia.
Madaktari waliomfanyua upasuaji hawakuwa na ujuzi wa kutosha.
Hata hizi operation zilizofanyika karibuni hazikuwa nzuri.
Hivyo wakashauri apelekwe India.
Kizungumkuti ni kwamba mume wake Clara hana kitu na familia yake nayo ni ya watu wa kawaida sana.

Nikabeba tena majukumu, Clara nikamgharimia akaenda India ambako alifanyiwa upasuaji tena.
Madaktari India walimwambia watafanya operation hiyo katika stage mbili. Mara ya kwanza walifanya operation nzito na wakamwambia inabidi apumzike miezi mitatu halafu arudi tena wammalizie operation ya mwisho.

Ikawa hivyo, na ndio kupona kwa Clara.

Tatizo nimemtibu mke wa mtu, lakini ni mama wa mtoto wangu.

Mwisho wa yote, alipopona sasa Clara nikasema kwa nini nisijaribu mitambo!
Na kwa kweli tukaitesti, tukarudi tulikokuwa zamani, lakini mimi bado mwizi!
Penzi likawa moto sana sana, mpaka bibie sasa akaniambia anataka mtoto mwingine!

Walimwengu niishie hapo.
Ushauri wenu tafadhali.
 
Dah....we bro nashukuru kwa kunielewa.

Nakuelewa ndio maana nakuomba ufanye maamuzi magumu sasa hivi.

Kuna hatari mbili kama sio tatu zinakukabili usipokua makini...

1. Mikosi kwa kumdhulumu huyo mme wa Clara, hii inawezekana ikapelekea biashara zikayumba na kujiletea madhsra yasiyoelezeka. Kumbuka mambo kukuendea vizuri ni neema na baraka, kwa kuwa umeshatenda wema kwa huyo binti, itoshe kuendelea na kulea mtoto, mtunze kama mzazi.

2. Hatari nyingine, najua utacheka na kuona masihara. Unaweza kujikuta unamuoa huyo Clara ndio anakuwa mke wako. Usiniulize mkeo wa sasa ataenda wapi. Na utaona kama jambo la kawaida tu kuoana na Clara.

3. Kuvunjiwa heshima na kupelekea kumpoteza mkeo wa sasa, hiyo itaambatana na mambo yako mengi kuyumba.
Hii ni kama inakua combination ya namba 1 na namba 2.

Tatizo la haya mambo, kadri unavyodhamiria kuacha ndivyo mvutano na sumaku ya kuwaweka karibu na upofu wa mahaba unavyozidi kupendeza.

Itafute movie moja ya kitambo inaitwa Match Point
 
Mke wa mtu anatakiwa anipe papuchi na pesa pia. Yaani nikimpa msimbazi, siku nikihutaji ananipa msimbazi na tembo.

Nimfungulie biashara nilimzaa mimi? Kawa mke wangu?

Itokee tu bahati mbaya nimempa laki halafu niende mbali. Kama nipo hapohapo, nampelekea moto na hiyo hela lazima irudi whether directly or indirectly.

Awe mke wa mtu au mwanamke huru, ewe mwanaume usiwekeze kwa nia ya kuendelea kuwa naye. Wanawake hawana huruma hata siku moja. Unampa pesa anampa mume mwenzio.
 
PART V
Wana MMU, haka kastori ni ka mtiririko wa miaka mingi.
Na nakaleta ili walimwengu muone mwanaume anavyoweza kuwa mjinga kwa penzi.
Mwanamke anakufunga kamba kwa kukupa uroda unaoweza kukupumbaza, wewe ukawa unampenda lakini yeye anakupenda just enough kupata kile anachokipata kwako.
Kama amekuchoka au ndo unaelekea down, kuna wanawake ni wajanja sana ku jump a sinking ship na kudandia nyingine.

Kitendo cha Clara kuolewa kilinikera haswa.
Lakini kabla hajaolewa niliongea naye kinaga ubaga.
Nilimwambia wewe Clara nilikutongoza ukiwa huna hili wala lile huko mkoani, ila ulichokuwa nacho ni ule uzuri wako natural ulioufunika katika nguo zisizo na hadhi.

