Ushauri wenu, dunia naona mviringo!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,882
13,171
Mimi si mwanachama na mchangiaji sana huku MMU, lakini hata bubu aking'atwa ataongea hata neno.
Huku kuna walimwengu wa maisha halisi ya kibantu.

Hadithi ni ndefu lakini nitaifupisha.
Nina mke na watoto, tena wakubwa tu.
Katika mishe mishe za safari mikoani huko, sitaji mkoa lakini nilikaa mwaka.

Hili na lile katika kuchapa ripoti za kazi tukaelewana sana dada mmoja, kwa kweli alikuwa mzuri na ni figure 8.

Kwa utani tu nikatongoza, hakujibu wala kukataa.
Bado nikaendelea kutongoza, mwisho baada ya miezi 3, akakakubali na akasema nikuambie kitu?
Nikastuka kidogo, ila akaniambia nitakuambia tukionana.
Kweli tukaenda outing, na tukala na kunywa.
Kwa kweli tuli enjoy.

Fukuto langu lilikuwa kujua anachotaka kuniambia.
Na wakati huo alivyo mzuri na umbo la kutia hamasa, moyo unanidunda ndi.. ndi..ndi...!

Nikamsihi aniambie.
Akaanza taratibu.
Kaka mimi nimeolewa.
Moyo wangu ukadondoka pwaa....!
Sasa itakuwaje tena kumpenda mke wa mtu?
Nikamwuliza na kujiuliza, na nikaanza kusononeka.
Yule dada aliona kusononeka kwangu, lakini akanituliza, akaniambia usijali kaka.
Akaniambia amenichunguza sana muda wote huu licha ya kuolewa, na amenipenda ndio maana ana kitu cha kunieleza.
Ha!
Nikajiuliza , kuna kingine tena ?
Nikamwuliza kuna kitu gani?

Yule dada kwa unyonge akasema nitakuwa pamoja na wewe ila nifichie siri yetu!
Nikamwambia mbona hilo si tatizo mpenzi!
Akanidakia tena, akaniambia tukisex hataki condom!
Hapo nikapigwa butwaa!

Sasa nami nikadakia, mbona sielewi?
Nikamwambia si utapata mimba?
Huku nikijzuia kumwambia magonjwa je?

Hapo ndii akanieleza taratibu, kuwa ameoana na mume wake miaka miwili na hajapata mimba.
Ikabidi waende hospitali wapimwe na ikagundulika mume wake hana uwezo wa kutengeneza mbegu za kiume.
Na kwamba wameenda hospitali tatu tofauti, majibu ni yale yale.
Akaniambia ,nami natafuta mtoto, nimekupenda.

Nilichanganyikiwa!
END OF PART I

Wadau ushauri wenu, part zingine NNE zitakuja mbele.

PART II
Nawashukuru sana wadau kwa kulitolea neno na maoni kwa mkasa huu ambao tayari umenipata kimaisha.
Ni mkasa mrefu, ila niwataarifu tu kuwa ni mkasa uliotokea muda mrefu, ingawaje niliyohadithia ni ya kweli kabisa.
Na sasa tuendelee....

Yule mtoto mzuri baada ya kunipa yake ya moyoni kuwa kwanza ameolewa, pili, mume wake hana uwezo kimwili kuzaa kwa vile madaktari wamesha sema hana mbegu za kutia mimba, tatu binti naye kanichunguza vizuri, ananipenda, na haja yake ya moyo ni kupata mimba na kuzaa.

Hili kwangu kama anavyosema Evelyn Salt, ndio bomu la Hiroshima.
Bibie kwa kweli nimempenda bure, ni mzuri na kuongea naye tu inatia hamasa.
Wanaume tulio wengi ukumpata bibi kama huyu unajipiga kifua cha u hero.
Lakini mmmm.... mke wa mtu.
Tena hataki condom, na anataka mtoto.
Hayo masharti na hali ni ngumu.
Nikaimba poo ili tuonane siku nyingine.

