Ushauri wa bure: Madereva wa private cars tembeeni usiku kama unafanya Safari ndefu

Usiku haufai kama unajijua unatabia ya kusinzia! Lazma ujue sleeping pattern yako vyema. Mfano mie usingizi wangu ni saa 6-7 hapo lazma nilale nisipolala hapo jua silali mpaka kunakucha. Ila nikinywa energy drink kabla ya huo muda silali kabisa.

Cha muhimu pumzika vya kutosha mchana kisha hakikisha unapoanza safari uko well hydrated ili macho yaone vizuri pia unaweza kutumia energy drink ilio diluted na maji ili ku activate mwili pia caffeine huondosha usingizi!
Namkunjuga wife kisawa sawa kabla ya safari, baada ya hapo huwa kuna ka usingizi kananipia kakikata tu hako naliamsha dude nikiwa mwepesi hapo hata 24hrs naweza nisilale.. na hapo ndio huwa nawin trip za usiku.. unakuta tunapiga game mitaa ya jioni flani hivi, nikishtuka tu nakiwasha😂😂😂😂
 
Imenisaidia mara kadhaa. Ni kiasi cha kuwa serious tu; pia ikitegemeana na muonekano wako na usafiri unaotumia. Wengine tuna sura za kikauzu, ukisema kitu unaaminika mara moja.
muonekano nao muhimu, mchana nikiwa nakumua ndinga huwa napiga smart shati imenyooka, ruluwale imesimama na moko moja matataa 😂😂😂.. alafu hata sibabaiki na reflector yangu ya kikazi... wakinisimamisha, naanza jambo afandeeeeeee.... hadi anacheka japo siku huwa hazifanani
 
Namkunjuga wife kisawa sawa kabla ya safari, baada ya hapo huwa kuna ka usingizi kananipia kakikata tu hako naliamsha dude nikiwa mwepesi hapo hata 24hrs naweza nisilale.. na hapo ndio huwa nawin trip za usiku.. unakuta tunapiga game mitaa ya jioni flani hivi, nikishtuka tu nakiwasha😂😂😂😂
Hahahah una balaa sana chief
 
Pale ndio mahala pa test, ukimaliza game ulale alafu uamke mwili unauma au kahasira flani hivi, inabidi utulie tu 😂😂😂😂.. ila kama ukashtuka tabasamuu furaha paka kwa moyo mwili umechangamka na damu inatembea vizuri.. hapo lianzishe tu 😎😎
Chapakaziii 🤓🤓🤓 mama lazma a appreciate kala kamsemo ka “Njoo nikuage!”
 
muonekano nao muhimu, mchana nikiwa nakumua ndinga huwa napiga smart shati imenyooka, ruluwale imesimama na moko moja matataa 😂😂😂.. alafu hata sibabaiki na reflector yangu ya kikazi... wakinisimamisha, naanza jambo afandeeeeeee.... hadi anacheka japo siku huwa hazifanani
Ukishasema “jambo afandeee” ushakosea tayari - umekuwa umejidogolesha!
 
Usiku unatembea vyema tu, ila kama ni mtu wa usingizi sio salama, na hasa ukianza kuhisi kucnzia paki upumzike. Kuna ile hali ya kucnzia bila kujua, ni hatari sana hii. Hasa ukiwa kwenye mwendo yani kuchochora ni simple tu, ajari za usiku 90% ni usingizi.

Mimi nikichoka huwa naanza kucnzia, na tena sitajua nimecnzia saa ngapi, ukimya ukitawala tu na ucngizi huu hapa. Kuna madereva wengine wana tabia ya kusinzia huku anaendesha, yani anajua kabisa kwamba anacnzia ila anaweka gari kati ndo anaanza kusinzia sasa, hii ni hatari sana.
 
Imekuwa desturi na mazoea kwa madereva wengi wanaoendesha magari yao binafsi kufanya safari zao ndefu muda wa mchana ingawa ni jambo jema ila kwa mtazamo wangu mimi naona ni shida na usumbufu mwingi njiani.

Naongea hivyo kwasababu ndani ya mwezi Machi nilifanya safari ndefu ya kwenda Mwanza na gari yangu. Nakumbuka nilianza safari usiku saa 7 kutoka Dar ili kuepusha usumbufu kwenye kipande cha Dar-Moro (kwa wazoefu wa kipande hiki watakubaliana na mimi). Muda wa mchana nilipata shida na usumbufu na traffic pamoja mabus na fujo zao mpaka naingia Mwanza usiku saa 3.

Mpaka nimeamua kuandika ushauri huu ni kwa madereva wenzangu ni ushuhuda niliouona kwa macho yangu wiki hii.

Jumamosi iliyopita nimefanya safari tena nyingine ya kwenda Mwanza kwa kupanda bus hakika vituko vya madereva wa bus ni noma, hawa jamaa wanatumia barabara watakavyo,wanaovertake watakavyo tena sehemu yeyote ile ilimradi amekupita, yaani zile speed za miaka ile zimerudi tena na traffic hawana la kusema kwasababu jamaa alipigwa tochi mara 5 na bado hakupigwa cheti mpaka tunafika Mwanza.

Dereva wa bus alikuwa anaovertake mpaka malori matano hasa pale akiona mbele yake inakuja gari ndogo yaani utake usitake utasimama tu mpaka amalize kuovertake kumbe jamaa wanatudharau sana mpaka wanatuita wamama wa nyumbani (msemo huu alikuwa anautumia dereva wa bus akiwa anafanya fujo zake).

Nimeshuhudia kwenye vibao vya speed 50 magari madogo wanakatwa na traffic huku bus letu linapita tu tena na mwendo mdundo bila shida tena likiwa speed 102 hata ile alarm ya speed hakuna.

Nawashauri madereva wenzangu tembeeni usiku kuepusha majanga mchana haya mambo ya mchana tuwaachiwe wenye njia yao madereva wa mabus kwasabb kama kuna watu wanaenyoj barabaran ni watu wa mabus tu...Wale wenzangu na mm tusione tabu kuendesha usiku
Pia usiku rami inakua imepoa so chances za pancha ni ndogo, magari machache Road na usumbufu wa trafiki nehi ila angalizo kama una poor night vision usifanye safari za usiku.
 
Mkuu mwezi wa 4 nilikua naenda Njombe na Luwinzo na nilikaa mbele kwa Konda..tulipofika Iyovi jamaa alikua anafuta kisahani kama kawa mwendo mchubuyu so mtoa mada yupo sahihi.
pureView Zeiss

Kaka,

Unachosema ni kweli. Binafsi nimekua mtu wa kuendesha usiku mara kwa mara.

Na nimeenda mikoa mingi tu.

Ila changamoto kubwa ya usiku ni hawa watu wa malori na pia mambo ya uharifu zaidi sana iwapo utapata dharura.

Watu wa malory asilimia kubwa wengi wao hua hawazingatii sana sheria nyakati hizo za usiku.

Wamesha sababisha ajali nyingi mno barabarani (baadhi yao)

Kuhusiana na suala la mabus, hizo speed unazosema kaka ni speed zipi?
Mbona jamaa wanatembea vizuri tu, zaidi sana magari yote ya abiria sasa hivi yanaving'amuzi.

Sina hakika kama hakika kweli wanaenda rough hivyo.

Usiku ni raha, lakini ni hatari kubwa sana.
 
Back
Top Bottom