Nikakuanzishia biashara, nikakununulia gari, umenona umependeza sasa unaniacha.
Nilimwambia mimi simjui na sitaki kumjua anayetaka kukuoa, ila ujue amekuona baada ya mimi kukuibua.
Na vile vile kwa wewe mwanamke nimekuinua sana kimaisha, kwa vile nakupenda.
Nikaendelea kumwambia kuwa nitaendelea kumpa support kwa elimu ya mtoto wangu.
Ila nikamsisitizia, ili nisiumie moyo sitamsumbua kwa lolote.
Na nikamwambia kumtakia heri, hata ndoa yake nitachangia, na nilifanya hivyo.

Maneno yalikuwa ni mazito na hata Clara alikuwa na masikitiko, ila hakuweza kujibu lolote la maana bali kusema wajomba ndivyo walivyo amua.
Clara alikuwa na mama yake tu, baba yake alifariki kitambo.

Tukaachana, na mimi nikaendelea na hamsini zangu.
Clara alioana na kijana mwenziwe na mimi wala sikutaka kwenda harusini licha ya kualikwa.
Niliona ndoa yao kwenye Facebook, wenyewe wakiwa na furaha tele.

Baada ya ndoa alinitumia ujumbe kuwa wanahamia Dar, lakini nikaona hayanihusu.

Mimi nikaendelea kufukuzia shilingi katika mishe mishe zangu jijini na kimsingi mambo yangu Alhamdulillahi yalianza kuwa poa.
Mimi kubadili fashion ya gari ilikuwa kama kawa, na kwa kweli nilimshukuru Mungu.
Ikapita zaidi ya mwaka na nusu, mie sina hili wala lile, mara nikapata simu, namba siifahamu.
Nikatuma ujumbe wa sms kuwa atume ujumbe, niko mkutanoni.

Ikapita saa nzima simu ile ikaita tena, nikaona hebu niipokee.

Ikaanza"mwanangu hujambo"
Nikamjibu "sijambo mama shikamoo , ninani anaongea?"

Akanijibu "mimi mama yako, mama yake Clara"
Nikaitazama simu na kushangaa!
Nikamuuliza kama ni wazima wa afya pamoja na mtoto wangu.
Akanijibu kuwa ni wazima, ila Clara alikuwa anaumwa tumbo lake lile alilofanyiwa operation.
Nikataka ampe pole Clara na kumtakia apone haraka.

Hapo ndipo mama Clara akafunguka.
"Mwanangu mimi mama yako nakuomba radhi kwa yote. Uniwie radhi sana, Clara ana matatizo makubwa na nisipokuarifu ili utusaidie tutampoteza. Uniwie radhi mwanangu hatukuelewa.
Mimi naongea na wewe ndugu zangu hawafahamu, naomba baba, naomba utusaidie"
Nikamwuliza mama sasa itakuwaje mimi kumhudumia mke wa mtu, na mumewe yupo.

Mama akasema yule kijana hana uwezo wowote, na ugonjwa wa Clara unahitaji specialist wa magonjwa ya wanawake, na kuwa hivi tunavyoongea kalazwa, na wako pamoja hospitali moja binafsi.

Duh...nikapigwa mkanganyiko.
Clara hatujaonana zaidi ya mwaka na ushee!
Sasa napata simu toka kwa mama yake!
Lakini nikasema nitaenda kumwona.
Nilipoingia chumba alimolazwa nilimkuta binti ambaye alitoka nje ,na mama Clara yeye kakaa pembeni .
Nikamsalimia mama na nikaenda kitanda alipo Clara.
Nikambusu shavuni, kwa upande nilimwona mama anainama huku akitabasamu.
Clara alifurahi ila uso ulikuwa na hali ya kuonyesha maumivu.
Nikaomba bili ya matibabu na nikawapa fedha zote.
Haraka haraka nikamwambia mama siwezi kukaa zaidi hapo maana nisijeshikwa ugoni!
Mama ajacheka akasema nisijali sana.
Nikaondoka.

Clara alikuja toka hospitali ila hakupona.
Tumbo liliendelea kumsumbua.
Sasa alipungua mwili akawa kama ufito.

Ilibidi kuwaona madktari bingwa ambao walisema tatizo kubwa ni ile operation ya kujifungua na operation iliyofuatia.
Madaktari waliomfanyua upasuaji hawakuwa na ujuzi wa kutosha.
Hata hizi operation zilizofanyika karibuni hazikuwa nzuri.
Hivyo wakashauri apelekwe India.
Kizungumkuti ni kwamba mume wake Clara hana kitu na familia yake nayo ni ya watu wa kawaida sana.