Bibie akatambua, nataka kuchomoka.
Na alishaona nimeshaingia mtego, mie nataka vitu, yeye ana shida, sharti ni kumpa mtoto.

Hapo nikakutana na Eva, yule aliyemtongiza Adam ili ale tunda.
Mwanamke uliyemtaka kwa kumtongoza, akikubali, kumchomoka ni miujiza!
Yule dada akajirembua na kuwa laini, sauti laini na si muda mrefu nami nikaingia line.

Tulipanga tukutane siku ya pili , lakini I took no chances, nilibeba kinga,condom.

Tukaenda hoteli ya hadhi nzuri, na baada ya maongezi, kula na kunywa, tukaingia swala la msingi. Na alipovua nguo ndio nilipigwa butwaa!
Yule dada alikuwa viwango vingine kabisa.
Nikisema alikuwa mzuri kwa kumwona kwenye nguo, basi alipotoa nguo zote nilichanganyikiwa.

Mimi napenda beutiful girls, hata mke wangu ni bomba, lakini huyu alipendelewa zaidi.

Wanaume tuna matatizo, tatizo kubwa ni hisia, ukiona mwamke mzuri tayari hisia zako zinakimbilia kula tunda uone utamu wake.
Nami vivyo.
Ila ukweli kuna wanaume, mimi simo, ambao wakiona tu vile alivyo binti mzuri, uchi kama alivyozaliwa, lazima anapata mfadhaiko na wengine kujikojolea!.

Nilichokuwa naona mbele yangu ni mwanamke aliyeumbika haswa, tako lipo ni zuri la wastani, paja na hips zimelifanya tako kuwa na mvuto wa pekee.
Matiti ni makubwa ya wastani, mviringo na chuchu zipo katikati, na hayo matiti wala hayajaanguka , yako imara.
Kakiuno kapo kazuri sana, kadogo na tumbo dogo.
Ndiyo ile figure 8 niliyikuwa naiongelea.
Akili ikanirudia kidogo!
Kwanza nikajiulizwa ,what am I doing?
Na nikatoa condom na kuanza kuchana kifungashio.
Bibie alipoona hivyo akatishia kuvaa nguo na kuondoka!
Nikaitupa condom na kumkumbatia
, baada ya romance kidogo mie wazimu kama unanipanda.

Tukala vitu!
Lakini mi nilikuwa over excited, sikudumu dk 3.
Kwishney!

Cha ajabu sana, bibie haraka haraka akavaa nguo, na kushika pochi yake, na kusema naondoka.
Hakuenda kunawa wala nini!
Nikawa bado kama sielewi, ndo nikakumbuka, lengo la bibie ni kupata mimba!
Nikalielewa hilo.
Nami nikarudi Dar nikiwa na mawazo mchanganyiko.

Baada ya kupita mwezi nikarudi tena mkoani.
Nikitaka rematch maana ile ya kwanza nilipigwa off side.
Sasa nataka full match!

Lakini nilipo onana na bibie Clara, I was in for a shock!
Tukaenda mgahawa maridadi na tukala chakula.
Biebie alionekana kuwa na furaha na katika maongezi, bado ni kama ana swala ambalo halijapata ufumbuzi.
Lakini alianza kwa kuangusha bomu!
"Mpenzi "aliniambia,
"nina mimba, ila kuna jambo sikukueleza"

Moyo ukaruka , na nikajiuliza baada ya hili bomu la mimba, kuna nini tena?

PART III inakuja!

PART III
"Kuna kitu sikukuambia, mpenzi,mume wangu anaumwa sana, tena kwa muda mrefu" alisema Clara

Moyo ukapiga paaaa.....!
Nikajisemea moyoni , mama yangu ukimwi huo!

Bibie aliona mkanganyiko wangu.
Baada ya muda nami nikapata nguvu ya kumuuliza.

"Ameathirika na ugonjwa gani", nilimuuliza.
Bibie alika kimya kwa muda, hakujua mimi huku moyo unadunda kama pampu ya maji.
Nilimuuliza mara ya pili anachoumwa mumewe, maana nilanza kukosa uvumilivu.

Clara alianza taaratibu kuelezea.
Mme wake katika kazi yake alipata matatizo ta kifua, inaelekea huko kiwanda anachofanya alivuta hewa chafu iliyomuathiri mfumo wa hewa na mapafu.
Aliniambia kwa miaka yote wameoana alianza kuugua taratibu lakini katika mwaka huu mmoja uliopita anashindwa kupumua sawasawa.
Aliniambia mwaka ule mmoja waliooana ndiyo amekuwa angalau anaweza tendo la ndoa,pamoja na mapungufu kuwa hawezi kuzaa, ila mwaka huu mzima uliopita amekuwa akiuguza tu na hawezi hata kudiriki kufanya tendo la ndoa.

Nilimuuliza tena sasa kwa kutaka uhakika, kama hajaathirika na ukimwi.
Clara alijibu, tena kwa kujimini na kushangaa, kuwa hapana, yeye tatizo lake ni hayo mapafu yanayomkosesha kupumua na mwili kukosa nguvu.

Nikashusha pumzi, si kwa furaha bali kwa kushukuru kuwa kawingu ka kufikiria kuwa sasa naweza kuwa nimeathirika na mimi, kamepita, ingawaje bado wasiwasi ulikuwepo moyoni bado.

Baada ya hapo ndio tukarudi kwenye bomu letu.
Mimba.
Nikamuuliza sasa itakuwaje watu wakiuliza umepata wapi mimba, na wanajua kuwa mume wako hawzi.

Hapo ndio nikatambua kuwa wanawake wanatuzidi.
Akanieleza kuwa siri ya ndani kwao ni yeye na mume wake, hakuna anayejua lolote, hata ndugu zake.

Sasa, nikamuuliza mumwe wako je , akiuliza mimba hiyo ya nani.
Bibie alinyamaza, machozi yakamlenga lenga, na alijibu taratibu kuwa kwa hali aliyonayo mumewe hajakata tamaa lakini kwa kweli ni changa moto.

Kwa mazungumzo hayo tuliyokuwa nayo, hata bia iliteremka kwa shida.
Na niliyotaraji ya rematch hayakuwepo tena.
Mpaka narudi Dar kwa kweli niliona kama nimepatikana , wala sijapata.

Ikapita miezi miwili hivi, usiku wa saa mbili nikapata simu toka kwa Clara.
"Mpenzi" , aliniambia
"Mume wangu amefariki"
Niliangusha simu chini kwa mshtuko.
Baada ya kupata fahamu, nikajua nimekula nanasi na maganda yake.

Itaendelea Part IV, coming soon!

PART IV
Bibie Clara akajifungua mtoto mzuri wa kike baada ya miezi yake tisa kupita.
Muda wa msiba ulipita na hapo ikawa ajira yake alipokuwepo haipo.
Na utegemezi wake ikawa mimi.
Nami kwa kuiona umuhimu ikabidi nijitahidi kumsaidia kila hali, ili ayamudu maisha.

Lakini nikikaa peke yangu na kufikiria nikawa nawaza.
Nimemla huyu Clara kiduchu tu, na nimebeba majukumu yote ya mume.
Nimefikaje hapo?
Pamoja na uzuri wake, udogo wake kiumri, lakini kesha badili punda na sasa mimi ndio mume na nina mtoto naye.
Hata hivyo kwa kuajibika kiubinadamu tu, siwezi kumwacha sasa hivi, kwani yeye hakupanga kuugua mumewe.
Lakini muda wotehuo moyoni alijua mumewe ndo anaishia, hivyo akashikilia unyasi uliokuwepo, unyasi uliojileta wenyewe kwa kumtongoza.

Hata hivyo mimi nilikuwa na furaha moyoni, furaha ya mtoto.
Kwa mke wangu nyumbani nilikuwa na wavulana watatu, sasa nimepata kajike.
Nililiwazika moyoni, na hili lilinipa uwezo wa kuyakubali majukumu.

