Ushauri wa bure: Madereva wa private cars tembeeni usiku kama unafanya Safari ndefu

Craig

JF-Expert Member
Feb 9, 2013
992
1,000
Wewe kama unaona usiku kwako dili usitushawishi wengine, Kuendesha kwangu kwangu starehe haya niendeshe usiku naenda vitani au !!?

Sura nitauza saa ngapi manake Ndinga yangu ni yakufanyia ubishoo. Usiku nikutane na madereva malori wanasinzia iweje ??
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
49,580
2,000
Nakumbuka kuna siku tulikuwa tunawahi harusi kesho yake. Tukatoka Mwanza saa 12 jioni ili tuingie Dar saa 2 au 3 asubuhi.

Kwenye gari kila mtu alilala, tukabaki mi na dereva tu tunapiga story.

Tukafika maeneo ya tabora nadhani igunga sijui mida ya saa 5 usiku, kitu kimewaka moto.

Hamadi kuna lorry kama mita 50 limezima kati ya barabara na halijaweka alama yeyote. Uzoefu wa dereva ulituokoa lasivyo tusingekuwa duniani leo.

Tulivyofika manyoni mida ya saa 7 hivi tukaamua kulala tu. Hatukuona sababu ya kuwahi tena mjini.

Safari za usiku zinahitaji chombo na dereva imara.
 
kingsize25

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
216
500
Kusafiri usiku ni raha ila panaitaji uwe mzoefu na barabara na gari iliyokamilika kila idara. Hauitaji kukimbia sana mwendo costant tuu 80-110 unafika vizuri, ila kwa sisi wa kumwaga moto basi tunachoma utambi tuu.
 
bush striker

Member
Feb 16, 2019
40
125
Kusafiri usiku siyo mbaya ila ni vizuri njia uwe unaipita mara kwa mara hivyo ni mzoefu wa njia hiyo vile vile taa zako ziwe na mwanga wa kutosha ili kuona mbali zaidi.
Kwa upande wa magari makubwa changamoto si nyingi kikubwa uwe unajuwa njia za mawasiliano na dereva mwenzio wa kutumia taa. Idereva w tahadhari unapopishana na magari makubwa na mara nyingi huwa wanatembea kwa kufatana hivuo tumia taa zako ukiwa mbali kidogo kuwasiliana na dereva unaepishana nae na ni lazima atakujibu tu hapo unaanza kujuwa kuwa ninaepishana nae yuko macho maana wengine huendesha wakiwa nusu macho nusu wako usingizini.
Indicate mwisho wa gari yako nae atafanya hivyo hapo unakuwa salama kupishana na ni vizuri ukipishana nae/nao ukiwa na speed 60km/h au chini ya hapo.
 
Nkolandoto

JF-Expert Member
Sep 18, 2016
3,163
2,000
Kuhusu speed aisee Kwenye haya Mabus niliyopanda hamna nilikaa mbele karibu na Dereva nimeona jamaa anapiga Hadi speed 127 km/h.....kama ujuavyo bus likiwa speed hiyo ni balaa yaani Ngoma inatembea balaa Hadi Mwanza nyegezi tumeingia saa 4:48 usiku
Huo unaousema ni mwendo wa kawaida sana siku hizi nadhani kipindi cha mzee wa msonga ungekuwa umechunguza ungelog off magari mwanza to Dar ilikuwa saa mbili zimechelewa ngoma tatu

Hawa jamaa wanakimbia kupita hasira
 
Nzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
13,957
2,000
Kusafiri usiku siyo mbaya ila ni vizuri njia uwe unaipita mara kwa mara hivyo ni mzoefu wa njia hiyo vile vile taa zako ziwe na mwanga wa kutosha ili kuona mbali zaidi.
Kwa upande wa magari makubwa changamoto si nyingi kikubwa uwe unajuwa njia za mawasiliano na dereva mwenzio wa kutumia taa. Idereva w tahadhari unapopishana na magari makubwa na mara nyingi huwa wanatembea kwa kufatana hivuo tumia taa zako ukiwa mbali kidogo kuwasiliana na dereva unaepishana nae na ni lazima atakujibu tu hapo unaanza kujuwa kuwa ninaepishana nae yuko macho maana wengine huendesha wakiwa nusu macho nusu wako usingizini.
Indicate mwisho wa gari yako nae atafanya hivyo hapo unakuwa salama kupishana na ni vizuri ukipishana nae/nao ukiwa na speed 60km/h au chini ya hapo.
Aisee haya uliyoyasema uwa nayazingatia sana. Uwasha indicator ya kulia kuonyesha mwisho wa gari langu. Pia uwasha high beam tokea mbali ili kuwasiliana na dereva anayekuja.

Usiku ya saa 7 hapana aisee. Mimi ni kama Bavaria, alfajiri ndiyo muda wa kuanza safari.

pureView Zeiss unatoka Dar saa 7 usiku na unafika Mwanza saa 3 usiku? Mbona ulitumia muda mwingi hivyo?
 
Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
54,558
2,000
Kuna faida na hasara za kusafiri usiku...

Kama unataka usafiri unatakiwa uzingatie tu vitu vichache...Unatakiwa uijue barabara mwanzo mwisho, uwe na gari iliyokaguliwa kila kitu, usiwe peke yako kwenye gari, usijifungie vioo vyote, jitahidi uongozane na gari au magari mengine...

Sisi wengine tunapenda safiri usiku kwa sababu unapunguza big time muda wa safari kama ungelisafiri mchana, safari ya masaa 12 unaweza ishusha hadi masaa 9...