Nikabeba tena majukumu, Clara nikamgharimia akaenda India ambako alifanyiwa upasuaji tena.
Madaktari India walimwambia watafanya operation hiyo katika stage mbili. Mara ya kwanza walifanya operation nzito na wakamwambia inabidi apumzike miezi mitatu halafu arudi tena wammalizie operation ya mwisho.

Ikawa hivyo, na ndio kupona kwa Clara.

Tatizo nimemtibu mke wa mtu, lakini ni mama wa mtoto wangu.

Mwisho wa yote, alipopona sasa Clara nikasema kwa nini nisijaribu mitambo!
Na kwa kweli tukaitesti, tukarudi tulikokuwa zamani, lakini mimi bado mwizi!
Penzi likawa moto sana sana, mpaka bibie sasa akaniambia anataka mtoto mwingine!

Walimwengu niishie hapo.
Ushauri wenu tafadhali.
Hiyo ndo ilikuwa akili yangu, nampiga mimba tena, jamaa alee nitakuja kumchukua mwanangu. Mali ulizompa zitumiwe na wanangu.
 
Kama bibilia inavyosema tu "Ndoa na iheshimiwe na watu wote" bhasi kwakua clara alishaolewa usingerudisha mahusiano nae tena ila ungebaki kama mwanaume uliezaa nae tu na heshima iwepo...
ukiheshimu ndoa yako na yake pia ndipo heshima yako itakapo onekana na kuheshimika pia.... ila huku unapoelekea mkuu unaenda dhalilika na kushuka heshima
Dogo kafunga ndoa na mke wa mtu, pana ndoa hapo wakati mke ana mtoto wa mtu?

Tunarudi kulekule, single mother huwa wanapasha viporo na wazazi wenzao
 
Wewe tunakupa cheo cha ukufunzi! Wengine wakiwa hatua za awali kabisa, yani pale mwanzoni mwanzoni tu hali ya hewa inachafuka makao makuu kwa kukamatwa. Nashangaa wewe umeogelea mikasa yote hiyo na bado umevuka.

Sasa Jemedari, najua itakua ngumu sana kunielewa na sio rahisi (Hapa naongea kama mwanaume) haitakua kazi rahisi sana kukaa mbali na huyo mwanamke (Mzazi mwenzio.

Kwamba umeshakwepa mishale mingi sio kesi sana, ila nnachokuhakikishia, siku wife akigundua na ikaleta tafrani, hautakaa utulie na akili itakurudi. Ni fedheha sana watu wazima kuanza kukaa kukujadili kwa kesi ya michepuko. Na kitakachomuuma zaidi wife sio kuzaa mtoto, ni ile mnaendelea.

Kwa akili zetu wanaume zilivyo, hiyo hali ilivyo na ulivyomgharamia imeongeza sana intimacy kati yenu, sio rahisi kuzinduka kwa sasa ila inabidi ufanye maamuzi magumu. Hapo ulipo ukimuwaza Clara kidogo na mambo mliyopitia ni dakika moja tu unafunga safari kwenda kumuona.

Itakuathiri kwa muda kusitisha mahusiano na Clara, lakini utajenga msingi imara wa future yenu wote. Kumbuka hadi hapo Clara hana cha kupoteza kuendelea na wewe, hata huyo mme wake sifikirii anamjali au kuona ni tatizo. Lakini kwako vitu vingi vipo hati hati.

Pamoja na maongezi yote hayo...bado mpango wetu na Evelyn Salt uko pale pale.
Weka wazi mpango wako na evelynSalt
 
Mkuu naona umefanywa jogoo la kuazimwa na umeazimwa kweli kweli...

Tatizo ya jogoo la kuazimwa, itapofika kipindi haliwezi fukuzia mitetea tena huwa linachinjwa na hadithi yake kuishia hapo...

Sasa mkuu, wewe kama jogoo hapo kati ulishachinjwa lakini naona kama wataka kufanya unimaginable kwa kufufuka na kurejea tena enzi...

Ulifanya kosa mara moja, pengine mara mbili au zaidi, haina maana sasa urudie kosa lile lile...
 
Back
Top Bottom