Hata hivyo huu ukawa mwanzo wa matatizo yangu ya muda mrefu.

Mtoto aliendelea kukua na nilipomwona baada ya miezi mitatu kupita nilifurahi sana.
Kwa kweli nilifanana naye kwa vitu vingi, nywele, macho, pua na meno yalivyojipanga na hata mdomo.
Na baada ya mwaka kupita ,hata rangi ya ngozi.

Clara mara nyingi akisema nina damu kali sana, kwani mtoto tumefanana.

Baada ya muda wa miaka miwili, kule bibie alikokuwa anafanyia kazi biashara ikayumba na kufungwa.
Hivyo akaniomba mtaji afungue ka Secretarial.
Nikamkubalia maana sasamahitaji yake niliyokuwa natuma kila mwezi yalikuwa makubwa, sasa inabidi aanze kujikimu kwa kiasi.

Biashara yake ikawa nzuri na kukua, nami safari za kwenda huko mkoani "kulea" zilikuwa haziishi.
Ghafla bibie akaanza kuugua tumbo la uzazi lililotokana na operation ya kujifungua.
Tatizo lilianza taratibu, na baada ya miaka mitatu au minne Clara alikuwa hata kukaa chini hawezi.
Madaktari walimwambia afanyiwe upasuaji mwingine, kuna mambo hayajakaa sawa tumboni.

Akafanyiwa upasuaji, na hapo ndio nikaonana na mama mkwe hospitali.
Niligharimia fedha zote za matibabu.
Mama mkwe alinitazama kwa makini tukisalimiana.
Mwisho nikajua tu, amenikubali maana mwanaye alikwisha muambia ninavyomhudumia.

Bibie alipona na kurudi kwenye biashara yake ambayo iliendelea kushamiri, na akaomba nimnunulie jenereta kutokana na kukatika katika umeme, nikamnunulia.
Na mtoto sasa akaanza nursery na
baada ya miaka miwili akaanza la kwanza, na sasa mkubwa.

Mahitaji ya bibie Clara yaliendelea kuwa makubwa, licha ya biashara yake kushamiri.
Bibie alinenepa na akawa mzuri zaidi, nami nikaendelea kujilia vitu taratibu, sasa nikimpa nauli aje Dar.
Hatimaye akaniomba nimnunulie gari dogo maana alisema anabanwa banwa sana kwenye usafiri wa umma.
Nami nikamkubalia, kwa wivu nilitaka niwe nambana mimi tu.
Maisha yakaendelea.
Ndugu zake wengi walitaka tufahamiane, mi nikakataa nilimwamnia Clara mradi nafahamiana na mama, inatosha!

Huku nyuma yangu mtoto kanawiri, na kwa kweli akivaa na kuonekana hadharani anapendeza.
Mijamaa ikaanza kumezea mate hukohuko mkoani.

Mimi sina hili wala lile, nina nyumba ndogi, sijaioa hivyo nikahisi huko naliwa vitu vyangu.

Nami nikaanza tena safari za kumtembelea huko mkoani.
Uhusiano haukuwa motomoto tena.
Nikawaza sana, nikajua ana mtu anamchukua.

Baada ya kwenda mara tatu mkoani na kuona kiwango cha penzi kikizidi kushuka ikabidi nimuulize tu kuwa kuna nini, umepata mfadhili mwingine?

Naye akashukuru kupata upenyo wa kuniambia.
Akaniambia kuwa anataka kuolewa.
Anaye jamaa wana uhusiano na wamepanga kuoana.
Ameshawaeleza ndugu zake na mipango imeshaanza ya ndoa.

Nilipigwa butwa, kama teke ni la tumbo basi lilikuwa hilo.

Nikamuuliza kama kweli alikuwa na uthubutu wa kunifanyia hivyo.
Akanijibu kuwa wajomba zake wameamua kuwa hawezi kuendelea kama alivyo, lazima aoelewe.
Iliniuma sana, nikamuuliza na mama kama yumo kwenye maamuzi hayo.
Akanijibu ndivyo familia ilivyokubaliana.
Nilisikitika, nikasononeka, lakini faraja pekee ni kuwa nina mtoto wangu.
Nikarudi Dar kwa majonzi ya kupokwa penzi.
Bibie nilimwinua toka hana kitu na hajulikani, sasa yuko matawi, kanipiga kibuti.
Nikakubaliana na hali, na nikajiambia kuwa yote ni yeye mwenyewe Clara, angeamua kubaki nami ni yeye.
Kaamua kuingiauhusiano mwingine ni maamuzi yake, si ya wajomba wala mama.

Nilikula vya watu, nikavifanya vya kwangu, nami vyangu vinaliwa na kuchukuliwa jumla.
Na bibie alikuwa mzuri kweli kweli, kachanua.
Ili nisiumie moyoni nikakubaliana na hali, nikakubali kuwa penzi langu na Clara limeishiwa vocha, na mimi inabidi nitembee.
Nikatembea
Itaendelea PART V
 
Mimi si mwanachama na mchanguaji sana huku MMU, lakini hata bubu aking'atwa ataongea hata neno.
Huku kuna walimwengu wa maisha halisi ya kibantu.

Hadithi ni ndefu lakini nitaifupisha.
Nina mke na watoto, tena wakubwa tu.
Katika mishe mishe za safari mikoani huko, sitaji mkoa lakini nilikaa mwaka.

Hili na lile katika kuchapa ripoti za kazi tukaelewana sana dada mmoja, kwa kweli alikuwa mzuri na ni figure 8.

Kwa utani tu nikatongoza, hakujibu wala kukataa.
Bado nikaendelea kutongoza, mwisho baada ya miezi 3, akakakubali na akasema nikuambie kitu?
Nikastuka kidogo, ila akaniambia nitakuambia tukionana.
Kweli tukaenda outing, na tukala na kunywa.
Kwa kweli tuli enjoy.

Fukuto langu lilikuwa kujua anachotaka kuniambia.
Na wakati huo alivyo mzuri na umbo la kutia hamasa, moyo unanidunda ndi.. ndi..ndi...!

Nikamsihi aniambie.
Akaanza taratibu.
Kaka mimi nimeolewa.
Moyo wangu ukadondoka pwaa....!
Sasa itakuwaje tena kumpenda mke wa mtu?
Nikamwuliza na kujiuliza, na nikaanza kusononeka.
Yule dada aliona kusononeka kwangu, lakini akanituliza, akaniambia usijali kaka.
Akaniambia amenichunguza sana muda wote huu licha ya kuolewa, na amenipenda ndio maana ana kitu cha kunieleza.
Ha!
Nikajiuliza , kuna kingine tena ?
Nikamwuliza kuna kitu gani?

Yule dada kwa unyonge akasema nitakuwa pamoja na wewe ila nifichie siri yetu!
Nikamwambia mbona hilo si tatizo mpenzi!
Akanidakia tena, akaniambia tukisex hataki condom!
Hapo nikapigwa butwaa!

Sasa nami nikadakia, mbona sielewi?
Nikamwambia si utapata mimba?
Huku nikijzuia kumwambia magonjwa je?

Hapo ndii akanieleza taratibu, kuwa ameoana na mume wake miaka miwili na hajapata mimba.
Ikabidi waende hospitali wapimwe na ikagundulika mume wake hana uwezo wa kutengeneza mbegu za kiume.
Na kwamba wameenda hospitali tatu tofauti, majibu ni yale yale.
Akaniambia ,nami natafuta mtoto, nimekupenda.

Nilichanganyikiwa!
END OF PART I

Wadau ushauri wenu, part zingine NNE zitakuja mbele.
Part 2 wap hyo??

Nashauri kupitia experience hii ,, tujitutumue tutengeneze movie,, tutspiga noti za kutosha
 
Back
Top Bottom