Muda wa usiku gari inapoa vizuri kutokana na hali ya hewa kutokuwa ya moto, hivyo unaweza ifanyisha kazi injini kwa muda mrefu, hakuna mambo ya 50 zaidi ya roadblocks/checkpoints chache...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
54,558
2,000
Tukafika maeneo ya tabora nadhani igunga sijui mida ya saa 5 usiku, kitu kimewaka moto.

Hamadi kuna lorry kama mita 50 limezima kati ya barabara na halijaweka alama yeyote. Uzoefu wa dereva ulituokoa lasivyo tusingekuwa duniani leo.

Hivyo huwa vinaitwa vicheche...

Sasa kuna hao wa malori na kuna wale wapumbavu wanaowahi na matrekta alfajiri kuanzia saa tisa kwenda kulima, na huwa hayana taa wala refleta yale...

Ushawasha mashine inacheza 170-180kph, anatokea kiazi mmoja na Powertila lake porini huko analiingiza barabarani kama mbwa anayevuka barabara...

Hawa wapo sana maeneo ya Iringa hadi Igurusi kwa barabara ya Tan-Zam, au maeneo ya Singida hadi Nzega kwa barabara ya kati...
 
Hata maeneo ya Same wapo wa aina hiyo.

Unaona taa moja unadhani pikipiki kumbe ni trekta.

Wengine unaona kichuguu kinatembea kumbe gari imetoka porini kubeba mazao.

Mara nyingi usiku magari yasio na vibali ndo yanatamba.
 
Kikusya

Senior Member
Oct 2, 2011
167
250
Usiku achana nao kabisa, mimi nilitoka Mbeya jioni, Kipindi kile mafuta ya shida sana. Nilipofika Morogoro ilibidi nizunguke sheli mbili pale msanvu ili niongeze mafuta. Nilipojaza tu nikaendelea na safari kuelekea Dar nikiwa peke. Kilichonishtua kwamba hii siyo kuelekea Dar, ni kibao pembeni kimeandikwa mto wami, hicho kibao sijawami kukiona njia ya Dar. Ikabidi nigeuze haraka kuelekea nilikotoka na kulala ndani ya gari pale Msamvu. Asubuhi na mapema nikanyanyuka huyo kuelekea Dar. Njiani niliona ajari ya gari dogo mbaya sana, yaani gari imebaki kama chapati. USIKU MI BARAA MINGI. Malori mabovu, matreka ndiyo muda wa kujidai.
 
Kikusya

Senior Member
Oct 2, 2011
167
250
usiku raha ,shida kuna wengine giza likiingia hawaon vizuri
Safari za usiku nzuri hujapatwa na janga kama breakdown nk

Nilikuwa nikisafiri usiku, siku moja porini kabisa hakuna watu bearing za nyuma zika jam. Sijawahi safiri tena usiku.

Pia niliwahi nusurika maeneo ya dakawa kupigwa na roli, nalipisha linajaa tu kwangu kesha vuka mstari wa kati unaotenganisha barabara.

Lakini pia usiku usisafiri kama gari yako haina beam ya kutosha taa za mbele. Barabara zetu ni mbovu sana hata za lami. Kukuta shimo katikati ya barabara ni kawaida sana

Mwaka 2013, baada ya kuvuka sekenke kutafuta vijiji vinavyofuata, almanusura na ingekuwa usiku pale na gari haina taa zenye mwanga, leo ningekuwa nishaihama Dunia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa, Usiku ni balaa. Huyu jamaa hii mada sijui anatafuta kuungwa mkono?
 
Kikusya

Senior Member
Oct 2, 2011
167
250
Nakumbuka kuna siku tulikuwa tunawahi harusi kesho yake. Tukatoka Mwanza saa 12 jioni ili tuingie Dar saa 2 au 3 asubuhi.

Kwenye gari kila mtu alilala, tukabaki mi na dereva tu tunapiga story.

Tukafika maeneo ya tabora nadhani igunga sijui mida ya saa 5 usiku, kitu kimewaka moto.

Hamadi kuna lorry kama mita 50 limezima kati ya barabara na halijaweka alama yeyote. Uzoefu wa dereva ulituokoa lasivyo tusingekuwa duniani leo.

Tulivyofika manyoni mida ya saa 7 hivi tukaamua kulala tu. Hatukuona sababu ya kuwahi tena mjini.

Safari za usiku zinahitaji chombo na dereva imara.
Kweli kabisa, nimewahi kutoa ushauri humu kwamba, ukiona kuna ulazima wa kusafiri usiku basi hakikisha unawasha taa kubwa zote na mwendo usizidi 50km kwa saa. Nimewahi kufanya hizi safari mara mbili si kwa kupenda. Moja nikiwa peke yangu na nyingine nikiwa na familia yangu. Yaani ajali ni nje nje. Hii spidi 50km kwa saa ilinisaidia kusima ghafla pia ilinisaidia kwenda nje ya barabara pindi malori yaapotanua barabara yote.
 
Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
54,558
2,000
Safari ya usiku hapana binafsi. Kama macho si mazuri, mara umepata dharura au mnyama anakatiza barabarani.

Habari za miaka BelindaJacob

Kuna safari moja almanusura aliyekuwa anatuendesha agonge tembo Mikumi hiyo, usiku mnene tembo anatoka upande huu anaenda upande wa pili...

Kama sio kumshtua, pengine yule tembo angelituletea balaa, kwanza kwa kujeruhiwa na pili faini ya tembo sio ya kitoto...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom